IGP Simon Sirro: Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara

IGP Simon Sirro: Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
857
Reaction score
2,241
INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema, magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoa wa Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji.

“Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji,” amesema IGP Sirro aliyekuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020.

IGP Sirro amesema, “tumefuatilia baadhi ya watu, wamekamatwa na wengine ni wa kwetu hapa tumewakamata tunaendelea kuwahoji.”

“Ukifanya uhalifu Tanzania na damu ya Mtanzania haiwezi kwenda hivi, waliofanya mauaji wengine wamerudi Msumbiji na wengine tumewakamta.”

IGP Sirro amesema, “tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa.”

Mkuu huyo wa jeshi amesema, watahakikisha wanakamatwa iwe wanakwenda Msumbiji, Kenya au kwingineko ili “mwisho wa siku haki itandendeka na watakamatwa na kupelekwa mahakamani.”

Soma pia > Tetesi: - Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...
 
Hivi hiyo idadi ya magaidi 300 ni kama platoon ngapi? Basi kwa idadi hiyo ya magaidi tena ikiwa ni kama walikuja kutesti zali tu tujihesabu kwamba hatuko salama kabisa. Kuna makubwa zaidi yanaweza kuwa yanakuja.
 
IGP Simon Sirro amesema magaidi "wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya- Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbakli ikiwemo mauaji.

Baadhi wamekimbia na wengine tumewakamata tunaendelea kuwahoji ili kuupata mtandao wote ulioanzia Kibiti na Rufiji.

Chanzo: MwanahalisiDigital
Walawitiwe ikiwezekana, hadi wataje aliyewatuma nani
 
Hapa bado kuna wale wanaoshindwa kufikiria nje ya box,wao kila kitu ni siasa watakuja kuponda utazani wanaishi nje ya Tanzania au labda magaidi wakishambulia watakuwa wanawaachia kisa wao ni wa chama fulani.

Kazi nzuri imefanywa na askari wetu.
 
Atakeye bishia hyo idadi ndiyo gaidi maana anajua fika wakati wanafanya tukio la uvamizi walikuwa wangapi.

Lakini upande wa pili wa shilingi watu 300 wanatoka upande mmoja wa nchi na kuingia upande mwingine wa nchi na kufanya uharifu basi ni wazi mipakani hakuna ulinzi wa kutosha kama tunavyoamini.
 
Back
Top Bottom