HABARI...
kwanza nikiri mara yangu ya kwanza kupiga kura ni 2020 na niliwapa CCM..
pili nikiri maovu yote ya uchaguzi nayafahamu na kuyafurahia (upande wa nafasi ya uraisi) maana upinzani bado unasafari ndefu kukamata nchi.
tatu nikiri kuchukizwa na kukosekana kwa wabunge wa upinzani bungeni kama taifa tuliteleza na ni kosa ambalo hata CCM wanalijua na halitojirudia.
KWENYE MADA.
leo MBOWE anakabiliwa na kesi ugaidi lakini ni ukweli kwamba hii kesi haina mashiko na hakuna ugaidi wa aina hii na ninachojua mimi (mimi) kitengo cha ugaidi (CT) hakifanyi kazi kwa staili hii (wachache watanielewa) na kama kingefanya kazi kwa stail hii TANZANIA lingekua lango la magaidi.
CT wana ramani zao, mipaka yao, uongozi wao, safari zao, wahisiwa wao, watuhumiwa wao, mawasiliano yao, selo zao, silaha zao na mengine mengi ambayo hayawezi kuwa wazi kama huu upuuzi unaoendelea.
watanzania, CCM, raisi SAMIA, wabunge, mawaziri, viongozi wa dini n.k kuna siku MBOWE atakufa je tutaongea nini katika msiba wake??
je spika wa bunge utatoa taarifa gani kuhusu mbowe??
viongozi CCM katika mazishi mtavaa sare gani na mtatoa hotuba gani??
MAMA SAMIA kama utaenda msibani utawaambia nini watanzania na familia ya mbowe kwa kipindi hicho??
CHADEMA mtatoa hotuba ya aina gani siku hiyo.??
je serikali itatoa mchango gani katika mazishi yake???
binadamu huzaliwa na mwisho wake ni kufa hata MBOWE atakufa niliowataja fikirieni hili maana siku yaja.
MWISHO:
SIKU HIYO TUTAKUA WANAFIKI TULIOPITILIZA.