DOKEZO IGP tuokoe na wizi ulioibuka Arusha unatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

bucho

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2010
Posts
5,149
Reaction score
3,209
Kumeibuka wizi mkoa wa Arusha unaotishia usalama wa wananchi wa kawaida na wafanyabiashara mbalimbali kuvamiwa na kuibiwa either kwa ujambazi wa kutumia pikipiki (tatu mzuka) ama kuibiwa manyumbani na wezi wa kawaida.

Wezi wa pikipiki ama tatu mzuka wamekuwa wakiwaibia watu kwa nguvu huku wakiwadhuru kwa kuwachoma visu ama spoko za baiskeli hata mchana kabisa, huku wakiwanyanganya vitu walivyobeba huku wananchi wa kawaida wakiogopa kuingilia kwa kuhofia maisha Yao.

Hawa wameua watu wengi sana wanojaribu kupambana nao ili kuzuia wizi.

Wezi wa pili ni wezi wa nyumbani na kuvamia sehemu za biashara. Hapa ndio watu wengi wanapoumizi watu zaidi .

Mfano.... Kata ya kimandolu imekumbwa na wezi wanaoiba kila nyumba na sehemu za biashara . Yaaani imekuwa kama imehalalishwa watu kuibiwa nyumba kwa nyumba na sehemu za biashara kila siku bila jeshi la polisi kuchukua hatua zozote za kuzuia wizi huo huku wakijua wahusika wa matukio yote ya wizi .

Mfano kwa kimandolu wanajua kuwa kuna kijana anaitwa ADAM ambaye amekuwa ni mwizi mkuu na ndiye anaye organize wizi wote unaotokea kimandolu. Mwezi watano mwaka Jana kama sijakosea kijana huyo alikamatwa akiwa amekodisha nyumba zaidi ya mbili zikiwa kama warehouse zake za kuifadhi vitu vyake anavyoibia wananchi.

Mwaka jana mwezi wa tano ama wa sita alikamatwa na laptop zaidi ya 30, pikipiki zaidi ya tano , generators zaidi ya kumi , tv haziesabiki na accessories kibao ila akaachiwa kutokana na polisi wasio waaminifu kutoa taarifa za whisle blowers waotoa taarifa. Hivyo wananchi waaogopa kwenda toa ushahidi mahakamani utakoweza kumtia hatiani kwa kuogopa kuja kuuliwa na mtuhumiwa.

Kinachotokea polisi wa doria na baadhi ya polisi central wanakuwa sehemu ya huu ujambazi unaotokea kila siku.

Huyu kijana na washirika wake wamekuwa tishio kwa Kimandolu na sehemu za karibu kwa sababu amekuwa na watu wake ndani ya Jeshi la polisi wanaompa taaarifa.

Chondechonde IGP tunaomba uingilie Kati wizi huu unaotusumbua mjini Arusha . Huyu kijana yupo well trained kiasi cha kwamba ana uwezo wa ku bypass camera na ana mavazi ya kujikinga na camera kutokana na polisi ambao wasio wema wamemtaarifu namna ya kujikinga ili asionekane kwenye camera sehemu mbalimbali anazokwenda kuiba.

Tunaomba IGP na viongozi waandamizi waaingilie kati kuingilia hili tatizo kwa mkoa wa Arusha maaana wananchi tumechoka .
 
Nimemkumbuka Abbas alisumbua sana maeneo ya Mbauda na Olasiti. Akikamatwa akipelekwa Kisongo anarudi baada ya week mbili. Ilifikia hatua wananchi wakachoka na wananchi walipochoka basi mwisho wake ulifika maeneo ya Tindigani JR. Bushmamy
 
Arusha mnapelekewa moto na warangi

Majambazi yote ya arusha yanatokea kondoa
Nimemkumbuka Abbas alisumbua sana maeneo ya Mbauda na Olasiti. Akikamatwa akipelekwa Kisongo anarudi baada ya week mbili. Ilifikia hatua wananchi wakachoka na wananchi walipochoka basi mwisho wake ulifika maeneo ya Tindigani JR. Bushmamy
 
Usiku wa kuamkia ijumaa wametuibia.
Wamekata bati wakaingia.Kuna frame nne zimeungana kila moja wameingia mbili tu ndio zimepona mana hawakuona cha kubeba ila hizi nyingine mbili wameiba.Na hawajachukua vitu vya kubebeka walichokua wanabeba ni voucher na hela tu.
Wanaturudisha nyuma sana.
 
