IGP Wambura awaonya vikali wanaotaka kuandamana, asema huo ni uhaini akitaka "Wakome" na Wasitishe matamshi yao ya Kichochezi...

More often Tanzanian police behave like idiots. How could a person plotting to overthrow the incumbent government go public to express his intentions?
Foolish
 
Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo za Maandamano.
View attachment 2714475
Ni vzr angetoa na kifungu cha katiba kinachosema kufanya maandamano au kuratibu maandamano ni uhaini!!
 
Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo za Maandamano.

=====

IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amesema kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – awamu ya sita kabla ya mwaka 2025.
Amesema watu hao ambao wamefanya kosa la uhaini, wanahusisha maandamano hayo na kushawishi watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti 2023 jijini Dar es salaam, IGP Wambura amesema aliamini hoja za bandari hujibiwa kwa hoja.
Pia amesema aliamini kwa vile baadhi ya watu hao walienda mahakamani wangeheshimu mahakama lakini badala yake wametoka na kuanza kutafuta ushawishi na kuchochea kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.
Wakili Mwabukusi
“Lakini mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanangusha serikali ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini,” amesisitiza.
IGP Wambura amewaonya watu hao kwamba wakome na wasitishe matamshi yao hayo ya kichochezi lakini pili amesema watachukuliwa hatua za kisheria kutokana na uchochezi wanaoufanya na uhaini wanaoupanga kwani vyote ni makosa ya jinai.
Amesema Jeshi la polisi halitakaa kimya na kuwavumilia, kama walidhani lipo kimya litaenda kuwaonesha kuwa halipo kimya kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi.
“Pili niwaombe watanzania wawapuuze watu hawa, Tanzania ni nchi ya amani ni nchi salama hawa wasitake kushawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko, hatujawahi kufika huko na hatutakaa tufike huko.
“Niwataarifu wachochezi hawa kuwa jeshi la polisi ni imara, wasitikise kiberiti kama waliwahi kutikisa wakaguswa kule nyuma wasiende hatua nyingine, huku wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya. Ninawaonya wasijaribu tena kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi huo,” amesema.
Aidha, amewaomba wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na utuvuli kama ambavyo ni mazoea, taratibu na desturi za Tanzania.
Ameongeza kuwa jeshi hilo halitakubaliana na aina yoyote ya uhalifu wa aina yoyote kwani walitegemea kama ni malengo ya kisiasa yaende kwenye hoja za kisiasa lakini yasitoke yakarudi kwenye matendo ya kihalifu.
“Maana nimeona na jeshi tumeona maneno ya uchochezi na kutisha na kuanza kuibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuweka ushawishi kwa jamii yetu ambayo ni tulivu.
“Aina hii ya uchochezi na kwa hatua waliyofika ni hatua mbaya kwa sababu mikutano ya hadhara haijazuiliwa, lakini tunachozungumza ni matamko, mtu yeyote asijaribu kusogea huko. Kama hajaona mamlaka ya vyombo vya dola basi this time atayaona,” amesema.
Kauli hiyo ya IGP Wambura imekuja siku moja baada ya Wakili Boniface Mwabukusi kutangaza kuwa wataandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima iwapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitafanyia marekebisho vifungu vya mkataba huo wa bandari ndani ya siku 14.
Jana tarehe 10 Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ilitoa huku na kutupa mbali hoja sita muhimu zilizowasilishwa na wakili huyo aliyewakilisha wananchi wane waliofungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Chanzo: Mwanahalisi online
View attachment 2714475
Mnachelewa sana. Msingoje kuzima moto, hakikisheni wachochea moto mnawazimisha wao kwanza.

Maxence Melo kama kiongozi mkuu wa JF, hakikisha, pamoja na "contents managers" ŵako, kuwa JF haitumiki kisiasa za kuiingiza nchi kwenye machafuko.

Panapofuka moshi panaficha moto.
 
Mnachelewa sana. Msingoje kuzima moto, ha k ikisheni wachochea moto mnawazimisha wao kwanza.

Maxence Melo kama kiongozi mkuu wa JF, hakikisha, pamoja na "contents managers" ŵako, kuwa JF haitumiki kisiasa za kuiingiza nchi kwenye machafuko.

Panapofuka moshi panaficha moto.
Umeongea kizalendo zaidi siyo Kidini!
 
Badala ya kuongea ongea Polisi wanatakiwa kuwachukulia hatua Kali waliotoa hayo matamshi ya kichochezi haraka sana Ili iwe funzo Kwa wengine.

Polisi acheni kuchekea manyani,Chukueni Hatua badala ya kutoa matamko.

