IGP Sirro anasema hawezi kumkamata Askofu Gwajima mpaka apate barua. Je, hivi ndivyo anafanya kwa makundi yote?

IGP Sirro anasema hawezi kumkamata Askofu Gwajima mpaka apate barua. Je, hivi ndivyo anafanya kwa makundi yote?

Askofu gwajima sio wakuzingatiwa ni wakumpuuza tu! Mtu tangia zamani anajulikana ni mropokaji ukibishana nae unajidhalilisha tu! Lakini pia ubunge wake ni kwasababu ya jpm alikuwa anawapenda watu wa aina hiyo. Ccm hawawezi kumfukuza ktk chama kwa kuofia uchaguzi mwingine ila amini nawaambia huyu harudi bungeni 2025
 
Sirro anadharau sana, mi naona tatizo linaanzia kule juu, bora katiba ibadilishwe Rais akifia madarakani nchi irud kwenye uchaguzi

Mtu anatuhumu Viongozi wamepewa hongo kuingiza chanjo means alikua anamaanisha Rais Samia bado ameachwa?

kipindi kile mtu yyte alikua hata akikohoa tu kuhusu JPM anakamatwa, Idris alicheka tu picha ya JPM akakamatwa

lakini Gwajima analiambia kanisa viongozi walioruhusu chanjo akili zao zimeenda kikizo halafu IGP anaongea nini sasa,

mi naona sasa kama vya chanjo tuachane navyo kwanzia leo maana ni kama vile hata Rais hatuna
Wanaccm Hao, angekuwa mpinzani tayari yuko selo siku nyingi
 
Hayupo ambaye hajavishuhudia vimbwanga vya askofu Gwajima kuhusiana na Corona na Chanjo zake.

Hadharani tuhuma za Gwajima kumhusu mheshimiwa Rais na wasaidizi wake zimesikika.

View attachment 1896148

Haya yakiendelea ni kweli kuna watanzania wasio na hatia wanaendelea kuwekwa hatarini kuhusiana na ugonjwa huu.

Sirro anasema hawezi kumkamata Gwajima kwamba yeye hayo anayasikia mitandaoni tu. Kwamba yeye hadi apate makaratasi rasmi na ajiridhishe kama kuna jinai imetendeka.

Hivi ndivyo Sirro anavyofanya kazi kwa makundi yote? Au ndiyo ile sote hatuko sawa mbele ya sheria?

Kwa msimamo wa Sirro na Dkt. Gwajima, mafahali wawili hawa, pana japo mmoja ambaye basi hafai kabisa.

Itapendeza basi mtu akiwajibika au kuwajibishwa japo kwa kadhia hii.
Sirro ni Sukuma Gang na ni jipu.
Atumbuliwe.
 
Imekuwa kawaida kwa viongozi wa vyama vya upinzani kukamatwa kwa maagizo ya mdomo ya 'wakubwa' chamani na Serikalini. Wakubwa wanapochafukwa, huagiza kukamatwa kwa kiongozi huyu au yule wa upinzani au hata wanachama wa kawaida. Kukamatwa lazima kutanguliwe na maagizo.

Waziri wa Afya Dkt. Doroth Gwajima ameagiza kukamatwa kwa Askofu Gwajima kwa kile alichodai kuwa Askofu huyo anaupotosha umma juu ya chanjo ya Corona. Ghafla, akajitokeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro na kutoa kauli. Kauli yake ni kuwa bado hawajapata maagizo ya maandishi ya kumkamata Askofu Gwajima.

IGP Sirro amesema kuwa baada ya kupata maandishi hayo, Polisi watapembua kuona kama kuna jinai au la ili hatua stahiki zichukuliwe. Amedai kuwa maagizo ya Waziri ya kumkamata Askofu Gwajima ameyaona mtandaoni.

Mara ngapi watu wamekuwa wakikamatwa kwa kauli tu za viongozi? Mara ngapi viongozi wa upinzani na wanachama wao wamekamatwa kwa maagizo ya mdomo ya viongozi wa chama tawala na Serikali? Lini na wapi Polisi walisubiri maandishi?

Agizo la kukamatwa lingewahusu Joseph Mbilinyi wa CHADEMA au Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, IGP Siro na Polisi wote wangesubiri maandishi?

Askofu Gwajima akamatwe ili saga liishe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Jamaa Sirro mjanja sana, hataki msala kama wa sabaya wa kupokea tu maagizo ya wakubwa bila official statement kimaandishi.

hii ni nzuri kama akija kupata msala kama sabaya anaonesha evidences za maagizo hayo kimaandishi
 
Sirro anaweza kuwa kundi moja na Gwajima mcheza movie, huko kujidai kwake kutaka barua ni ili amlinde kiaina jamaa yake, kwasababu Sirro kwa tabia zake hajawahi kuwa na ustaarabu huo anaojidai nao sasa.

Kama waziri akiamua kuandika hiyo barua, bado ana sababu za msingi kumshawishi Sirro akamkamate Gwajima.

- Anadai chanjo feki, atatakiwa kuthibitisha.

- Anasema wamepewa hela, athibitishe.

All in all, haya yanatokea kwasababu ya udhaifu wa kiongozi tuliyenaye, ukimya wake uliopitiliza unasababisha kila mmoja huko kwao kujiona yuko juu ya mwenzake.
 
I.J.P ndio Nini kumbe kilaza hivi

USSR
 
Haya maagizo ambayo kila mtu anaweza kutoa kwa vyombo vya dola ni ujinga sana. Hatuwezi kuwa taifa lenye kuamrisha idara za usalama kama unaamrisha nzige.

Waziri aagiza jeshi la polisi,

Naibu Waziri aagiza jeshi la polisi,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Njombe aagiza jeshi la polisi,

Katibu mkuu wizara ya Afya aagiza jeshi la polisi,

Mkuu wa wilaya aagiza jeshi la polisi.

Kila mtu anaweza kuwaagiza maana mmetoka kwenye utumishi wa umma na kuingia kwenye utumishi wa wanasiasa na mali zao.
 
Gwajima ni mfumo ndani ya mfumo sirro hana hadhi ya kumkamata
 
Mimi ninasali na kuomba siku yakitokea ya Zambia asitokee mtu akajifanya eti sijui mlifanya moja mbili tatu ila mimi nasamehe. Ujinga mtupu huu. Ni vyema siku moja kila mtu awajibike kwa matendo yake na matamshi yake

Asante
 
Yaani nchi hii na jeshi hili vilishaharibika kabisa! Kiuhalisia uonevu kwa wapinzani ni mkubwa sana! Wangekuwa ni viongozi wa upinzani hata polisi tu wa kawaida wasingesubiri maagizo ya Sirro!
 
Back
Top Bottom