Ijue historia ya kaburi la Sharif Abdushakur Salim Al Attas lililopo Samora, Posta Jijini Dar es Salaam

Ijue historia ya kaburi la Sharif Abdushakur Salim Al Attas lililopo Samora, Posta Jijini Dar es Salaam

Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna KABURI LA AJABU wacha nikufahamishe:-
Huenda ulishawahi kuliona lakini hujui chochote kuhusu kaburi hilo,
Jijini Dar es salaam katikati ya barabara ya SAMORA, INDIA na MOSQUE,
Katika eneo maarufu lijulikanalo kama CLOCK TOWER,

Ukifika katika maeneo hayo kitu cha kwanza,
Utakacho kiona pale ni KABURI lililo jengewa na marumaru nyeupe,
Kaburi lenyewe ni hilo hapo chini ndugu yangu,
Kaburi hilo unalo liona lina miaka zaidi ya 200 hapo,
Kaburi hilo licha ya kuzikwa miaka mingi iliopita,
Lakini cha ajabu muda wote utakao kwenda hulikuti chafu,
Yaani nisafi na hicho ndio kitu kinacho washangaza wengi,
Kwani hawaja wahi kumuona yoyote anasafisha kaburi hilo,

Kaburi hilo lipo hapo kwa zaidi ya miaka 200,
Katika kaburi hilo kuna mtu maalumu ambaye,
Hulifanyia usafi kila siku kwa kuliosha na kusafisha,
Lakini mtu huyo hufanya kazi hiyo mara nyingi usiku,

Mtu huyo hulipwa kabisa pesa kwa kazi hiyo,
Lakini haijulikani hulipwa mshahara wake kwa kazi hiyo na nani,
Vile vile kwenye hilo kaburi baadhi ya watu huenda kuabudu,
Na ibada hiyo mara nyingi sana hufanyika usiku tu.

Je, kaburi hili ni la nani katika historia ya nchi yetu hadi akazikwa katikati ya jiji?,
Naje kaburi hili likihamishwa pale kama mengine yalivyo hamishwaga kutakuwa na athari gani?,
Nilidhani mtu wa muhimu sana katika historia ya nchi yetu,
Ni Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tu,
Ambaye kama angelizikwa pale au sehemu inayofanana na hiyo,
Isingekua jambo la kushangaza na ingetoa mwanya,
Hata kwa vizazi vyetu vijavyo kuona na kushuhudia alipolazwa muasisi wa Taifa letu,
Lakini sio yeye na Tanzania kuna watu maarufu wengi,

Hilo kaburi la mtu mmoja aliekuwa SHARIF na IMAM mkuu,
Wa msikiti mkubwa uliokuwepo hapo kabla ya kuingia wajerumani,
Msikiti huo ndio wa kwanza kabla ya kanisa la St Joseph pale Sokoine Drive,
Wajerumani waliposhika hatamu za Tanganyika,
Waliamua kujenga ofisi na nyumba zao barabara hii ya samora na sokoine,
Na hapo ndipo mjii wa kisasa ulipoanza kujengwa,
Hivyo huu msikiti ulikuwapo hapo CLOCK TOWER,
Nao ukawa lazima uvunjwe katika master plan yao,
Wajerumani walipata upinzani mkubwa sana,
Kutoka jumuia ya waislam na wenyeji kuhusu kuvunjwa msikiti huo,

Baadae Governor wa Ujerumani Tanganyika,
Alikubaliana na wenyeji ya kwamba msikiti huo uhamishwe,
Na kujengwa pale Kitumbini lakini kaburi hilo lilibaki hapo hapo,
Ndipo kaburi hilo la SHARIF na IMAM ikabidi,
Libaki hapo hapo lilipo kama ukumbusho wao,

Wajerumani walitawala Tanganyika lakini waliheshimu sana,
Mila na taratibu za wenyeji kama uchifu na Customary laws,
Msikiti wa Kitumbini ulijengwa na Wajerumani,
Kulipa ule iliokuwapo CLOCK TOWER na upo hadi leo,
Msikiti huo kwa jinsi ulivyo imara unaweza kudhani umejengwa juzi,
Kuhusu umbali wa Kaburi hilo lipo meta 300 kusini mwa mnara wa saa,
Jijini Dar es Salaam ipo bustani ya muda sana ya zaidi ya miaka 220,
Upande wa Magharibi kuna Barabara ya Samora,
Na India street huku upande wa Kaskazini na Kusini,
Kuna barabara ya Aggrey na Mosque street,

Lakini upande wa Kusini mwa bustani hiyo ya kale,
Ndipo lilipo KABURI hilo kongwe sana lisilokuwa na jina,
Wala mwaka wala alama yoyote ile limekuwa mahali hapo yapata miaka karibu 200 iliopita,

Je, ni nani huyu asiyekua hana jina nani?,
Na kwanini alizikwa mahali pale tena peke yake?,

Usiwe na shaka kila kitu utakijua leo kuhusu kaburi hilo,
Watu wengi hawajui siri kubwa ya kaburi hili,
La mtu asiejulikana wala jina lake halipo hapo kaburini,
Jina lake kamili anaitwa ABDUL SHAKUR SALIM LATASI,
Alifariki dunia mwaka 1862 kabla SEYYID MAJJID wa OMAN,
Na wakoloni wa kijerumani kutua hapa nchinI,
Kwenye miaka hiyo wakati jiji la Dar es salaam pakiitwa MZIZIMA,
Eneo hilo kuanzia clock tower mpaka kule Magomeni,
Liliitawaliwa na huyo jamaa kama diwani wa eneo hilo,

