Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Hakuna namna nyingine sahihi sana ya kuwaenzi hawa zaidi ya kuwajengea minara katika mikoa husika. Mnara mkuu utawekwa Dar Es salaam. Utaitwa mnara wa pili wa mashujaa. Kisha kila mkoa ambao.palitokea mauaji ya halaiki pajengwe mnara kisha majina yote ya waliouawa yawekwe hapo.
Kadhalika picha zao zitafutwe na zitafutiwe namna ambayo zitahifadhiwa vyema eneo hilo, iwe kielekriloniki au kwenye faili.
Sehemu hizi zitakuwa kama vituo vya hija na maeneo ya makumbusho ambapo vizazi vijavyo vitapata kujua kuwa palikuwepo na vijana ambao damu zao zilimwagika kwa ajili ya ukombozi wa pili.
Bila kujali kama walikwapua au nini, kitendo cha kutoka siku hiyo kuandamana ni ushujaa tosha na ujumbe tosha kuwa tendo lao lilileta mabadiliko.
Kadhalika wasisahaulike wale ambao hawakutoka kuandamana ila vifo viliwakuta katika purukushani hizo.
Ukiacha picha zao (passport size), ziwepo pia picha za matukio yote ya mauaji na ukatili wote uliofanyika. Hii italeta heshima kwa marehemu na faraja kwa wafiwa. Pia italeta hofu na uwajibikaji kwa watawala.
Baba uwasamehe makosa yao.
Raha ya milele uwape ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapumzike kwa amani, Amina 🙏