Ijue Comoro: Fursa za Biashara na Changamoto Zake

tanx mda mwingine tunatakiwa kuthink ahead tusibeze Sana na kukejeli maarifa ujuzi na taarifa Kama hizi ni Kama tools ya kusaidiana tuyafikie malengo
 
Maandishi ya kiutu uzima, yaliyojitosheleza, hata kipofu anaweza kuona na kiziwi akasikia.

Hii ndio JF niliyokuwa naijuwa mimi.
 
Bwana kaijage nauli kutoka dar mpaka comoro inafika shi ngapi kwa makadirio
 
Soma vizuri hapo kwenye paragraph ya uchumi uliandika nini? Umeandika pesa ya Comoro iko juu ya zaidi dola na euro na pesa yetu ya madafu, hapo ndio umetuacha wengi na mshangao.😲😲
Kama umesoma vizuri ukaelewa, nilisema sielewi kwanini pesa yao ina thamani ukilinganisha na ya kwetu.

Kwa mfano 1000 ya Comoro ni almost 5400 ya kwetu ukiipeleka kwenye USD unapata ngapi?
Soma upya ulichoandika kwenye post yako ya kwanza category ya uchumi.
Yeah na 1 Tzs=0.00043 USD. What's your point?
Hana point yoyote ni mauzauza matupu.

Anataka kuaminisha watu pia kwamba Mayote na ufaransa ni kama Hawaii na Marekani, hizi ni bangi za Malawi.
 

Hapo nadhani kakosea maelezo,ipo hivi
Comorian franc haijazidi thamani dollar wala euro ila imeizid tshs, kimtaa mtaa kule

1 Euro~ 490- 500 KMF
1 Usd~350- 420 KMF
1 KMF~5.5-6 Tshs

Halafu kuhusu Mayotte na Ufaransa. Mayotte ni oversea department ya ufaransa, France autre-mer kama ilivyo Reunion island,Martinique,Guadeloupe etc. Kuna conditions zake pia za mtu ku move kwenda France Metropolitan( France yenyewe).

Kwa hiyo haimaanishi ukiwa mayote basi unaenda tuu France kama unatoka bara unaenda Zenji.

Huo ndio ufaham wangu wakati niko Comoros
 
Bwana kaijage nauli kutoka dar mpaka comoro inafika shi ngapi kwa makadirio

Usafiri ni wa ndege ATC ilikuwa ina jumamosi, jumanne na alhamisi, then waka change jumanne na alhamisi sijui kwa siku hizi.

Nauli ilikuwa 140,000-160,000 KMF kitu kama around 700,000-800,000 Tshs kama sijakosea.
Ila check na website ya Airtanzania.

Asikudanganye mtu kuwa kuna usafiri wa meli, maana meli zenyewe hata mizigo tuu huwa hakunaga guarantee, kuna mkondo wa Mozambique ni hatari.

So meli huchukua muda mrefu........
 
tanx mda mwingine tunatakiwa kuthink ahead tusibeze Sana na kukejeli maarifa ujuzi na taarifa Kama hizi ni Kama tools ya kusaidiana tuyafikie malengo
Asante kwa kusaidia kufafanua hili. Hilo ndio lengo kubwa la uzi huu. Kuna vitu nimejaribu kuvigusia ambavyo ni muhimu sana.
 
Wewe naona unatafuta bwana. Tuliza nye hiyo situmii.
 
Nilisema mtu akitaka kuzamia France njia nyepesi ni kupitia Mayyote, sijasema eti ukifika Mayyote ndio umefika France.
 
Shida ya watanzania mnabisha bila kuchunguza.

Narudia tena, kwa sasa kuna Meli inatoka Dar - Moroni na Nauli yake ni 90,0000KMF

Hiyo Meli ilikuwa hapa na imeahageuza kurudi Dar. Jumamosi inategemea kurudi.
 
Duuh parefu,
shukrani
 
Shida ya watanzania mnabisha bila kuchunguza.

Narudia tena, kwa sasa kuna Meli inatoka Dar - Moroni na Nauli yake ni 90,0000KMF

Hiyo Meli ilikuwa hapa na imeahageuza kurudi Dar. Jumamosi inategemea kurudi.

Sawa, hiyo sina taarifa,navyojua meli za mizigo zenyewe haziko sure,anyway ni kampuni gani?Agency ziko wapi?inatumia muda gani hadi kufika kule?

Wanapandia wapi? Maana pale bandari nishafika mpaka kule kwenye kupeleka mizigo gate la kupitia Central sijui ni namba ngapi lile sijaona kitu.

Share taarifa huru kila mtu apate kujua, 90,000KMF wanalipa Comoros je huku wanalipa Tshs ngapi?
 
Bado nafuatilia hizo taarifa.
Wanapandia pale wanapopandia watu wa Zanibar; kwa maelezo niliyoyapata. Kwa sasa ninachojua hiyo Meli itaondoka Jumamosi hii. Kama Uko jirani unaweza kufika hapo

Ni kweli hizo Meli za mizigo haziko consistent; zinasumbua Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…