IGP Sirro: Ukiwa na mtoto mhalifu halafu usitoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wewe ni tatizo kwa Watanzania

Namwomba Mh.,aliyoyasema kwenye kuaga miili hiyo,aende pia awaambie na wale watakaokuwa wanaaga mwili wa Hamza kabla ya maziko ili nao wajifunze.Bila shaka jeneza lake litakapokuwa limefunikwa na ile bendera ya kile chama likiwa pia likibebwa na wale watu kwani alikuwa kamanda wao kule Mbeya na aliwajengea ofisi ya chama pia aliwasaidia sana kwenye kampeni kama wanavyokiri wenyewe.Heshima yake mpeni.Haki huinua Taifa,bali dhambi ni aibu kwa taifa,
 
Pole kwa askari wetu wa jeshi la polisi, pole kwa wafiwa, ila IGP, ebu fanya utafiti la hili swala kwamba baadhi ya askari wako, wanawanyima haki raia, wanawatesa, wanapenda rushwa, wanabambika kesi, wanatumia madaraka yao vibaya, wanawapora mali (mpaka nyama?!), sasa ukifumbia hili tatizo basi bado uhusiano wa polisi na raia utaendelea kudorora..
 
Bongo nyosso
 
IGP yuko sahihi,Askari ukiwa na silaha inabidi uwe makini na mwangalifu Sana,tofauti na unapokuwa huna silaha,hata Kama nchi hiyo ni ya amani.
IGP alikuwa anatoa ujumbe kwa askari waliohai,kuwa makini na waangalifu kuepusha matukio Kama haya siku za usoni.
Ushauri
1). Askari wafuate kanuni/taratibu/GPO katika utendaji wao wankazi
2).Jeshi la polisi ,likiwapendeza,wapige marufuku,Askari kuongea/ku chat na simu( zisizo la lazima) wakati ubeba silaha,mitaani au kwenye malindo.Amini usiamani hizi simu/mambo ya kuchat ni Changa,tunaona hata majumbani mwetu,vijana wanatumia muda mwingi kuchat na simu tu,kuangalia matukio ya michezo nk
 
IGP Sirro nawe mbona unawakumbatia askari wahalifu? Siku Hamza anafanya yake ilikuwa siku hiyohiyo Rais akikukumbusha vitendo visivyokubalika ndani ya polisi, mimi mara zote hukuona kama ni mwanasiasa tu na kada mzuri wa CCM.
 
Kauli hatari kabisa kuwahi kutolewa na mtu kama IGP nchi hii na Mama amuwajibishe huyu mara moja ile kauli ulinzi shirikishi tusaidiane itatoweka na uhalifu utaongezeka. Sasa tumeanza kuogopana na ile tabia ya Traffic police kusogeleana kwenye magari na vichaka kuombana rushwa ife kuna issue simama meter moja niambie kosa andika fine wengine tuna vipele tusije kujikuna tu risasi. Ila huyu mzee awajibike tu na kauli hizi ni mbaya sana kuwahi kutokea.
 
Sirro anatakiwa aseme nini kimetokea kabla ya kuleta haya maporojo.....lile tukio sio la kawaida unapokuja na general statements kama hizi hutaeleweka....
 
Mtu mzima wa miaka 30 alieamua kufuata njia yake familia inahusika na nini??
Polisi acheni kubambikizia watu kesi za kipuuzi,watu huchoka na hilo tukio ni mfano mzuri..
Mtu akiwa desperate anaona hana cha kulose...

Mjue dunia imebadilika watu wanmingle kiurahisi ..

Msije dhani is Watu wote ni wajinga na mnaweza kuwadanganya tuu...

Polisi muwe wakweli... zama za kuongoza kwa Uongo na janjajanja ushapitwa na wakati
 
Mbona kama Vile ametangaza vita?

ni mwendo wa kuliana timing saivi au?

au mwandishi ndio kaiwasilisha vibaya?
View attachment 1911601
Kwa Lugha nyingine ni kwamba IGP Sirro sasa ameshawatengenezea Biashara Wauza Majeneza Tanzania nzima kwa Kumaanisha kuwa Askari wake Watatuua Wananchi kama Kuku na Inzi kwani Hamza kawapandisha Hasira mno.
 
"Wakati mwingine tunaambiwa tunatumia nguvu kubwa sana sio au hatutendi haki sio? Lakini yanapotekea hapa hatusikii mtu anasema habari ya haki ya polisi maana yake nini msiwe na Double Standard. Kazi hii ni ngumu sana mtu akiiona hivi anajua ni kitu rahisirahisi tu lakini kudeal na mhalifu sio jambo dogo!." .......... Hii kauli mbona kama Sirro anamjibu namba ile inayofuata baada ya 0?
 
RAIA ambao hamna mafunzo ya usalama na ulinzi, mnasumbua kwa kuhoji kila kitu, kinacho zungumzwa na jeshi la police
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…