Iko hivi Comoros ni nchi ya kitu kidogo rushwa na ubwanyenye ni mwingi sana.
Kwa hiyo hata mambo yanavyoendeshwa ni lazima uwe na connection ya kukushika mkono.
1. Nilishuhudi mtanzania akiharibiwa matikiti maji yake kisa kakosana na mamlaka.
2.Ukiwa mgeni ukiwekeza uwekezaji mkubwa huyo aliyekushika mkono anaweza kukufanya kitega uchumi pia.
3.Usafiri ni ndege tena ATC na kuna vindege vingine vidogo nimesahau majina
4.Meli ni kwa ajili ya mizigo, by the time niko kule kuna kampuni ilikuwa inafanya research ya kupeleka meli na hata JMT kupitia JWTZ walitaka kupeleka meli za mizigo.
5.Nchi haiko stable kisiasa, Rais wa madarakani ka edit katiba kaongeza muda, halafu kamuweka lockdown raisi wa Zamani Sambi.
6.Visa, zipo za airport ila mpaka uwe na justificative za wapi unafikia, kifupi jamaa hawako systematic, walishawahi kumzuia jamaa fulani pale airport aliletwa na kampuni.
7.Ukitaka kuona sisi JMT ni matajiri nenda Comoros.
8.Mademu wakali wengi ni wa Kianjouan wana kama mixer.
9.Comoros iko kwenye arab league.
10.Mtanzania unaitwa Mdarisalama
11.Moroni kwa hapa kwetu ni kama pale Rangi tatu
Kutoka Zakhem mpaka Charambe, kwa anayepajua jenga picha hiyo.
12.Fursa za biashara ni za chakula sana sana,zamani mpaka nyama
Mchele( maele),magimbi, ndizi, mayai hivi utauza,jamaa hawaujui ugali.
Watu wanapeleka mpaka ndimu.
13.Kilimo:Ardhi ya Grande Comoros sehemu kubwa ina mawe, kilimo labda kisiwa cha Mohel na Anjouan.
14.Wabongo wapo mpaka mama ntilie, mafundi simu, wauza maduka. Asilimia kubwa ni wazanzibar kutoka na historical back ground kwani kuna mpaka majina ya sehemu kufanana
Mfano ngome kongwe kule kuna Ngome kazi kama sikosei.
15.Lugha ni Chikomore na Kifaransa, Kiingereza chako utawapata wachache, hata mademu itakuwa shida, bora uongee kiswahili wanakuelewa kidogo.
16. Muunganiko wa watanzia upo ila haupo thabiti sana kwa kweli, kuhujumiana, majungu kibiashara kupo sana.
Inatosha hapa