IGP Wambura: Polisi hatuhusiki na matukio ya utekaji watu

IGP Wambura: Polisi hatuhusiki na matukio ya utekaji watu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hakuna haja ya kuongeza neno, Taarifa yake hii hapa.
---
1721070428601.png
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura amesema jeshi hilo halihusiki na matukio yanayodaiwa kuwa ni ya utekaji, kwani jukumu lake la msingi na la kikatiba ni kuhakikisha linalinda usalama wa raia na mali zao.

IGP Wambura amesema hayo leo Jumatatu Julai 15, 2024 akiwa mkoani Simiyu katika ziara ya kuzungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akiwa bungeni alitaja vyanzo vya matukio ya utekaji na kupotea kwa watu kuwa ni wivu wa mapenzi, ushirikina, kugombania ardhi, urithi, kujiteka, visasi na utapeli.

Mwaka huu, Mwananchi limeripoti matukio ya watu zaidi ya 10 kutoweka na wengine baadaye kuelezwa kuwapo mikononi mwa Polisi.

Jana Julai 14, 2024 Polisi Mkoa wa Tanga lilikiri kumshikilia kada wa Chadema, Kombo Mbwana (29) kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mtandao aliyetoweka siku 29 zilizopita.

TOA MAONI YAKO

PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Sativa: Nilitekwa na Jeshi la Polisi wakiwa na lengo la kuniua, hata nikipotea kesho Jeshi la Polisi litakuwa limehusika

- Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Hii ni aibu. Kama hawakamatwi au kuchukuliwa na polisi kwa makosa mbalimbali wako wapi? Ina maana polisi wetu hawana uwezo kweli wa kuchunguza tuhuma hizi na wamekaa kimya tu wakati watu wanalalamika kuwa watu wametoweka? Hapana. Nahisi kuna kitu hakiko sawa.

Naomba mkuu aliangalie upya swala hilo. Kama walalamikaji ni waongo basi wachukuliwe hatua stahiki. Kama watu wametoweka polisi wafanye uchunguzi wa kina watupatie majibu sahihi.

Wale waliojiteka waadhibiwe kwa kuleta taharuki katika jamii. Waliotekwa tujue wako wapi na watekaji waadhibiwe. Na wanaoshikiliwa na polisi tuwajuwe na tufahamishwe tuhuma zao. Kinyume chake lawama zitaendelea kuelekezwa polisi wenye jukumu la kuwalinda raia na mali zao.
 

Siku chache baada ya Kamanda Murilo kutoa kauli yenye utata juu ya matukio ya utekaji na kupotezwa kwa watanzania, IGP kaibuka na kusema Polisi hawahusiki na matukio hayo.

Wambura amesema “Sisi ni Jeshi linalolinda usalama wa watu na mali zao. Wanaoleta tuhuma za namna hiyo (kuhusisha jeshi la Polisi na vitendo vya utekaji) ni kutukosea adabu.

“Jeshi la Polisi linafanya kazi kubwa ya kuwakamata wahalifu na kuwaokoa wale waliotekwa” ameongeza Wambura.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillius Wambura kwa mara ya kwanza amezungumzia taarifa zilizopo ambazo zimekuwa zikihusisha jeshi la Polisi kuhusika katika matukio ya utekezaji wa watu mbalimbali hapa nchini, akibainisha kuwa Jeshi hilo halihusiki na matukio hayo.

IGP Wambura ametoa kauli hiyo leo, wakati akizungumza na waandishi wa Habari, mara baada ya kuweka jiwe la Msingi jengo la Mkuu wa Polisi Bariadi Mkoani humo pamoja na kuzungumza na Askari wa Jeshi hilo katika kituo kikuu cha Polisi Bariadi.

Wambura amebainisha kuwa Jeshi hilo haliwezi kuhusika na matukio hayo, ambapo ameeleza katika baadhi ya matukio wamebaini kuwa watu wamekuwa wakijiteka kisha kutoa taarifa za uongo kuwa wametekwa.

“ Haya matukio ya watu kutekwa au kupotea yamezungumzwa sana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya ndani, niseme hapa Jeshi la polisi halihusiki hata kidogo na matukio haya, na wale wote ambao wamekuwa wakitoa tuhuma hizo dhidi yetu wanatukosea heshima na adabu,” amesema IGP Wambura…..

“ Kuna matukio Mwanza, Mbeya na sehemu nyingine watu wamepotea wametekwa, na baada ya kufuatilia tumegundua wamejiteka na wanatoa taarifa kuwa wametekwa, jambo hili siyo jema na tutawachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivyo,” ameongeza IGP Wabura.

Mkuu huyo wa Polisi nchini, aliwataka wananchi kuacha tabia za ajabu za kujiteka kisha kulisingizia jeshi la polisi kuhusika katika matukio hayo na badala yake wabadilike kwa kuacha kutoa taarifa za uongo.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, aliwahakikishia wananchi usalama wa kutosha wakati wa zoezi la uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Chanzo: Global TV
 
Back
Top Bottom