dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Salaam,
Ni kweli bila Polisi hakuna utii wa Sheria.
Ila Kitendo cha Polisi kujipendekeza kwa Wanasiasa ili wasifiwe au wapewe vyeo vya kisiasa ni kuwaonea wananchi.
Ni kweli Polisi wanapambania matumbo yao, ila hili la kuzuia wafanyabiasha na Wasafiri kuchelewa kufika kisa kiongozi wa kisiasa anahutubia si sahihi.
Muleba Mkoani Kagera, Polisi wamezuia Magari kwa Masaa matatu kusubiri Makonda ahutubie na kupita. Kuna Magari ya Mafuta, sumu, wagonjwa na wengine wanawahi Bukoba Airport. Eti wakapaki Magari katika ya barabara kama rais anavyofanya.
Tunaomba Polisi Msirudie tena. Tumeteseka.. Watu tumekesha ndani ya basi halafu unazuiliwa kupita ukapumzike kisa mwanasiasa wa chama.
Uchumi utakua vipi jamani? Tupendane. Siasa zifanyike kwa ustaarabu bula kuharibiana ratiba. Si wote wanafuatilia Siasa.