IGP Simon Sirro, kwanini askari polisi wanatumwa field na silaha nzito wamevaa kiraia? Kwanini unatuma askari na silaha nyingi tukio dogo la kiraia?

IGP Simon Sirro, kwanini askari polisi wanatumwa field na silaha nzito wamevaa kiraia? Kwanini unatuma askari na silaha nyingi tukio dogo la kiraia?

Ni jambo ambalo linazidi kuenea Tanzania. Mara nyingi unakuta askari polisi wanatumwa kwenye tukio linalohitaji silaha (japo ni machache Tanzania) huku wakiwa wamesheheni silaha na bado wamevaa kiraia. Kwa nini wanafanya hivyo? Je inaruhusiwa kwa askari polisi aliye kwenye response unit kwenda akiwa na silaha kamili za kuingia filed lakini akawa amevaa kiraia?

Nimeangalia askari walioenda kumkamata huyu mama wa Iringa alietoroka kambi ya Corona, na karibu askari wote walioenda walikuwa wamesheheni silaha lakini wamevaa kiraia.

Halafu, hili tukio si la ujambazi. Kwa nini Polisi wapeleke kikosi chenye uzito wa silaha kiasi hiki kumkamata mwanamke mmoja aliekimbia kambi ya Corona? Hivi polisi wetu wanawashwa kubeba silaha na kuzitumia?

Nchi haiko vitani, unapeleka kikosi cha polisi kumkamata mwanamke mmoja aliyetoroka kambi ya Corona utafikiri unaenda kumkamata kiongozi wa Al-Qaeda, Unataka kumtisha nani na askari wako na silaha zao, wananchi wa Tanzania?

Unapeleka askari na silaha kwenye tukio dogo kama hili utafikiri huyo mwanamke ndio Corona yenyewe unaenda kuikamata! Mkitukanwa mnatumia nguvu badala ya busara mnalalamika. Hii display ya force kwenye tukio kama hili inawasaidia nini hasa? Polisi badilikeni. Mnatuaibisha.

Siku moja askari wako wenye silaha na wamevaa kiraia watakuja kuuwawa wakidhaniwa ni majambazi.

View attachment 1407862

View attachment 1407865
Ohooo!!! Mukuu acha kutikisa muzinga wa nyuki. Kwani ukijikalia kimya unakosa nini?
 
Kama kuna askari huko uliko anamiliki nyumba ya kifahari, gari la kifahari, au biashara halali kubwa nyoosha kidole.
Unafikiri hawavitamani?
Hapo ndio stress huanzia.
Akikuona mwana unakatiza kitaa na harrier yako anatamani ugonge hata kuku akuonyeshe yeye nani.
 
Acha povu bwanamdogo PGO ni Police General Orders. Hivyo ulikuja na hamaki kwa kulaumu ufavaaji huo, kana kwamba kwenye PGO wamevunja kifungu.
Ndio kusema nakutaka kukufunda kabla hujalalamika suala ambalo hulifahamu jitahidi ufahamu nalo kabla ya kutoa lalamiko.

Lalamiko ni hitimisho kwamba walikosea kwa mujibu wako, by theway nisamehe hapo juu kama nilitumia lugha mbaya.
Polisi wajinga tu. mibunduki ya nini kwenda zako na ujinga eti PGO
 
Watanzania tuna matatizo sana.kujifanya wajuaji
Mtu mmoja anaweza kuambikza watu.800 ndani ya dakika 5 tu halafu.unasema.nchi haiko vitani
Hujui polisi wanafanya

vipi.operesheni.zao kwa hiyo kaa kimya tu
Kwa mfano imepigwa redio kwamba kuna mtu hatari ametoroka na.ana corona.yupo iringa sokoni,maana.yake gari yoyote ya patrol ilio karibu incharge .wake.ndio.atakua wa kwanza kufika,bila ya kujali wamevaa vichupi au wana mishale,watakama tu

Sijui ulitaka wazitupe kwanza bunduki,wavae sare ndipo,wakakamate huyo mueneza corona.halafu warudie bunduki?
Yoyote anaeneza corona.kwa makusudi ni wa kuuwa kama panya tu
Ujinga tu. MTU mwenye korona anakamatwa kwa bunduki au, anakamatwa na wauguzi waliovalia rasmi kujikinga na korona
 
wewe mama acha visa.

umeshawahi shuhudia ukamataji wa polisi eneo lolote,ukafanikiwa bila pingamizi???

huku mtaani tuna usela mavi sana wa kujifanya wapigania haki tusizozijua,visa kibao vya polisi kudhulika ama kushindwa kutekeleza majukumu yao vimeripotiwa.na nyinyi humu ndio wa kwanza kubeza.

zile silaha sio kwa ajili ya mauzo zinapiga kweli.


Sent using Jamii Forums mobile app
We Una cheo gani ? Ulipata div. gani?
 
