Tunaishauri mamlaka ya uteuzi wa igp siro immulike huyu mtu kwa makini Sana namna anavyolisimamia jeshi hili inatia Shaka ni Kama anaichonganisha serikali na watu wake approval rating a mama imeshuka kwa kiwango Cha kutisha mno lakini ukiangalia kwa undani jeshi la polisi chini ya siro limehusika kwa asilimia Mia.
Kwa mfano tunaweza tukaivumilia MAKATO ya MIAMALA ya simu na tukasema potelea mbali labda faida tutaipata huko kwenye kujengewa barabara vijijini nk tukajipa matumaini hivyo.
Sasa mwenendo wa jeshi la polisi chini ya siro tokea ameteuliwa kuwa igp ni wa hovyo Sana amevuka hata viwango vya mahita swali la kujiuliza taifa linapata faida gani ofisi za chadema zikivunjwa milango na polisi nchi nzima au wanachadema wanapokamatwa na polisi kisa kuendesha mikutano yao ambayo katiba haiwazuii nchi inapata faida gani?
Mbowe anapopewa kesi ya ugaidi taifa linafaidikaje? Infact jeshi la polisi ndio magaidi dhidi ya mbowe.
Mbowe mmeharibu bustani zake za mauwa Sasa mauwa na siasa wapi na wapi? Amekaa kimya.
Mbowe mwaka 2019 mmemuibia mashina ya mitaa kwenye uchaguzi nchi nzima amekaa kimya.
Mbowe kwenye ubunge mmempokonya Jimbo lake na ngome zote za majimbo yake ambayo kwa haki msingeshinda amekaa kimya.
Mbowe viongozi wa chama chake TAL ameshambuliwa na risasi 32 huku 16 zikimuingia mwilini siro amekaa kimya.
Sasa hapa Kati ya siro na mbowe gaidi ninani?
Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan tunakuomba umuondoe siro ili uliponye taifa na angalau urudishe approval rating yako angalau kwa sehemu.
Mama kwa taarifa yako hata development partners hawakuelewi kwasasa kwasababu ya siro.
Mwananchi mtiifu.
Moderator na
Maxence Melo nawaomba Sana Sana Sana msifute Wala ku merge Uzi wangu huu Mimi mwananchi wa kawaida Sina pa kutolea kero yangu ikamfikia mh rais moja kwa moja isipokuwa hapa jamiiforum.
Mama muondoe siro.