DOKEZO IGP tuokoe na wizi ulioibuka Arusha unatisha

DOKEZO IGP tuokoe na wizi ulioibuka Arusha unatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sio kimandolu tu,Lemala,daraja mbili na Uzunguni bara bara ya blue stone,kwa week mbili mfululizo wameuawa watu watatu kwa kuchomwa visu na tatu mzuka,bara bara za uzunguni uporaji hufanyika mchana,Sijaona jitihada kuwadhibiti,Mbaya zaidi wameanza kugusa wageni.

Mnalia na watu watatu kwenye pikipiki? Wakija panya road kama wa Dsm si mtajifungia ndani. Nilijuaga arusha ni wagumu kumbe hakuna kitu bora wanaume wa Dar tuu. Pambaneni
 
Kumeibuka wizi mkoa wa Arusha unaotishia usalama wa wananchi wa kawaida na wafanyabiashara mbalimbali kuvamiwa na kuibiwa either kwa ujambazi wa kutumia pikipiki (tatu mzuka) ama kuibiwa manyumbani na wezi wa kawaida.

Wezi wa pikipiki ama tatu mzuka wamekuwa wakiwaibia watu kwa nguvu huku wakiwadhuru kwa kuwachoma visu ama spoko za baiskeli hata mchana kabisa, huku wakiwanyanganya vitu walivyobeba huku wananchi wa kawaida wakiogopa kuingilia kwa kuhofia maisha Yao.

Hawa wameua watu wengi sana wanojaribu kupambana nao ili kuzuia wizi.

Wezi wa pili ni wezi wa nyumbani na kuvamia sehemu za biashara. Hapa ndio watu wengi wanapoumizi watu zaidi .

Mfano.... Kata ya kimandolu imekumbwa na wezi wanaoiba kila nyumba na sehemu za biashara . Yaaani imekuwa kama imehalalishwa watu kuibiwa nyumba kwa nyumba na sehemu za biashara kila siku bila jeshi la polisi kuchukua hatua zozote za kuzuia wizi huo huku wakijua wahusika wa matukio yote ya wizi .

Mfano kwa kimandolu wanajua kuwa kuna kijana anaitwa ADAM ambaye amekuwa ni mwizi mkuu na ndiye anaye organize wizi wote unaotokea kimandolu. Mwezi watano mwaka Jana kama sijakosea kijana huyo alikamatwa akiwa amekodisha nyumba zaidi ya mbili zikiwa kama warehouse zake za kuifadhi vitu vyake anavyoibia wananchi.

Mwaka jana mwezi wa tano ama wa sita alikamatwa na laptop zaidi ya 30, pikipiki zaidi ya tano , generators zaidi ya kumi , tv haziesabiki na accessories kibao ila akaachiwa kutokana na polisi wasio waaminifu kutoa taarifa za whisle blowers waotoa taarifa. Hivyo wananchi waaogopa kwenda toa ushahidi mahakamani utakoweza kumtia hatiani kwa kuogopa kuja kuuliwa na mtuhumiwa.

Kinachotokea polisi wa doria na baadhi ya polisi central wanakuwa sehemu ya huu ujambazi unaotokea kila siku.

Huyu kijana na washirika wake wamekuwa tishio kwa Kimandolu na sehemu za karibu kwa sababu amekuwa na watu wake ndani ya Jeshi la polisi wanaompa taaarifa.

Chondechonde IGP tunaomba uingilie Kati wizi huu unaotusumbua mjini Arusha . Huyu kijana yupo well trained kiasi cha kwamba ana uwezo wa ku bypass camera na ana mavazi ya kujikinga na camera kutokana na polisi ambao wasio wema wamemtaarifu namna ya kujikinga ili asionekane kwenye camera sehemu mbalimbali anazokwenda kuiba.

Tunaomba IGP na viongozi waandamizi waaingilie kati kuingilia hili tatizo kwa mkoa wa Arusha maaana wananchi tumechoka .
Nihuyuhuyu Adam,
 
Mnakwama wap machalii?!si mliwachekaga wanaume wa dar kisa kuwagwaya panyaroad,now its ur turn!
 
Tanzania hii hunidanganyi shughuli zangu zimenifanya niwajue watanzania wote kwa kina

Majambazi wengi wa Arusha toka zamani wana asili ya kondoa hata ukienda mererani watu katili zaidi ni warangi ndio wanaongoza kwa natukio ya kuua
Kwa mererani enzi hizo mamurere wengi ni Wasonjo hao jamaa ndio walikua makatili sana na ndio majambazi, kuua kwao sio issue.
 
Ina maana wachuga mliokuwa mkiwadiss wadaslam kuhusu panya rodi ndio mnahanya tatu mzuka aisee. Aisee ni vipi chalii yangu Chaliifrancisco mnanyuti tu ani ilibidi muwatie ma beroo ao mawaki adi wadedi
Hamna kitu hao ni porojo tu !! Na ivyo vijambazi vyao ni stimu za bangi tu mirungi hata miili havina vimekauka kwa kuvaa mashati oversize.
 
Sio kimandolu tu,Lemala,daraja mbili na Uzunguni bara bara ya blue stone,kwa week mbili mfululizo wameuawa watu watatu kwa kuchomwa visu na tatu mzuka,bara bara za uzunguni uporaji hufanyika mchana,Sijaona jitihada kuwadhibiti,Mbaya zaidi wameanza kugusa wageni.
Zile sehemu ni hatari sana maana zipo kimya boda boda wakifanya uharifu pana njia nyingi za kutokea...
 
Mnalia na watu watatu kwenye pikipiki? Wakija panya road kama wa Dsm si mtajifungia ndani. Nilijuaga arusha ni wagumu kumbe hakuna kitu bora wanaume wa Dar tuu. Pambaneni
Huelewi,hao 3mzuka wanavizia pale ambapo hakuna raia wengine ila huyo victim tu,mfano Barabara ya East Africa kule unaweza kufika mahali usione mtu yeyote kwa umbali hata wa 500mts kila upande,sasa wakikubania hapo ndiyo Huna wa kukusaidia.
 
Ifike mahali kila raia aruhusiwe tu kumiliki angalau ka bastola tu..ndo tutaheshimiana.
Skia,ikifikia hapo wewe utauliwa na mtu aliye nyuma yako,na yeye atauliwa na aliye nyuma yake,na yeye atauliwa na wa nyuma yake,imagine
 
Back
Top Bottom