Uchaguzi 2020 IGP Sirro: Tutawashughulikia walioandaliwa kufanya vurugu

Uchaguzi 2020 IGP Sirro: Tutawashughulikia walioandaliwa kufanya vurugu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema hadi sasa wananchi wengi wamekuwa watulivu licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wachache walioandaliwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kufanya vurugu na kujiingiza kwenye uhalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kuwataka baadhi ya viongozi kufanya masuala ya siasa na kuacha kuwatumia vijana na kuwaingiza kwenye uhalifu na kwamba yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Kuhusu upigaji wa kura Zanzibar, IGP Sirro amesema, wapo baadhi ya watu wanaohamasisha baadhi ya watu au kikundi cha watu kuvunja sheria wakati wa zoezi la upigaji kura kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
 
Naomba kufahamishwa pia,hatua zilizochukuliwa na mkuu huyu,kwa watu wake ambao wamekuwa na viashiria vya kuvuruga uchaguzi Hadi wakati huu ,kwa wajuzi was hatua zilizochukuliwa wanijuze tafadhali.
 
Naambiwa huu mfumo wa vyama vingi ulipopigiwa kura ili kuona kama utafaa au vipi, wengi waliokuwepo kwenye system waliukataa.
Lakini ukapitishwa kibabe na mzee.

Ukiangalia mwenendo unavyokwenda, utagundua kwakuwa mzee hayupo, na system ndio imebaki, basi system inaendelea kuukataa kistyle yake huku ikijifanya inamuenzi mzee.
 
Sirro huwezi ku deal na nguvu ya umma
Mbona watu wameshaanza kufanya vurugu? Bendera za uipnzani zinashushwa mchana kweupe, Hai vijana wa CHADEMA wanatekwa na kuteswa, Singida kijana wa CHADEMA ameuliwa kikatili!

Au vurugu ipi anazungumzia Afande Sirro au labda mpaka wa upande wa pili wawafanyie hao wa mbogamboga ndio ionekane vurugu?
 
Jeshi la polisi linawajibu wa kuwakamata wahalifu. Huu mkwala nia yake ni nini??? Nani mwenye kutaka machafuko zaidi ya polisi wanaotaka viongozi wakisiasa walio madarakani waendelee bila kujali matakwa ya taaluma yao na wananchi. Hivi vyombo kwa kukosa ueledi vimetuweka kuwa tatizo.
 
Back
Top Bottom