IGP Simon Sirro: Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara

Wale jamaa hawajakamatwa hata mmoja, kilichofanyika baada ya tukio askari mtwara walikuwa wanakamata watu ovyo kwa kuhisi.
Wahanga wanasema walikuja kama 80 walivyomaliza ishu zao wakasepa wote, hawa polisi wa bongo kuwaamini inahitaji PhD
Watu 80 wenye silaha wanaweza kuingia bongo na kutoka kirahisi hivyo? Kama ni rahisi hivyo tungekuwa tunashambuliwa kila siku.
 
siasa pembeni usalama wa nchi ni wa muhimu na sina shaka na jeshi la polisi ...hao wanajisumbua tu huko kutaka kuja kutuharibia utulivu wetu, majeshi yetu yapo IMARA sana, kuna wajuba "komandoos" wametulia tu wanasubiria simu tu kama wataitwa waingie kati
 
Watu 80 wenye silaha wanaweza kuingia bongo na kutoka kirahisi hivyo? Kama ni rahisi hivyo tungekuwa tunashambuliwa kila siku.
Ukisema hivyo ina maana hiyo idadi ya magaidi 300 iliyotajwa na Sirro ilitoka wapi au unataka kusema hao wote hawakuvuka mpaka kuja bongo na badala yake walitokea humu humu ndani?
 
Matukio mengi ya kigaidi yanaandaliwa taratibu sio kwa mkupuo kama hivyo, wanaingia wanakaa wanaishi na wahusika na kunakua na ushiriki na watu wa ndani.
 
Nani aliwahesabu hao magaidi?
Mbona hasemi watu wangapi wameuawa?
 
Watu 80 wenye silaha wanaweza kuingia bongo na kutoka kirahisi hivyo? Kama ni rahisi hivyo tungekuwa tunashambuliwa kila siku.
Kaka ungejua kilichokuwa kinafanyika usingebisha, serikali wanaleta siasa unajua kitaya kwenye tukio pakoje, serikali inaleta siasa tu ni ukweli hali ni mbaya sana
 
Mkuu, mi nazungumza kwa mtazamo, lakini kama una ufahamu zaidi wa nini kilifanyika, hata kwa dondoo tuu tufahamishe, taarifa zaidi zinasaidia kuuweka majadala sawa.
 
Pale siasa inapoingia kwenye mambo ya USALAMA.
Yaani habari ya Kitaya Media za Msumbiji ndizo zimeandika vizuri na kwa uwazi.
Semeni watu wangapi wamekufa, mazingira ya ambush, waliingiaje nchini, walitokaje nchini baada ya ambush n.k
 
Atakeye bishia hyo idadi ndiyo gaidi maana anajua fika wakati wanafanya tukio la uvamizi walikuwa wangapi.

Lakini upande wa pili wa shilingi watu 300 wanatoka upande mmoja wa nchi na kuingia upande mwingine wa nchi na kufanya uharifu basi ni wazi mipakani hakuna ulinzi wa kutosha kama tunavyoamini.
Walinzi wako bize kupiga kura za ndio huko Pemba ya Msumbiji ili FRELIMO itawale milele
 
CCM na Mashekhe hawataki kutamka neno haki. SIRO kalitamka ya kuwa haki itendeke bila haki hakuna amani. CC: Slow slow
 
Mkuu, mi nazungumza kwa mtazamo, lakini kama una ufahamu zaidi wa nini kilifanyika, hata kwa dondoo tuu tufahamishe, taarifa zaidi zinasaidia kuuweka majadala sawa.
Nimekusoma, unajua geographical location ya Kitaya imekaa vibaya sana, alaf ni kijiji kikubwa sana.
Kilichofanyika hawa jamaa walizingiria kijiji kizima hakuna kuingia mtu wala kutoka.
Then wengine ndio walikuwa wanafanya umafia ndani ya kijiji, wameondoka na watu vilevile, shortly hali ilikuwa mbaya sana
 
Atakeye bishia hyo idadi ndiyo gaidi maana anajua fika wakati wanafanya tukio la uvamizi walikuwa wangapi.

Lakini upande wa pili wa shilingi watu 300 wanatoka upande mmoja wa nchi na kuingia upande mwingine wa nchi na kufanya uharifu basi ni wazi mipakani hakuna ulinzi wa kutosha kama tunavyoamini.
Ulinzi wote anapewa mtu mmoja, sijui ana adui gani?
 
Back
Top Bottom