Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

Hutakiwi kusoma bible and quran pekee ili kupata ukweli wa haya soma vitabu vingi zaidi ya vivyo viwili, funga safari nenda Misri, kule unaweza kupata mapya kuliko kitabu cha bible quran and science tuu!
Well said!
 
Wasomi wa taaluma ipi?! Manake kama unatk kuzungumzia vyuo vikuu vya Mali hususani Timbuktu, inafahamika focus yao ilikuwa sana kwenye masuala ya dini ya Kiislamu na kidog masuala ya biashara ambayo pia imezungumzwa sana kwenye dini ya Kiislamu hasa ukizingatia hata Mtume Muhammad kabla ya kupata daraja la utume, alifanya sana biashara kupitia mke wake Bi. Khadija!!!

Na kwa kuthibitisha elimu haimtupi mwenye nayo; Mali hadi kesho ni taifa ambalo dini ya Kiislamu wameishika kisawasawa! Hata akina Manka Mussa tunaeambiwa ndo richest person kupata kutokea duniani, anafahamika alikuwa ni devoted muslim ambae alichangia sana katika ujenzi wa hivyo vituo vya elimu ambavyo matunda yake hadi leo yanaonekana!

Na kwavile najua utakuja na hoja ya "kwani elimu ni nini...!" Nakupa jibu kabisa.... hapa tunazungumzia elimu ile ambayo mabara ya wenzetu inawafanya wapige hatua kimaendeleo wakati sie tuko pale pale! Elimu ya huko Mali endapo ingekuwa ndo hii tunayoizungumzia hapa basi matunda ya elimu hiyo yangeendelea kuwapo hadi sasa kama tunavyoona kwenye suala la elimu ya Kiislamu!

Kaka nimekusoma, hoja yako hasa ni ipi?,
1: kwamba Misri ya Kale haikuwa ya weusi na hao Mapharao hawakuwa weusi?
2: kwamba Misri hakukuwa na Elimu ya kisasa ikitolewa hapo?
3: kwamba mapharao walikuwa ni Miungu?

Naomba uniweke sawa kwenye misimamo yako
 
Kama tunapinga na habari za farao zilizo katika quran tukufu Mimi naomba majibu ya maswali yafuatayo.
1 Kama mwili wake ulionekana miaka ya 1899,je mtume Mohammad(saw)alizifahamu vipi habari za farao?
2Ni kiashiria gani kilimjulisha kuwa kuna mtu ambaye ni faraho aliishi misri na mwili haujaharibika hadi wakati wake na pia mwili huo hautahalibika hata baada ya kufa kwake?
3Je tukiacha Quran ni kitabu gani ambacho kimeandika habari za faraho kuhusiana na kufa kwake na mwili kuhufadhiwa hadi Leo(weka link tusome).
4Wakati Quran inasema mwili wake hautahalibika hadi siku ya mwisho.mwandishi alijua kuwa hadi miaka hii ungekuwa haujaoza?.Naomba majibu ya maswali yangu

Kwanza ukae ukijua Pharao sio jina, bali ni cheo ni kama vile unavyosema , Mfalme, Rais, Sultan nk, so Mapharao walikuwa wengi sana wala sio mmoja
1: Mohammad alizifahamu habari za Mapharao kwa sababu zilikuwa zinajulikana na watu wote wa ukanda huo wa middle east

2: hilo la mwili kutoharibika lilikuwa linajulikana na ukanda wote huo, kuwa mapharao wakifa huwa wanakaushwa na kuhifadhiwa so miili mingi ya Mapharao waliopita imepatikana, hata Mzee Jakobo Babayake na Yusuf alienda Misri kukaa na mwanae Yusufu na alipokufa walimkausha kama wanavyofanywa Mapharao na wakamuweka kwenye Sanduku kama wanavyofanywa mapharao na alikaa kwa muda mrefu kabla ya kina Yufusu kuja kumzika babayao Kwao (Soma Biblia kisa cha Yusufu utayaona hayo)

3: Maandishi yapo mengi kwenye mapango na makaburi ya mapharao hapo misri yenye kuelezea hayo,

4: Wakati quran inaandikwa kulikuwa na mapharao ambao walishakaushwa kwa zaidi ya miaaka 2000 na walikuwa bado wapo na mpaka leo bado wapo, ni kitu kilichokuwa kinajulikana
 
Ila hawa red Indians ,South America wamejaa kibao pale Brazil. Colombia, Venezuela n.k
Nalog off
Hao walipelekwa Brazil kwenda kulima miwa wakitolewa kwenye nchi yao ya Asili America, baada ya kuonekana kuwa hawana nguvu sana na wanachoka mapema ndio wazungu(Wareno) walipokuja Africa kiwachukua wakina Pele kwenda kulima miwa kwa ajili ya Sukari
 