Mnamo mwaka 1820 ulikuwapo msikiti ambao,
Ilijengwa na huyu bwana Sharif Abdul L'aatasi,
Kwa kusaidiana na watu wengine wa Mzizima wakati huo,
Msikiti huo ulikua wa udongo wa kuchoma,
Na miti na kuwako hadi mwaka 1865 hivi,
Wakati SAYYED MAJJID akiishi jumba alilojenga ambalo sasa ni ikulu ya Magogoni,

Wakoloni walipokuja wa kujerumani mnano 1885,
Baada ya kifo cha SAYYED MAJJID walifanya kazi,
Na LATASI kama kadhi mkuu mpaka alipofariki dunia,
Diwani LATASI SHARIF ni mzaliwa wa Mzizima,
Lakini anaasili ya damu ya Uajemi au Persian,
Alikuwa maarufu sana pia aliaminika sana na Wajerumani,
Alifariki mwaka 1862 na kuzikwa nje karibu na msikiti wake,
Na hatimae Mwanae OMARI SALIM LATASI alirithi kiti kama kadhi mkuu,
Wakati ule ulitokea mgongano mkubwa kati ya watu na imani zao,
Hasa baada ya wajerumani kujenga maeneo hayo,
Na shughuli za kijamii eneo la msikiti wa LATASI,

Hivyo ilibidi wakubaliane msikiti ule uhamishwe na watachangia kujenga msikiti mpya,
Basi wajerumani walitoa rupee 50 kama fidia ya jengo jipya,
Lakini kaburi lisihamishwe na kubaki kwasababu nilio ieleza hapo juu,
Eneo jipya lililojengwa msikiti likawa ndio hapo Msikiti wa Ijumaa wa Kitumbini,
Ulipo kwa sasa kwa kawaida Wakoloni hasa wajerumani,
wanaheshimu Sana makaburi hasa ya watu ambao walisaidiana nao kipindi cha ukoloni,

Hivyo kaburi lake likabakia pale pale hadi leo,
Cha ajabu halikuandikwa jina na limebaki kama,
Kaburi lisilo na jina kabisa jijini Dar es salaam,
Watu wamegeuza kiti cha kupunga upepo kaburi hilo,
Bila kujua kuwa historia ya KABURI hilo na pengine hawajui,
Ya kwamba usiku kuna watu huja kufanya ibada hapo
 

Attachments

  • posta.jpg
    posta.jpg
    31.5 KB · Views: 4
Kwann wafanye ibada kwa binadamu mwenzao tena kila siku??

Ni Nan analifanyia usafi?

Na analipwa na nani huyo anaelisafisha?

Reference yako n ip?
 
Itakua alikua mzee wa busara...nadhani mnaelewa...
 
Hivyo kaburi lake likabakia pale pale hadi leo,
Cha ajabu halikuandikwa jina na limebaki kama,
Kaburi lisilo na jina kabisa jijini Dar es salaam,
Watu wamegeuza kiti cha kupunga upepo kaburi hilo,
Bila kujua kuwa historia ya KABURI hilo na pengine hawajui,
Ya kwamba usiku kuna watu huja kufanya ibada hapo
Nashauri jina lake liandikwe na lijengewe uzio mdogo na historia yake iandikwe ikawekwe Makumbusho ya Taifa
 
Kuna bustani moja katikati ya jiji la Dar es salaam (katikati ya barabara ya Samora, India na Mosque) maeneo ya clock tower. Ukifika katika bustani hiyo, kitu cha kwanza utakachokiona pale ni kaburi lililojengewa na marumaru nyeupe na ambalo kwa mujibu wa watu waliozoea kukaa pale mara kwa mara ni kwamba kuna mtu maalumu ambaye hulifanyia usafi kila siku kwa kuliosha na kusafisha mazingira yaliyozunguka kaburi hilo (siyo bustani yote!) na hulipwa mshahara wake kwa kazi hiyo (sijui hulipwa na nani). Vile vile nimesikia kwamba baadhi ya watu huenda kuabudu pale nyakati za usiku.

Je, kaburi hili ni la nani katika historia ya nchi yetu hadi akazikwa katikati ya jiji?​
Je, kaburi hili likihamishwa pale kama mengine yavyohamishwaga kutakuwa na athari gani?​

Nilidhani mtu wa muhimu sana katika historia ya nchi yetu ni Marehemu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere ambaye kama angelizikwa pale au sehemu inayofanana na hiyo ingetoa mwanya hata vizazi vyetu vijavyo kuona na kushuhudia alipolazwa mhasisi wa Taifa letu, vile vile kwa vitendo vya hawa MAFISADI tungeweza kuamua wana JF tukaenda kuwaombea dua baya.

View attachment 1833063

Maoni kutoka kwa wadau


************
Ben Zen Tarot orat hii hapa habari kwa undani
 
Ni uhuni tu na wizi wa ardhi kupitia mgongo wa dini, Kiongozi hewa wa kiislam aliezaliwa ndotoni wakampa cheo na kufia ndotoni huko huko. Hakuwah kuwepo hakuna aliezikwa hapo hakuna hata mfupa. Anaebisha anitajia Jina na Tarehe za Kuzaliwa na Kufa kwa huyo Mchawi aliegoma kuchimbika...?
Duuh?!
 
Back
Top Bottom