Mkuu
Kilwa94 nimeuliza hivyo ili nijue ni nani hasa anaepanga wa kuu wa vituo hivya chini ndani ya wilaya.
Kuna mkuu wa kituo cha Mtibwa ni mpemba "mla urojo" aliletwa kituo hiki akitokea Zanzibar. Alibadilishana vituo na mkuu wa awali aitwae Zayumba.
Sasa tangu afike kituo hiki hakuna mabadiliko yoyote uharifu mtaani umerudi upya, vijana wetu wanaporwa pikipiki na kuuawa kikatiri, rushwa pale kituoni imekithiri mahabusu hawapati haki zao za msingi.
Mtu unakamatwa na kuswekwa rumande wiki nzima bila hata chukuliwa maelezo.
Kesi za vibaka ndo za kupelekwa mahakamani.
Ukiombwa rushwa ukatoa haraka dau linapanda hata mara tatu make unaonekana una hela nyingi.
Wafugaji wavaa mashuka ndo wahanga wakuu wa rushwa.
Tunaomba mamlaka za uteuzi na wanaopanga wakifumue kituo cha mtibwa.
Pale kuna polisi wawili Baraka na Dulla waondolewe haraka sana ndo wamemshika mkuu kwa hela ya rushwa.
Pale kituoni kwa wk wachukua rushwa hata zaidi ya mil30! Imagine hizo hela zinatoka kwa wakulima watu kipato cha chini.