IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
IGP Sirro amesema jeshi la polisi linakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu kinachoongozwa na Ole Nguruma baada ya kituo hicho kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka nje.

Sirro amesema kwa mwaka huu pekee kuanzia mwezi January kituo hicho kimepokea takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje hivyo Jeshi linataka kujiridhisha uhalali wa fedha hizo zisijekutumika kwa nia ovu ikiwemo ugaidi na utakatishaji.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

Maendeleo hayana vyama!
 
Hawa Polisi wakikwambia 10 usishike hata moja. Ndiyo hawa hawa wanabambikia kesi FAKE Watanzania wengi wasio na hatia hivyo hata huu ushahidi wao pia unaweza kuwa ni FAKE. Kumbukeni kesi chungu nzima FAKE walizobambikiwa Watanzania mbali mbali ikiwemo yule Kabendera na kusababisha kifo cha mama yake mzazi.

johnthebaptist,
 
Kuna watu humu wanatetea utafikiri wao ndo wanaijua nchi kushinda serikali yenyewe!.. mbona hilo ni utaratibu yakinifu au mlitaka waachiwe tu kwa kuwa Kuna huu msamiati "watetezi wa haki za binadamu!!"

Serikali hebu kagueni hizo mutu mpk mjiridhishe hakuna cha kuangalia usoni hapa,hayo matetezi kwanza yanavunjaga na mipaka yanatetea mpk ndoa za kinyume na jinsia!!
 
Dah hii ni Tanzania.Kaka yangu Ole Ngurumwa hata wakizuia Pesa.lazima tutawanyoosha tu kwenye sanduku la kura ije jua ije mvua.
 
Back
Top Bottom