Acha uongo,askari wote wanapaswa kuvaa uniform na kuwa na kitambulisho.
Ina maana gani kutovaa uniform halafu umebeba silaha?
Tatizo labda iwe hizo silaha ila sio nguo.
Hao askari wa idara ya upepelezi, ambao kimajukumu hawavai uniform.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini raia waingilie kuzuia asichukuliwe?
Umewahi kufuatilia visa ambavyo raia wanaingilia kuzuia mtu asichukuliwe?
Hata wewe mwenyewe ungejiuliza maswali mengi,kwa huyo mama ni tofauti kabisa kwa sababu ametoroka karantini.
What if raia wakaingilia kuzuia Sichukuliwe hujaona mapambano ya namna hii katika nchi nyingine..?



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini kitumike kikosi cha kupambana na Ujambazi katika tukio linalohusisha ugonjwa?
Pole Mwananchi Mwenzngu kwa upeo mdogo juu ya jambo hili.
Hicho ni kikosi cha kupambana na Ujambazi na dharula zote hivyo muda wote wanatembea wakiwa kamili kupambana ndiyo maana hata ukisikia Mtoto katupwa jalalani watakuja hivyo hivyo na hizo ndizo Laptop zao. Hiyo miwatu inaitwa Ant Robbery ni moja ya vitengo ndani ya Idara ya Upelelezi na ndiyo maana wakifika eneo la tukio wanakusanya Mpaka vielelezo na kuhoji Mashaidi. Hao ndiyo watu wa Mwanzo wanaojenga kesi au kuibomoa. Kwa ufupi ni watu wenye Nguvu za kupambambana kibunduki na kiakili na Shule yao imeelemea kwenye Upelelezi .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo wa utoaji huduma wa askari wetu ndio matokeo yake sio wao
Askari wa Tz ni ngumu kuongea vzr na mtuhumiwa na huwa na culture ya wao kutak kuonekan wako juu katk Taifa hili kuliko binadamu wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaaaaaaa. Wewe mbumbumbu umepewa sababu kwanini wapo kiraia, kuwa wapo idara ya Upelelezj, wazako wamehoji juu ya silaha umeambia kwa dharula yoyote iitakayojitokeza. Mmoja kahoji Corona ni Dharula niemueleza nidharula kubwa Sana. Kuna kauliza kuna ulazima gani kwenda na silaha nzito/kubwa nikamueleza ndiyo moja ya vitendea kazi vyao. Kulikuwa na ulazima gani kiende kikosi kile. Wait walipewa kieneo hicho kumtafuta anayehisiwa Mgonjwa maana hata Sasa wewe unataka iende Ambulance umesahau kuwa amekataa kutii shetia bila shuruti. Maana aliambiwa akae karantini ametoroka. Lijitu hata kufikkuri kwanini ametoroka?. Hali za hao askari zitakuwaje baada ya kumamata Hugo mtu. Je wananchi wrnye hasira kali wangefanya nini juu ya Mtu anayetaka kusambaza virusi. Unawaza silaha zao ukasahau Kabisa kuwa Afrika mashariki sisi ndiyo Nchi pekee hgatupo katika Vita ya bunduki kwasababu ya Mifumo ya ulinzi wa Nchi. Kwa upande wangu nawapongeza hao Mapolisi kwa kazi nzuri waliofanya. Sasa kama wewe ungekuwa IGP sijuk ungetuma kikosi gani kumkamata ambacho hakitembei na bunduki. i

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ni Maelezo ya MTU aliyeshindwa shule
 
Sasa huko wameenda kupeleza kitu gani? Uliona askari anaenda kupeleleza kajivalisha mibomu ya machozi kama hana akili sawa?

Askari wawili wenye SMG walitosha kabisa, na hata bila kuwa na silaha isingekuwa tatizo. Hata mmoja, kwa sababu hili sio tukio ambalo lingeweza kuleta vurugu.

Au labda huyo mwanamke ni mwanachama wa Chadema!
Hao wanazingua ilitakiwa kikosi kidogo tu cha wana intelejensia wanamnyakua wanatoweka nae kimykimy kutishana2 bila sababu za msingi
 
Mtoto ni wewe. Mie natumia busara ya kawaida katika mazingira ya Tanzania. Sasa ukiniletea term zenu za polisi na mimi sio polisi unategemea nini? Na mimi nikikuletea terms za kazi yangu nitegemee utanielewa? Ndio maana mnaambiwa jaribu kutumia akili kidogo.Sihitaji kujua P.G.O sijui kuelewa upumbavu na ujinga unaojionyesha hapa. Hizo P.G.O mbona mkiitwa kwenye tukio la ujambazi mnazisahau?
Yeye ndio atufafanulie hizo PG0 ndio dudu gani?
 
Tatizo ni kuto kujua silaha nzito na nyepesi ni zipi! Mambo ya kipolisi nadhani yana elimu yake kama mimi na wewe hatujasomea elimu hiyo hatuna haki ya kukosoa utendaji wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom