IGP Sirro: Ukiwa na mtoto mhalifu halafu usitoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wewe ni tatizo kwa Watanzania

Itabidi hadi trafiki wanaongoze magari na silaha za kivita kama Wataliban, ukikosea tu wanakumiminia za kutosha
 
Mbona kama Vile ametangaza vita?

ni mwendo wa kuliana timing saivi au?

au mwandishi ndio kaiwasilisha vibaya?
View attachment 1911601
Wakati nchi makini wanatumia technolojia kama jicho muhimu katika masuala ya ulinzi na usalama, jeshi letu la polisi lipo "busy" kudhiti wapinzani na kukusanya hongo kutokana makosa ya barabarani. Jeshi letu ni lazima lijiongeze ili kuendana na matakwa ya wakati.

Siro asianze kutafuta visingizio ili kuficha dhuluma ambayo ipo nyuma ya pazia kuhusu vijana wake dhidi ya Hamza. Mbona siku nyingine katika matukio kama haya huwa anaunda tume ya uchunguzi mbona katika hili yupo kimya!?

Badala ya kufikiria kuanza matumizi ya kamera maalumu ikiwa kama jicho makini na mbadala ili aweze kufuatilia kwa kificho matendo ya kihalifu, yeye anaona ni vyema kuwajaza askari wetu mitaani na pengine kuanza kuuwa watu fulani waliowakusudia kwa makusudi kwa kisingizio cha tukio la Hamza. Siro uzee ndio huo unakunyemelea, na umepitwa na wakati, ni vyema ukampisha mtu mwingine atumie 'state of art technology" ili kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama hapa nchini.
 
Binafsi huwa nashangaa watu wanaotajataja ICC
 
Askali wangejuaje kama hamza wa hovyo
 
Awaase watu wake waache dhulumati sio wao pekee ndo wenye shida ya pesa
 
Dogo angekuwa gaidi ile Eicher isingeachwa vile


Inategemea!

Mbona magaidi wa Nigeria wanatekaga wanafunzi wa Shule mabinti mara nyingi?

Kwanini wasiteke watu wowote bila kujali jinsia wala umri?!
 
Msomali amefanya jambo la kikatili sana !

Kuua watu wetu ? ! [emoji24][emoji24][emoji24]

Kwanini??? [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Ukiwa na mapolisi wezi, vibaka, madhulumati na usiwachukulie hatua basi jeshi lote huenekana wote ni wezi na majambazi kama ilivyotokea
 
Huyu baba huyu! Kama alivyofanya kwa Mbowe. Anamalizia kabisa hukumu. Kakosa ethics kabisaa, ndio maana jeshi linakwenda bora liende.
Kinachoogopesha ni kuona raia wamepoteza imani na jeshi la polisi huku polisi wakionesha kujiamini kulikopoteza mvuto! Inaogopesha zaidi pale Hamza anapoonekana shujaa huku polisi wakionekana waonevu dhidi ya raia. Nadhani tuliandika humu mara kadhaa idara hii ijitathmini ili uwepo ushiririkiano wa dhati usio na mashaka baina yake na raia kwa ajili ya ustawi wa nchi na watu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…