Dah ndio maana Africa tunashindwa, ni kwa sababu ya hizi cheap wisdoms.
Ukitaka kujua kama jambo ni baya au zuri andika herufi U kabla ya jina la jambo hilo. Jina utakalo lipata baada ya kuweka herufi U ndilo litakalo kupa majibu kama jambo hilo ni zuri ama sio zuri.
Natoa mifano kadhaa.
1. Dini.
Ukiweka herufi U kabla ya neno Dini unapata neno UDINI.
Maana yake ni kwamba DINI sio jambo zuri. Na kweli dini sio nzuri. Hakuna kitu kimeleta matatizo mazito duniani kama dini.
2. Kabila.
Ukiweka herufi U kabla ya neno kabila unapata UKABILA.
UKABILA sio mzuri . KWA hiyo kabila sio kitu kizuri. Makabila hayafai kuwepo.
3. Tajiri= UTAJIRI.
UTAJIRI ni mzuri KWA hiyo kuwa tajiri ni kitu kizuri ( hakikisha unakuwa tajiri)
Ongeza mifano YAKO mingine