Sasa mbona neno firauni huwa linahusishwa na matendo mabaya, utasikia yule jamaa firauni sana amebaka mtoto, au lina maana zaidi y moja?
Mzee Mapharao walikuwa ni moja wa watu wastaarabu waliopata kuishi Ulimwenguni, na ustaarabu mwingi uliopo leo ulimwenguni umetokea kwenye kingdom ya Misri ambako ndipo MaPharao walitawala! Hayo unayoyasema ni upotoshaji wa Biblia na Quran kutuziba weusi tusijitambue maana hao mapharao walikuwa ni weusi tii! Kama sisi na walikuwa na nguvu kiasi kwamba waliweza kuwatawala hadi waisrael
 
hutyo herode si alikuwa mfalme wa Israel Mkuu-na kama ndivyo basi ni dhahiri alikuwa akiongoza weupe wenzake kwa maana hiyo waisrael ni weupe.sasa dhana na ya kuwa waisrael halisi walikuwa weusi inatoka wapi??
herode alikuwa mrumi na alikuwa pale israel kuwakilisha dola ya roma hivyo yeye alikuwa mweupe
 
Hivi ni kwa nn na kwa vp mababu zetu walikubali kutawaliwa kufanywa watumwa na kutumikishwa na wazungu na waarabu kwa nyakati tofauti wkt tunaamini tuliishakuwa na akili na uwezo sawa tangu kumbwa kwetu....
Ni kwa nn hali hiyo ya kujitawala kiuchumi hatuifikii sisi wafrica zaidi ya madeni ya mataifa yetu kuongezeka kila mwaka na kitegemea misaada kwenye bajeti zetu?
Just curious
 
Watu weusi tuna taabu!! Tusipojiegesha kwa Wayahudi utasikia Misri ya Kale tulikuwa sisi!!

Tulivyo maboya, upande mwingine tunaamini sisi ni watoto wa Ibrahim! Na kuhitimisha uboya kama sio ukila.za wetu hapo hapo tunakubali, Ishmael ni mtoto wa Ibrahim na huyu Ishmael mama ake alitokea Misri! Na kutokana na unduze huo huo tulionao tunakubali Ishmael ndie chimbuko la Waarabu-- kwamba mtoto wa mama Mmisri ndie chimbuko la Waarabu na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa kwamba mama ake Ishmael nae alikuwa Mwarabu wa Misri!

Sasa hao Waarabu walienda wapi hadi Misri ikageuka kuwa ya Wamatumbi akina Firauni?! Mbona hawa Wamatumbi hatusikii kwamba ndio wanadamu wa kale nchi jirani na Misri?!

Miafrika bhana... kusikia Wayahudi eti ma-genius na yenyewe inataka kujinasibisha na Wayahudi! Kusikia Mzungu na jeuri yake yote hadi leo hafahamu mapiramidi yalijengwaje... Wamatumbi hao; kama mkojo wa asubuhi kwamba eti mapiramidi yalijengwa na mababu zao!!

Ajabu ni kwamba, hawafananii na chochote na hao kimaarifa! Japo miaka elfu kadhaa ishapita, ndo kwanza wengine tunajiita Tanzania ya Viwanda lakini viwanda vyenyewe ni vile ambavyo Ulaya vilikuwepo miaka 500 iliyopita!
umeandika makala ndefu ila utumbo mtupu....
 
Mimi niliyeukubali Uafrika wangu na nyie ambao mara mjinasibishe na Wayahudi mara mjinasibishe na akina Farao; ni kati yetu anayestahili kuitwa nyani?! Ni nani kati yetu anayejidharau?! Unaona ulivyo na akili za kitumwa?! Kumbe kutokuwa tayari kujinasibisha na akina Farao ni sawa na kuwa takataka! Na ili usiwe takataka ndio maana hamuishi kujinasibisha na akina Farao na Wayahudi?! Halafu ona unavyotoa mifano irrelevant! Sasa hao Wachina wamejinasibisha na Mafarao?!

Mtu kama mimi ninayekubali Uafrika wangu bila kujinasibisha na yeyote siwezi kujisikia takataka lakini wewe unaeamini eti Farao huenda alikuwa babu yako ndie unayejiona takataka cuz' you can't stand on your own!

Badala ya kunyesha mapovu; jibu hoja!
vipimo vya kisayans vinaonyesha farao alikua mweus....pharaos na egytian gods wote walikua weus kama haujui
waliposambaratika baada ya kuja mgiriki,mroma na muarabu wakaanza kuja kusin mwa africa ndiomaana utaona wamasai,wanyarwanda,wasomali na hata waethiopia wanafanana

SOMA SANA ME SIO MUONGEAJI
 
IMG_0413.JPG
Indeed!
 
Sasa mbona neno firauni huwa linahusishwa na matendo mabaya, utasikia yule jamaa firauni sana amebaka mtoto, au lina maana zaidi y moja?
leo mtoto akiitwa bashite inaonekana dharau kwasababu ya kitu flan

ila kabla ya haya bashite lilikua jina zuri tu

hamna mtu anapenda kumuita mwanae kain coz alimuua mwenzake

au kuna mtu anapenda kumuita mwanae PILATO AU GOLIATH???
 
Na mimi nimrods, jamaa anajichukia anaweza kujilisha sumu yeye na ukoo wake walahi! A pure slave mind! Poor fella!
hahhhhaa mentak slavery na kutokutambua mambo...anajipenda kama mweus ila hajui kuna nn ndan yake
 
Back
Top Bottom