IGP Sirro: CHADEMA wanamuona Mbowe Malaika hawezi kosea, ushahidi tunao

Baada ya kesi ya uongo ya ugaidi inayomkabili Mcha Mungu Mbowe kuonekana kuamsha presha ndani na nje ya Nchi , huku Jumuiya ya Ulaya (EU) , Amnesty International na Ubalozi wa Marekani kutangaza kutuma wawakilishi wake Mahakamani ili kusikiliza ugaidi wa Mbowe , pia kitendo cha Chadema kuhamasisha wanachama wake nchi nzima kuhudhuria kesi hiyo , ambapo Mabasi kadhaa kutoka mikoani yameanza kuleta wafuasi wa chama hicho tangu tarehe 1.8.2021 Jijini DSM , Mamlaka nchini Tanzania imepata mchecheto na tayari kuna tetesi kwamba huenda Mtuhumiwa huyo asifikishwe Mahakamani ili kuahirisha Munkali wa dunia .

Tuendelee kutega sikio hapa hapa JF kwa taarifa zaidi
Mungu ibariki CHADEMA..Mungu zidi kumtia nguvu mwamba na kumpigania
 
Fake tetesi,UGAIDI na mataifa ya nje ni sumu.Hivyo kipimo kama upo au haupo ni vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Baada ya kesi ya uongo ya ugaidi inayomkabili Mcha Mungu Mbowe kuonekana kuamsha presha ndani na nje ya Nchi , huku Jumuiya ya Ulaya (EU) , Amnesty International na Ubalozi wa Marekani kutangaza kutuma wawakilishi wake Mahakamani ili kusikiliza ugaidi wa Mbowe , pia kitendo cha Chadema kuhamasisha wanachama wake nchi nzima kuhudhuria kesi hiyo , ambapo Mabasi kadhaa kutoka mikoani yameanza kuleta wafuasi wa chama hicho tangu tarehe 1.8.2021 Jijini DSM , Mamlaka nchini Tanzania imepata mchecheto na tayari kuna tetesi kwamba huenda Mtuhumiwa huyo asifikishwe Mahakamani ili kuahirisha Munkali wa dunia .

Tuendelee kutega sikio hapa hapa JF kwa taarifa zaidi
Nasikitika kwamba uonevu unaendelea nchini chini ya uongozi wa mama Samia. Huyu mama kama hatatubu na kuacha uovu wake basi yatamkuta mabaya.
 
Raisi Samia hahusiki na chochote. Mbowe kaanza kushutumiwa au kuhusishwa na umafia dhidi ya wenzake muda mrefu sana kabla mama Samia hajawa hata makamu wa raisi.

Mbowe alihusishwa na kifo cha chacha wangwe baada ya chacha kuonesha nia ya kutaka kupambana nae kwenye uenyekiti wa chama, Mbowe kahusishwa na lile sakata la kutaka kummaliza Zito na sumu bahati nzuri mmanyema yule kachanjiwa na kuzindikwa barabara huko kwao ujiji.

Mbowe kahusishwa na kupotea kwa Ben saa8 baada ya kufika ofisini kwake na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, hapo hatujaweka zile shutuma za kushambuliwa Lisu baada ya kuonekana anaweza kupindua meza kabla ya uchaguzi mkuu wa chama kufika nk. Kwahiyo huyu jamaa anashutuma nyingi na kwahiyo vyombo vya dola vimeamua sasa vimkamate ili kumchunguza kwa shutuma zote anazohusishwa nazo.
Na kwa vile wanampenda sana Mbowe ndio maana hajawahi kushitakiwa kwa hizi tuhuma? Hauoni hapo unatia Dora vyombo vyetu vya dola kuwa wamemuachia muuaji wa aina ile aendelee kutamba uraani mpaka alipopanga kuhudhuria kikao cha Katiba Mpya?

Amandla...
 
Baada ya kesi ya uongo ya ugaidi inayomkabili Mcha Mungu Mbowe kuonekana kuamsha presha ndani na nje ya Nchi , huku Jumuiya ya Ulaya (EU) , Amnesty International na Ubalozi wa Marekani kutangaza kutuma wawakilishi wake Mahakamani ili kusikiliza ugaidi wa Mbowe , pia kitendo cha Chadema kuhamasisha wanachama wake nchi nzima kuhudhuria kesi hiyo , ambapo Mabasi kadhaa kutoka mikoani yameanza kuleta wafuasi wa chama hicho tangu tarehe 1.8.2021 Jijini DSM , Mamlaka nchini Tanzania imepata mchecheto na tayari kuna tetesi kwamba huenda Mtuhumiwa huyo asifikishwe Mahakamani ili kuahirisha Munkali wa dunia .

