IGP Simon Sirro afanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi

IGP Simon Sirro afanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi

Ni dhahiri kwamba polisi kwa sasa wanapaswa kutenganishwa zaidi kama ilivyokuwa zamani kwenye kuendesha mashtaka mpaka walipoondolewa hiyo power.

Hii ya kuchunguza pia waondolewe iwe no Agency inayojitegemea ili haki itendeke.

Mtu anayekukamata ndio anakupeleleza hii sio sawa anaweza kuamua kukuwekea ushahidi wa kubambikia ilimradi akukomeshe tu.

Anayepeleleza jinai watoke kwa DCI na wasiingiliane kiutawala kabisa. Anayekamata alete ushahidi, anayechunguza adhibitishe kama kuna kosa na huo ushahidi ni wa kweli then wapeleke kwa DPP ili apeleke mahakamani.

Hapo kila mmoja atakuwa na sehemu yake ya utendaji na itakuwa rahisi sana kujua nani hafanyi kazi kwa haki.

Hapa karibuni kulikuwa na malalamiko mengi sana kwamba DPP hatendi haki Mahakamani jambo ambalo sio la kweli.

DPP huletewa ushahidi na polisi waliomkamata mtu wanayemtuhumu ni muhalifu. DPP kazi yake ni kwenda mahakamani kusimama kwa niaba ya Jamhuri Ila yeye hahusiki popote zaidi ya kuletewa malalamiko na mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi.

Naelewa itatengeneza gharama katika kufungua ofisi za public investigation kila mkoa na wilaya Ila ili tuweze kutengeneza misingi ya haki ni bora kuwaachia wahalifu 100 kuliko kumfunga mwenye haki mmoja tu kwa uzembe .

Na wakifungua hizi ofisi za public investigation pia waruhusu private investigation ili kuwa na option ya upelelezi sio kutegemea polisi pekee ambao nao wanaweza kukwama kwa sababu mbalimbali.
DCI bado ni Polisi,Nakubaliana na Mawazo yako kuwa Crime Investigation Dept. iwe tofauti na Polisi, ili unapokamatwa na charges zako waje separate independent agency(Iwe Crime Investigation Dept) wachunguze/wapepeleleze na kukusanya ushahidi, na kama umekamtwa na Ushahidi red handed pia ushahidi uchunguzwe kama kweli umekamatwa nao au umebambikiziwa ndipo upelekwe mahakamani, hii inaweza kupunguza mambo ya kubambikiziana kesi na kufungana pasipo makosa, Lakini pia itapunguza hucheleweshaji wa kesi, kuna kesi nyingine zinakwenda mahakamani pasi na ushahidi halafu matokeo yake zinatajwatajwa bila kusikilizwa na kufutwa, haya ni matumizi mabaya ya muda na rasilimali za mchi na usumbufu kwa raia.
Hii ya PrIvate investigation sio mbaya endapo tu naye itawekewa mipaka ya ushahidi wake, na pia Mhakamani wawe kama mashaidi.
 
mkuu polisi kama zilivyo taasisi nyingine inakabiliwa na ufanisi wa mtendaji wa mtu mmoja mmoja.
mbaya zaidi ni kwamba yenyewe inahitaji watu walio commited kufanya kazi hiyo zaidi kuliko cheo.

usidhani vyeo ndio utendaji,wakati sirro anapokea jeshi kwa mangu lilikuwa ktk mfumo huo unaozungumzia,akagundua ufanisi uko chini baada ya wengi kuwa watu wa kujitizama mabega zaidi,field wanatuma watu tu,akabadili.angalia rpc kanda maalumu sasa hivi,kalingana vyeo na wadogo zake wote ACPs,na kila mkoa unao watatu,RPC,STAFF OF,OPP OF.

kwao wao sio ishu maana unaweza amka ukajikuta umekuwa OCD liwale,kutokea RCO ilala.ukiishafikia cheo cha afisa hauna hatimiliki na kitengo,muda wowote kinanuka.

