Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Watapata taabu sana yaani,tume walimwita Lissu then Lissu akawapiga kifungu kuwa hawezi kwenda kwa kuitwa kwenye mitandao.

Tume wakapeleka barua makao makuu ya chadema kwa bodaboda na kusogeza tarehe ya kumwita mbele halafu Lissu akawapiga kifungu kingine kuwa barua anatakiwa kupelekewa yeye mwenyewe mkono kwa mkono.

Sasa hivi tume wanahaha jinsi ya kumpelekea Lissu barua mkono kwa mkono na siku wakipeleka watakumbana na kifungu kingine.

Huyo IGP atapigwa kifungu simple tu kuwa anatakiwa kupeleka malalamiko yake kwenye tume ya maadili halafu atanywea kama zuzu
 
Sirro wa sasa hivi hamna kitu, Sirro aliyefanya kazi kiweledi ni yule Sirro aliyekuwa RPC Mwanza 2010. Hili jepesi sana kwa Lissu, Lissu atamjibu Sirro na atanywea kama alivyonywea Wilson Mahera Charles. Huyu igp anatest tu.
 
Haya tusubiri tuone, ataenda au atakaidi Amri ya askari wetu?
Wakambebe wakamlaze lockup huku mgombea mwingine ana Nadi Sera zake za ubaguzi huko tunduma, uchaguzi huu umeanza kuvurugwa na tume kwa kuvunja kanuni walizojitungia wao wenyewe.Haiingii akilini tukio LA kiuchaguzi lipelekwe polis badala ya kulalamika tume ya maadili.
 
Lissu asichanganye polisi wa kawaida na wale wa mahakamani wanaobishanaga nao!

Hawa hawaangalii sura!
 
Back
Top Bottom