Tuendelee kutega sikio hapa hapa JF kwa taarifa zaidi
Wakome na bambikabambika zao
 
View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:

“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”

“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”

“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”

“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”

“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”

Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”

“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”

“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”
Uharifu hauna chama.
 
Kitu pekee alichonacho SIRRO na anajivunia nacho ni hiyo mitutu ya Bunduki na Mabomu alivyopewa na wananchi awafanyie kazi ya kulinda usalama wao; lakini badala yake, ameamua kutumia vitu hivyo kuwanyanyasa wananchi.

Bila ya hiyo mitutu, huyu mtu asingekoroma hapa kama yupo usingizini.
 
Na kwa vile wanampenda sana Mbowe ndio maana hajawahi kushitakiwa kwa hizi tuhuma? Hauoni hapo unatia Dora vyombo vyetu vya dola kuwa wamemuachia muuaji wa aina ile aendelee kutamba uraani mpaka alipopanga kuhudhuria kikao cha Katiba Mpya?

Amandla...
Mwanzo ilikuwa ni tuhuma tu, lkn sasa huenda familia ya chacha wangwe au ben saa8 wameamua kwenda kumfungulia kesi ndo ikabidi dola iingilie kati kuangalia kama kweli alihusika au hakuhusika na hayo matukio.
 
Speculations. Kesi ya mauaji inafunguliwa na Jamhuri sio familia. Kwa vile mnasema hizi tuhuma ni za muda mrefu dola ilipaswa kuzichunguza mara baada ya kujitokeza. Kuanza kufukua sasa kwa sababu mtu kasema na sio wao kuwa na ushahidi itakuwa uonevu.

Amandla...
 
Mwanzo ilikuwa ni tuhuma tu, lkn sasa huenda familia ya chacha wangwe au ben saa8 wameamua kwenda kumfungulia kesi ndo ikabidi dola iingilie kati kuangalia kama kweli alihusika au hakuhusika na hayo matukio.
Mbona mnahamisha hamisha kesi, siyo kuua viongozi wa serikali tena Na kulipua vituo vya mafuta?

Yani familia zimefanya upelelezi zimegundua mbowe aliua watu wao serikali haijui mpaka ikashituliwa na wana familia ndo serikali ikaingilia kati?

Akili yako ni ndogo sana kujadili hili jambo ni bora ungekaa kimya
 
Naibu waziri wa mambo ya siasa U.S.A amekutana na viongozi wakuu wa upinzani kikiwemo chama chenye mtuhumiwa wa UGAIDI.

GAIDI ni hatari nchini na nje ya nchi,Iweje MTU huyu kukaa na watu wenye itikadi za kigaidi?

IGP kwanini usiwe unakaa na wapinzani kuliko kuwavunja miguu, ni yupi unayemtumikia yeye na Mali zake.
 
Mbona mnahamisha hamisha kesi, siyo kuua viongozi wa serikali tena Na kulipua vituo vya mafuta?

Yani familia zimefanya upelelezi zimegundua mbowe aliua watu wao serikali haijui mpaka ikashituliwa na wana familia ndo serikali ikaingilia kati?

Akili yako ni ndogo sana kujadili hili jambo ni bora ungekaa kimya
Kama hautokuwa na kazi ya kufanya kesho, basi futilia kesi yake ili kujua sababu ya kukamatwa kwake na kushtakiwa. Mimi sio polisi wala mwanasheria wa serikali ndio maana kweny comment yang nimetumia neno "huenda"
 
Naibu waziri wa mambo ya siasa U.S.A amekutana na viongozi wakuu wa upinzani kikiwemo chama chenye mtuhumiwa wa UGAIDI.

GAIDI ni hatari nchini na nje ya nchi,Iweje MTU huyu kukaa na watu wenye itikadi za kigaidi?
IGP kwanini usiwe unakaa na wapinzani kuliko kuwavunja miguu,ni yupi unayemtumikia yeye na Mali zake.
Ugaidi gani?! . Uliwahi kuonyeshwa gari iliyotumika kumteka Moo. Habari zake zikoje ?!. Si ni huyu huyu anayewabatiza watu leo UGAIDI ?!
 
Back
Top Bottom