Maslahi ya Mamilioni ya Watanzania ni muhimu kuliko hao wapuuzi wachache,tokomeza wakafie mbele huko.
Nami nashangaa kwa kweli, watu wametamka wanataka 'kuipindua serikali' wewe mlinzi unakuja kutamka maneno tu! Hivi kweli yupo serious na kazi!?
Au amejiropokea yeye mwenyewe tu?
 
Nchi Ina raia wa ovyo hii,hakuna waandamanaji labda wa mitandaoni ubavu huo hawana 😀,na hivi wanajeshi wamefanya mazoezi ya kivita juzi juzi😂😂😂😂
Hao wanajeshi wangekwenda Russia kumsaidia Putin badala ya kupiga raia wanaotetea haki yao ya kidemokrasio,uhuru wa kutoa maoni!
 
Porojo zilizojaa kiki ndani yake , huyu anataka cheo gani sasa ? maana IGP ndio cheo cha Juu cha Polisi .
 
Naamini hata yeye hajui kama kaonya kapinga ama kashauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_2023-08-08-11-20-10-1.jpg
 
Tuombe tu mambo ya udini yasifike majeshini yaishie humu humu Siasani tunamokunywa kahawa chungu!
Aamina. Naamini majeshi yetu yamejaa weledi na busara ya hali ya juu, hayawezi kamwe kuingia katika ujinga huu......huo ni wa huku kwa kina mwamakula na kishki
 
Nchi Ina raia wa ovyo hii,hakuna waandamanaji labda wa mitandaoni ubavu huo hawana [emoji3],na hivi wanajeshi wamefanya mazoezi ya kivita juzi juzi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1] tunasubiria simba yanga,wasafi festivo tu haha [emoji1]

Ova
 
Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo za Maandamano.

=====

IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amesema kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – awamu ya sita kabla ya mwaka 2025.

Amesema watu hao ambao wamefanya kosa la uhaini, wanahusisha maandamano hayo na kushawishi watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti 2023 jijini Dar es salaam, IGP Wambura amesema aliamini hoja za bandari hujibiwa kwa hoja.

Pia amesema aliamini kwa vile baadhi ya watu hao walienda mahakamani wangeheshimu mahakama lakini badala yake wametoka na kuanza kutafuta ushawishi na kuchochea kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.

“Lakini mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanangusha serikali ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini,” amesisitiza.

IGP Wambura amewaonya watu hao kwamba wakome na wasitishe matamshi yao hayo ya kichochezi lakini pili amesema watachukuliwa hatua za kisheria kutokana na uchochezi wanaoufanya na uhaini wanaoupanga kwani vyote ni makosa ya jinai.

Amesema Jeshi la polisi halitakaa kimya na kuwavumilia, kama walidhani lipo kimya litaenda kuwaonesha kuwa halipo kimya kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi.
“Pili niwaombe watanzania wawapuuze watu hawa, Tanzania ni nchi ya amani ni nchi salama hawa wasitake kushawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko, hatujawahi kufika huko na hatutakaa tufike huko.

“Niwataarifu wachochezi hawa kuwa jeshi la polisi ni imara, wasitikise kiberiti kama waliwahi kutikisa wakaguswa kule nyuma wasiende hatua nyingine, huku wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya. Ninawaonya wasijaribu tena kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi huo,” amesema.

Aidha, amewaomba wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na utuvuli kama ambavyo ni mazoea, taratibu na desturi za Tanzania.

Ameongeza kuwa jeshi hilo halitakubaliana na aina yoyote ya uhalifu wa aina yoyote kwani walitegemea kama ni malengo ya kisiasa yaende kwenye hoja za kisiasa lakini yasitoke yakarudi kwenye matendo ya kihalifu.

“Maana nimeona na jeshi tumeona maneno ya uchochezi na kutisha na kuanza kuibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuweka ushawishi kwa jamii yetu ambayo ni tulivu.

“Aina hii ya uchochezi na kwa hatua waliyofika ni hatua mbaya kwa sababu mikutano ya hadhara haijazuiliwa, lakini tunachozungumza ni matamko, mtu yeyote asijaribu kusogea huko. Kama hajaona mamlaka ya vyombo vya dola basi this time atayaona,” amesema.
Kauli hiyo ya IGP Wambura imekuja siku moja baada ya Wakili Boniface Mwabukusi kutangaza kuwa wataandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima iwapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitafanyia marekebisho vifungu vya mkataba huo wa bandari ndani ya siku 14.

Jana tarehe 10 Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ilitoa huku na kutupa mbali hoja sita muhimu zilizowasilishwa na wakili huyo aliyewakilisha wananchi wane waliofungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Chanzo: Mwanahalisi online
View attachment 2714475

Hakuna wakati mgum kama kipindi nikionacho mbele, watu wamechoka sana
 
Back
Top Bottom