Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimesema mara nyingi sana humu JF, kwamba namna ya utendaji wa Polisi wa Tanzania ni ile ambayo inazalisha chuki na wananchi badala ya kukuza uhusiano mzuri. Watu wengi sana wana chuki na Polisi kutokana na vitendo vyao, iwe suala la rushwa, kubambikiwa kesi, matumizi ya nguvi isivyostahili, upendeleo kwa chama tawala nk.
Je umewahi kushuhudia ndugu yako, mtu wa karibu, akipigwa, akikamatwa bila kosa, akinyanyaswa na Polisi? Ulipata hisia gani dhidi ya Polisi? Polisi wametengeneza tabaka la Watanzania ambao hata kama huyu jamaa angesikika akisema kesho naenda kuua Polisi, wasingetoa taarifa kwa Polisi!
Polisi wanajisahau sana na kuwa na utendaji unaowatukuza watawala na kuwakandamiza au kuwapuuza raia, na hili linasababisha watu wengi kuwachukia Polisi. Kuna nchi ambazo raia huwaona Polisi kama rafiki lakini sio Tanzania. Polisi mngejenga uhusiano mzuri na raia, msingehitaji kuahidi zawadi kwa atakaetoa taarifa juu ya huyu mtu, watu wangejitokeza bila hata ahadi ya zawadi.
Kuna wakati hata niliuliza kwamba, hivi kuna mtu yeyote alie upande wa vyama vya upinzani ambae anawaona Polisi kama marafiki? Na nikasema, Polisi hawaoni kwamba ni tatizo kubwa kuwa na idadi kama hiyo inayowachukia?
Naamini kwa dhati kabisa tukio lililotokea la mauaji ya Polisi limetokana na hasira na chuki dhidi ya Polisi kwa mambo fulani waliyomfanyia huyu mtu (inasemekana walimdhulumu dhahabu waliyomkuta nayo) au hata ndugu yake. Ikafikia mahali huyu mtu ali "snap", akapata uenda wazimu wa ghafla (temporary insanity) na kuamua kutafuta Polisi ili awaue.
Sasa hili ni jambo Polisi hawapaswi kulichukulia upande mmoja, kwamba Polisi wenzao wameuwawa, bali wajiulize kwa makini sana kwa nini wameuwawa, na kama linaweza kujirudia. Sintashangaa kama huko nje kuna watu wenye hasira pia dhidi ya Polisi ambao wanaona huyu mtu kafanya kitendo cha ujasiri, na wao pia kwa hasira waliyonayo dhidi ya Polisi wakaona hata wao wanaweza!