Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

NEC, police, bado wasiojulikana. Huu mwaka tutaona mengi. Lazima nyoka atoke pangoni.
Hizi ni dalili za nyoka kutoka pangoni. SHINGO IMEGEUKIA KIBLA.
FB_IMG_16014074303386681.jpeg
 
Huyu kada awaambie mapolisi wake waache dabo standard ili wasigombezwe Tena, wakitenda haki hakuna wa kuwagombeza
 
Nyinyi endeleeni kumvimbisha kichwa tu huyo Lissu. Atakapoanza kunyea ndoo mtakaa kimyaa kama wakati ule Faru John ananyea ndoo mlikuwa mbaliii.
Lissu ni rais ajaye wa JMT,mhutu ndo atanyea debe
 
Nyinyi endeleeni kumvimbisha kichwa tu huyo Lissu. Atakapoanza kunyea ndoo mtakaa kimyaa kama wakati ule Faru John ananyea ndoo mlikuwa mbaliii.
Hilo ndilo kimbilio lenu la mwisho. Hamuwezi kushindana kwa haki
 
Safi kabisa,! Lisu asifikiri Beberu wake Amsterdam atamsaidia kwa lolote hii ni chi huru
Kwa hiyo magu na ccm yake,pamoja na kufanya kampeni kwa miaka mitano pekee yao,pamoja na kunadi madaraja,ndege na reli bado hawezi bila msaada wa police,nec na msajiri? No wonder haoni aibu kupigia watoto wa shule ya msingi magoti
 
Tundu Lisu kayataka mwenyewe.
yaaani amekuwa akiwa tukana Askari hadi mimi mwenyewe naogopa!!!
halafu cha kushangaza wakati huo huo anataka ulinzi !! Duh!!
Mkuu kwani police wote ni wajinga?au ndo hivyo mmoja akioza wote wameoza?
 
Tundu Lisu kayataka mwenyewe.
yaaani amekuwa akiwa tukana Askari hadi mimi mwenyewe naogopa!!!
halafu cha kushangaza wakati huo huo anataka ulinzi !! Duh!!
Mjinga sio tusi....
Mpumbavu sio tusi....
kwa mujibu wa sheria.
 
IGP ajue kuwa Jeshi la polisi halina nguvu yoyote juu ya umma!

Jeshi lenye askari wasiofika laki moja nchi nzima litakuwaje juu ya mamilioni ya wananchi wanaomuunga mkono Lissu?

IGP asitutishe!
 
Nilikuwa sina mpango wa kumpigia kura Tundu Lissu kwasabau JPM amefanya mengi yanaonekana. sasa ndio nitampigia Lissu once and for all
Nimewasikia malaika Mbinguni wakikupigia makofi kwa kutoka kwako gizani na kuingia nuruni.nami kwa kukazia nasema waache wafu wazikane
 


Amesema hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa.

Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

"Tundu Lissu hayupo juu ya sheria, tukiamua kutimiza majukumu yetu asilalamike,"IGP Simon Sirro

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, amri hiyo inatokana na IGP kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na matendo mbalimbali ambayo wanayofanya.

Akifafanua suala hili IGP Sirro amesema "Nimeona matukio kadhaa yakifanyika na Viongozi wa Chadema, wamekuwa wakikaripia na kuwagombeza Askari Polisi. Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana na Viongozi wa Polisi".

"Jana nimeongea na Kiongozi wake Bwana Mbowe akae na viongozi wake wazungumze suala la kutii sheria bila shuruti. Anayoyafanya Watanzania wenye hekima na Wazalendo wanaona. Lissu hayuko juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake. Vyama vipo karibu kumi na mbili, Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na Jeshi la Polisi."

"Asije akafika mahali akawa na kiburi akadhani ana uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi. Niwasihi sana na niwaombe sana ndugu zetu wa Chama cha Chadema hii tabia iishe. Tundu Lissu aende akaripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aende akaeleze aliyoyafanya jana. Lakini niwaombe wanasiasa na Viongozi wote katika ngazi zote. Suala la Udiwani, Ubunge, Urais bila amani na utulivu huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe. Kwahiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuchague viongozi tunaowataka lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo viongozi wachache wanayoitaka ili uchaguzi usifanyike. Nawaambia uchaguzi utafanyika lakini itafika mahala tutawashughulikia sana."
View attachment 1587125


Usitufokee, nyooo. Kila ulichovaa hapo ni Kodi zetu. Chako labda ni boxer tu! Na lenyewe, siri yako, hujalifua!
 
Back
Top Bottom