Kuna bustani moja katikati ya jiji la Dar es salaam (katikati ya barabara ya Samora, India na Mosque) maeneo ya clock tower. Ukifika katika bustani hiyo, kitu cha kwanza utakachokiona pale ni kaburi lililojengewa na marumaru nyeupe na ambalo kwa mujibu wa watu waliozoea kukaa pale mara kwa mara ni kwamba kuna mtu maalumu ambaye hulifanyia usafi kila siku kwa kuliosha na kusafisha mazingira yaliyozunguka kaburi hilo (siyo bustani yote!) na hulipwa mshahara wake kwa kazi hiyo (sijui hulipwa na nani). Vile vile nimesikia kwamba baadhi ya watu huenda kuabudu pale nyakati za usiku.
Swali, je kaburi hili ni la nani ambaye ni muhimu sana kiasi hicho katika historia ya nchi yetu hadi akazikwa katikati ya jiji? Je, kaburi hili likihamishwa pale kama mengine yavyohamishwaga kutakuwa na athari gani?
Nilidhani mtu wa muhimu sana katika historia ya nchi yetu ni Marehemu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere ambaye kama angelizikwa pale au sehemu inayofanana na hiyo ingetoa mwanya hata vizazi vyetu vijavyo kuona na kushuhudia alipolazwa mhasisi wa Taifa letu, vile vile kwa vitendo vya hawa MAFISADI tungeweza kuamua wana JF tukaenda kuwaombea dua baya.