IGP: Polisi mnaweza kufanya kazi zenu mkiwa marafiki wa Raia wema!

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
Jana ilitokea ajali ya polisi kupinduka na gari na wengi waliumia na wengine hali si ya kuridhisha. mmoja amekufa ! RIP.

Nimesikitika sana na sijapenda reaction ya wananchi niliowashuhudia around. Wote, wote walikuwa wanashangilia na kutoa negative sympathy kwa majeruhi.

Sijapenda. Ukiwauliza kwanini mnakuwa "wanyama" wanasema polisi wanawaonea raia ngoja Mungu awalipie.

Kama kuna polisi wanakiuka miiko/miongozo ya kazi zao, hao ni kidogo, wengi ni wazuri, tuwaombee mema katika kazi zao.

Nina uhakika polisi wanaweza kufanya kazi nzuri wakiwa marafiki wa raia wema. Tujitahidi tuwe marafiki wa Raia!
 
Hizi ni ndoto za alinacha.

Siyo Siri hata kidogo, Polisi na Tiss ndio Maadui wakubwa zaidi wa Usalama wa Umma hapa Tanzania kwa Sasa.
Hili lipo wazi kabisa, Wala hakuna kificho, ushahidi wote kabisa upo wazi.
Chuki ni kubwa sana kupita kiasi katika jamii dhidi ya Watu hao

Vitendo vya Utekaji, uporaji, Utesaji, kubambikia Watu Kesi za uongo na Mauaji ya makusudi kiholela dhidi ya raia wema ndio chanzo kikuu Cha kuibuka kwa Chuki kubwa sana Kati ya raia wema dhidi ya Polisi na Tiss
 
sijakupata

Siyo Siri hata kidogo, Polisi na Tiss ndio Maadui wakubwa zaidi wa Usalama wa Umma hapa Tanzania kwa Sasa.
Hili lipo wazi kabisa, Wala hakuna kificho, ushahidi wote kabisa upo wazi.
Chuki ni kubwa sana kupita kiasi katika jamii dhidi ya Watu hao.
Vitendo vya Utekaji, uporaji, Utesaji kubambikia Watu Kesi za uongo na Mauaji ya makusudi kiholela dhidi ya raia wema ndio chanzo kukuu Cha kuibuka kwa Chuki kubwa sana Kati ya Polisi na Tiss dhidi ya raia.
 
😆😆😆😆😆

Screenshot_2025-08-13-01-21-48-1.png
 
Hizi ni ndoto za alinacha.

Siyo Siri hata kidogo, Polisi na Tiss ndio Maadui wakubwa zaidi wa Usalama wa Umma hapa Tanzania kwa Sasa.
Hili lipo wazi kabisa, Wala hakuna kificho, ushahidi wote kabisa upo wazi.
Chuki ni kubwa sana kupita kiasi katika jamii dhidi ya Watu hao
sahihi, nimeandika kwa code, soft language
 
sawa kuna wabaya kabisa, lkn wengne ni wazuri

Polisi wazuri na wema ni wachache Sana kupita kiasi, wengi wao ni wabaya na Waovu. Hao Polisi wazuri na wema wengi wao wanapigwa Vita vibaya sana na Mapolisi wenzao ambao ni Waovu.

Tambua ya kwamba, Uovu, udhalimu na Uhalifu ambao umekuwa ukifanywa na Watu hao hauchagui cheo Cha mtu, itikadi za Vyama, makabila, au kigezo kingine chochote kile. Hata wao kwa wao pia wamekuwa wakifanyiana Uovu, Polisi wanaolengwa zaidi na Uovu wao ni wale baadhi ya Askari Polisi wachache ambao ni Waadilifu, Wapenda Haki na kupinga uonevu na udhalimu. Rejea tukio la Mauaji ya makusudi ya yule Mfanyabiashara wa Madini kule Mtwara, yule Askari Polisi aliyekuwa Muadilifu na aliyefichua Mauaji yale wenzake (wakubwa wake) walimkamata na kumuweka rumande kwenye Kituo Cha Polisi, na ilipofika mida ya usiku yule Askari Polisi aliuawa kwa kunyongwa na kisha watekelezaji wa tukio hilo asubuhi walitoa taarifa kwa umma kwamba eti Askari Polisi huyo alijinyonga kwa kutumia dekio akiwa katika Mahabusu ya Polisi. Nafikiri utakuwa unalikumbuka vizuri tukio hili.
 
Huu uadui sio mzuri,sio kila polisi ni mbaya au mla rushwa au mkatili.Hata hao usalama,mbona wanafanya mengi mazuri tuwe makini na hizi chuki sio nzuri kwa taifa ukizingatia Tanzania tunaoa na kuolewa kila mahali bila kujali kabila.Sasa utajuaje kwamba ndio unamwacha shemeji yako au mjomba wako afie kwenye ajali kwa vile ni polisi.
 
Hii inanikumbusha kuhusu afande Lugola, mdogo wake Kangi Lugola alivyokuwa anapiga rungu kwa nguvu wananchi kana kwamba anaua nyoka pale Kisutu, kwa "kosa" la kwenda kuhudhuria kesi ya Lissu
 
Hujawahi ingi
Huu uadui sio mzuri,sio kila polisi ni mbaya au mla rushwa au mkatili.Hata hao usalama,mbona wanafanya mengi mazuri tuwe makini na hizi chuki sio nzuri kwa taifa ukizingatia Tanzania tunaoa na kuolewa kila mahali bila kujali kabila.Sasa utajuaje kwamba ndio unamwacha shemeji yako au mjomba wako afie kwenye ajali kwa vile ni polisi.
Hujawahi Ingia kwenye 18 za Police wewe tena innocently. Hawana huruma kabisa. Kwao kila tukio la Raia ni mtaji.
 
Huu uadui sio mzuri,sio kila polisi ni mbaya au mla rushwa au mkatili.Hata hao usalama,mbona wanafanya mengi mazuri tuwe makini na hizi chuki sio nzuri kwa taifa ukizingatia Tanzania tunaoa na kuolewa kila mahali bila kujali kabila.Sasa utajuaje kwamba ndio unamwacha shemeji yako au mjomba wako afie kwenye ajali kwa vile ni polisi.
Endapo kama ungeyajua mambo yao kwa undani zaidi basi naamini kwamba usingeweza kuandika comment yako hii.
 
Back
Top Bottom