Kuna kitu kinanitatiza kimawazo.
Kwanza siamini kwamba hii kesi ya Mbowe ni utashi wa Mama Samia.
Mama Samia aliingia madarakani kama msahihishaji wa excesses za Awamu iliyopita,.
Na kiukweli watu tulianza kupata amani na imani na serikali.
Na si sisi tu waTanzania , bali watu wengi toka nje ya nchi na hata wawakilishi wa kibalozi nchini hapa walionyesha wazi kuridhika na msimamo wa Mama Samia juu ya mwenendo mpya wa nchi.
Mwenendo huo ni kiusalama na kiuchumi na hata kwa haki za binadamu.
Sasa hivi ati Mama kabadilika, na kina Mbowe, hata baada ya ahueni hii ya kisiasa ya Awamu ya sita, nao wamebadilika?
Kina Mbowe wanaanza kutafuta chokochoko za kigaidi?
Siamini.
Na mtetezi mkubwa wa hali hii sasa amekuwa kamanda Sirro?
Hatujui nini kiko nyuma ya pazia.
Wale waliokuwa wanamuona Mama ni wa Haki sasa wanaenda kusikiliza wenyewe kesi Mhakamani
Jamani taratibu , nchi hii ya Mungu ni yetu sote!!!