IGP Simon Sirro afanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi

IGP Simon Sirro afanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi

Mkuu Kilwa94 nimeuliza hivyo ili nijue ni nani hasa anaepanga wa kuu wa vituo hivya chini ndani ya wilaya.

Kuna mkuu wa kituo cha Mtibwa ni mpemba "mla urojo" aliletwa kituo hiki akitokea Zanzibar. Alibadilishana vituo na mkuu wa awali aitwae Zayumba.

Sasa tangu afike kituo hiki hakuna mabadiliko yoyote uharifu mtaani umerudi upya, vijana wetu wanaporwa pikipiki na kuuawa kikatiri, rushwa pale kituoni imekithiri mahabusu hawapati haki zao za msingi.
Mtu unakamatwa na kuswekwa rumande wiki nzima bila hata chukuliwa maelezo.
Kesi za vibaka ndo za kupelekwa mahakamani.

Ukiombwa rushwa ukatoa haraka dau linapanda hata mara tatu make unaonekana una hela nyingi.
Wafugaji wavaa mashuka ndo wahanga wakuu wa rushwa.

Tunaomba mamlaka za uteuzi na wanaopanga wakifumue kituo cha mtibwa.
Pale kuna polisi wawili Baraka na Dulla waondolewe haraka sana ndo wamemshika mkuu kwa hela ya rushwa.
Pale kituoni kwa wk wachukua rushwa hata zaidi ya mil30! Imagine hizo hela zinatoka kwa wakulima watu kipato cha chini.
Daah! hili ni jambo la kulipinga wazi wazi,natumai polisi wamo humu watachukua hatua.
 
Nauliza tu Askari wa magereza anaweza kuwajibishwa na OCD endapo atafanya kosa?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Yeah!sheria inachukua mkondo wake hata hawe na rank gani akifanya jinai kubwa,OCD anaweza toa amri ya ukamataji wa mtuhumiwa.Ipo hivyo afisa wa jeshi lolote anaweza wajibishwa na polisi kwa mujibu wa sheria.Ila hawa wavaa magwanda wanabebana sana.
 
Yeah!sheria inachukua mkondo wake hata hawe na rank gani akifanya jinai kubwa,OCD anaweza toa amri ya ukamataji wa mtuhumiwa.Ipo hivyo afisa wa jeshi lolote anaweza wajibishwa na polisi kwa mujibu wa sheria.Ila hawa wavaa magwanda wanabebana sana.
Wanajeshi au?
 
yes! naposema afisa simaanishi maafisa wa vyeo vya juu.Hawa wa ranks za chini nimewashuhudia mara nyingi wakikumbwa na madhila ya kukamatwa na polisi.
Wanakunywa bar hawalipi
 
Nipe darasa kidogo kuhusu RCO na RTO... nani bosi? Je RTO anaweza kuwa RCO and vice versa?

Bosi wa usalama barabarani Tanzania anapopelekwa kuwa RPC Morogoro.. inakuwa demotion au promotion?
RCO anaweza kulingana cheo na RTO kwakuwa hivo ni vyeo vya ki utawala tu. Hivo hakuna Boss kati yao, ndio RTO anaweza kuwa RCO
 
Mi namshauri Afande IGP kuweka Ma RCO wa rank ya ACP maana kwa kweli ma RCO kuwa na rank sawa na MaOCS kwa kweli Dah! OCD kuwa SSP sawa ila SSP kuwa RCO dah!
mkuu polisi kama zilivyo taasisi nyingine inakabiliwa na ufanisi wa mtendaji wa mtu mmoja mmoja.
mbaya zaidi ni kwamba yenyewe inahitaji watu walio commited kufanya kazi hiyo zaidi kuliko cheo.

usidhani vyeo ndio utendaji,wakati sirro anapokea jeshi kwa mangu lilikuwa ktk mfumo huo unaozungumzia,akagundua ufanisi uko chini baada ya wengi kuwa watu wa kujitizama mabega zaidi,field wanatuma watu tu,akabadili.angalia rpc kanda maalumu sasa hivi,kalingana vyeo na wadogo zake wote ACPs,na kila mkoa unao watatu,RPC,STAFF OF,OPP OF.

kwao wao sio ishu maana unaweza amka ukajikuta umekuwa OCD liwale,kutokea RCO ilala.ukiishafikia cheo cha afisa hauna hatimiliki na kitengo,muda wowote kinanuka.
 
Back
Top Bottom