Usiku wa kuamkia ijumaa wametuibia.
Wamekata bati wakaingia.Kuna frame nne zimeungana kila moja wameingia mbili tu ndio zimepoma mana hawakuona Cha kubeba ila hizi nyingine mbili wameiba.Na hawajachukua vitu vya kubebeka walichokua wanabeba ni voucher na hela tu.
Wanaturudisha nyuma sana.
Huyo ni Adam sugu amaekaa kimandolu ndio style yake ya wizi hiyo. Polisi wanajua na wanakaaa kimya. Aibu kubwa sana hii
 
Kumeibuka wizi mkoa wa Arusha unaotishia usalama wa wananchi wa kawaida na wafanyabiashara mbalimbali kuvamiwa na kuibiwa either kwa ujambazi wa kutumia pikipiki (tatu mzuka) ama kuibiwa manyumbani na wezi wa kawaida.

Wezi wa pikipiki ama tatu mzuka wamekuwa wakiwaibia watu kwa nguvu huku wakiwadhuru kwa kuwachoma visu ama spoko za baiskeli hata mchana kabisa, huku wakiwanyanganya vitu walivyobeba huku wananchi wa kawaida wakiogopa kuingilia kwa kuhofia maisha Yao.

Hawa wameua watu wengi sana wanojaribu kupambana nao ili kuzuia wizi.

Wezi wa pili ni wezi wa nyumbani na kuvamia sehemu za biashara. Hapa ndio watu wengi wanapoumizi watu zaidi .

Mfano.... Kata ya kimandolu imekumbwa na wezi wanaoiba kila nyumba na sehemu za biashara . Yaaani imekuwa kama imehalalishwa watu kuibiwa nyumba kwa nyumba na sehemu za biashara kila siku bila jeshi la polisi kuchukua hatua zozote za kuzuia wizi huo huku wakijua wahusika wa matukio yote ya wizi .

Mfano kwa kimandolu wanajua kuwa kuna kijana anaitwa ADAM ambaye amekuwa ni mwizi mkuu na ndiye anaye organize wizi wote unaotokea kimandolu. Mwezi watano mwaka Jana kama sijakosea kijana huyo alikamatwa akiwa amekodisha nyumba zaidi ya mbili zikiwa kama warehouse zake za kuifadhi vitu vyake anavyoibia wananchi.

Mwaka jana mwezi wa tano ama wa sita alikamatwa na laptop zaidi ya 30, pikipiki zaidi ya tano , generators zaidi ya kumi , tv haziesabiki na accessories kibao ila akaachiwa kutokana na polisi wasio waaminifu kutoa taarifa za whisle blowers waotoa taarifa. Hivyo wananchi waaogopa kwenda toa ushahidi mahakamani utakoweza kumtia hatiani kwa kuogopa kuja kuuliwa na mtuhumiwa.

Kinachotokea polisi wa doria na baadhi ya polisi central wanakuwa sehemu ya huu ujambazi unaotokea kila siku.

Huyu kijana na washirika wake wamekuwa tishio kwa Kimandolu na sehemu za karibu kwa sababu amekuwa na watu wake ndani ya Jeshi la polisi wanaompa taaarifa.

Chondechonde IGP tunaomba uingilie Kati wizi huu unaotusumbua mjini Arusha . Huyu kijana yupo well trained kiasi cha kwamba ana uwezo wa ku bypass camera na ana mavazi ya kujikinga na camera kutokana na polisi ambao wasio wema wamemtaarifu namna ya kujikinga ili asionekane kwenye camera sehemu mbalimbali anazokwenda kuiba.

Tunaomba IGP na viongozi waandamizi waaingilie kati kuingilia hili tatizo kwa mkoa wa Arusha maaana wananchi tumechoka .
Sio kimandolu tu, Lemala, daraja mbili na Uzunguni bara bara ya blue stone, kwa week mbili mfululizo wameuawa watu watatu kwa kuchomwa visu na tatu mzuka,bara bara za uzunguni uporaji hufanyika mchana, Sijaona jitihada kuwadhibiti, Mbaya zaidi wameanza kugusa wageni.
 
Back
Top Bottom