Kumbe ni halali wanachofanyiwa kama ndio ilikuwa mtindo wao kutuma tuu watu badala ya kufika wenyewe field
 
DCI bado ni Polisi,Nakubaliana na Mawazo yako kuwa Crime Investigation Dept. iwe tofauti na Polisi, ili unapokamatwa na charges zako waje separate independent agency(Iwe Crime Investigation Dept) wachunguze/wapepeleleze na kukusanya ushahidi, na kama umekamtwa na Ushahidi red handed pia ushahidi uchunguzwe kama kweli umekamatwa nao au umebambikiziwa ndipo upelekwe mahakamani, hii inaweza kupunguza mambo ya kubambikiziana kesi na kufungana pasipo makosa, Lakini pia itapunguza hucheleweshaji wa kesi, kuna kesi nyingine zinakwenda mahakamani pasi na ushahidi halafu matokeo yake zinatajwatajwa bila kusikilizwa na kufutwa, haya ni matumizi mabaya ya muda na rasilimali za mchi na usumbufu kwa raia.
Hii ya PrIvate investigation sio mbaya endapo tu naye itawekewa mipaka ya ushahidi wake, na pia Mhakamani wawe kama mashaidi.
Sahihi sana mkuu, hii ya private investigation ipo sema hawajaiweka vizuri zaidi Ila wapo but ndio akina Mahindi ambaye aliwahi kuwa IGP.

Ikitungwa sheria itasaidia, nimefanyia research kwa kuangalia marekani inasaidia sana kumaliza kesi mapema na kutoa haki.

Hawa private investigator huwa wanaweza kuwa hired na serikali kwenye kesi fulani ambazo Wana utaalamu nazo na unakuta wamebobea zaidi.

Inasaidia kumaliza kesi.
 
Hujanielewa umesoma halafu hukutaka kuelewa maana yangu anyway sawa boss umekuja kutafuta umaarufu kwa kunisagia kunguni kwa yote ya maana niliyoandika. Umechukua neno moja ukajisokotesha ufahamu wakati ulipaswa kusoma sentensi nzima bila kuacha neno.
pole mkuu kama nimekukwaza ha ha ha ha take it easy enjoy life
 
Sahihi sana mkuu, hii ya private investigation ipo sema hawajaiweka vizuri zaidi Ila wapo but ndio akina Mahindi ambaye aliwahi kuwa IGP.

Ikitungwa sheria itasaidia, nimefanyia research kwa kuangalia marekani inasaidia sana kumaliza kesi mapema na kutoa haki.

Hawa private investigator huwa wanaweza kuwa hired na serikali kwenye kesi fulani ambazo Wana utaalamu nazo na unakuta wamebobea zaidi.

Inasaidia kumaliza kesi.
sio mahindi ni IGP mahundi marehemu
 
sio mahindi ni IGP mahundi marehemu
It's just clerical error, bado upo nami tu🙆🏼‍♀️🤷hujataka kusoma kila kitu. Namjua maana hata chuoni CCP/MPA kuna bweni Lina jina lake so naelewa almost kila kitu I've been there and done it mwaka 2009.
 
Mkuu Kilwa94 nimeuliza hivyo ili nijue ni nani hasa anaepanga wa kuu wa vituo hivya chini ndani ya wilaya.

Kuna mkuu wa kituo cha Mtibwa ni mpemba "mla urojo" aliletwa kituo hiki akitokea Zanzibar. Alibadilishana vituo na mkuu wa awali aitwae Zayumba.

Sasa tangu afike kituo hiki hakuna mabadiliko yoyote uharifu mtaani umerudi upya, vijana wetu wanaporwa pikipiki na kuuawa kikatiri, rushwa pale kituoni imekithiri mahabusu hawapati haki zao za msingi.
Mtu unakamatwa na kuswekwa rumande wiki nzima bila hata chukuliwa maelezo.
Kesi za vibaka ndo za kupelekwa mahakamani.

Ukiombwa rushwa ukatoa haraka dau linapanda hata mara tatu make unaonekana una hela nyingi.
Wafugaji wavaa mashuka ndo wahanga wakuu wa rushwa.

Tunaomba mamlaka za uteuzi na wanaopanga wakifumue kituo cha mtibwa.
Pale kuna polisi wawili Baraka na Dulla waondolewe haraka sana ndo wamemshika mkuu kwa hela ya rushwa.
Pale kituoni kwa wk wachukua rushwa hata zaidi ya mil30! Imagine hizo hela zinatoka kwa wakulima watu kipato cha chini.
nimekusikia kijana.
jumatatu nitakua hapo madizini
nitakutafuta

na ahidi kuyafanyia kazi haya yote uliyo andika hapa.
 
Back
Top Bottom