Ijue Historia ya muasisi wa TANU, Ally Kleist Sykes (1926 - 2013)

Ijue Historia ya muasisi wa TANU, Ally Kleist Sykes (1926 - 2013)

Mkuu wangu si umesema umesoma vidatu vingi lakini hakuna sehemu umefundishwa kuwa Ally Sykes ni mwasisi au nakusingizia.

Mie nikakujibu kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na chuo cha Kivukoni kimemtaja Ally Sykes pamoja kuwa na mapungufu mengi. Kama umesoma Chuo Kikuu nenda kwenye historia ya Tanganyika utakutana na jina la Ally Sykes.

Historia ya Ilunga mie sijapata kuisikia mie nimemjua Ally Sykes kupitia vitabu nilivyokutajia na wazee wangu.

RITZ,
By Mwungwana asikushuulishe! huyu historia aliyofundishwa ni kuwa kabla ya kuwa binaadamu alikuwa Nyani sasa mtu anaeamini kuwa alikuwa Nyani atamjuaje Shujaa Ally Sykes?
 
Viongozi wa dini wote walikuwepo?

Viongozi wa Dini ya KirastaFari walikuwepo?

Viongozi wa Dini ya Kiyahudi walikuwepo?

Viongozi wa Dini ya Su-Yang walikuwepo?

Viongozi wa Soka walikuwepo?

Viongozi wa ..... Walikuwepo?

Umeathiriwa na udini sana, halafu ajabu sana unalaumu kuwa "wazee wako" hawaenziwi na serikali huku wewe ni mfia ccm hiyo hiyo ya Julius Nyerere unaemdhihaki kila uchao!

Nikufunde ndugu,

Chama cha siasa misiba sio nembo ya siasa zake!

Mwenye nyota ya misiba ni mwenyekiti wa chama chako ccm tu katika nchi hii!

yericko huyo ameshavurugwa na ngano za MZEE SIDE
 
RITZ,
By Mwungwana asikushuulishe! huyu historia aliyofundishwa ni kuwa kabla ya kuwa binaadamu alikuwa Nyani sasa mtu anaeamini kuwa alikuwa Nyani atamjuaje Shujaa Ally Sykes?

walewale..
Kwani wewe kuna shule inayofundisha tufauti na hivyo
 
History ya ally sykes inahuzunisha hakufaidi matunda ya uhuru wale waliokuwa Pamoja na mkoloni Leo Ndio wanaotutawala hata kizazi chake sikioni ktk serikali tunawaona kina nape na January makamba wanakula nchi
 
Ndoto yake haikuwa kugawana vyeo,ndoto yake ilikuwa ni sisi watoto wa Tanzania tupate UHURU.NAAM ndoto yake imetimia! Ametimiza wajibu wake Ni wajibu wetu kuutambua na kuuenzi.tuna deni kubwa la shukurani kwa mzee Ally sykes na inanishangaza mtaa wa kongo alipozaliwa unaitwa mtaa makamba.UTOVU WETU WA SHUKURANI HAUNA KIFANI! Mungu ailaze roho ya mzee wetu Ally sykes peponi.
 
KWELI ITASHINDA KESHO KAMA LEO HAITOSHI! Mzalendo Muasisi wa TANU aliyemwandikia na Kumkabidhi Julius Nyerere Kadi ya TANU Na. 1[/B][/CENTER][/CENTER]
Historia ina kawaida ya kujirudia. Ally Sykes mmoja wa waasisi wa TANU, mmoja wa wale watu wasiozidi takriban saba walikuwa katika kamati ya ndani ya TAA iliyounda TANU, mmoja wa wafadhili wakuu wa TANU, mmoja wa askari na hapa nalitumia neno ‘’askari’’ kwa maana yake halisi kwa kuwa ni Ally Sykes ndiye TAA hadi TANU ikimtegemea kwa kutekeleza mambo ya hatari dhidi ya Waingereza, amefariki dunia. Ally Sykes ndiye alikuwa akipewa kazi za hatari za kumwaga ‘’sumu na upupu’’ dhidi ya serikali. Sumu na ----- huu yalikuwa makaratasi aliyokuwa akichapa nyumbani kwake usiku makaratasi ambayo Waingereza waliyaita makaratasi ya ‘’uchochezi.’’ Waingereza na makachero wake walikuwa wanamjua Ally Sykes vizuri. Waingereza walikuwa wakijua kuwa alikuwa na medali ya mlenga shabaha bingwa aliyopata Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Huyu ndiye Ally Sykes mzalendo muasisi wa TANU ambae sahihi yake ndiyo iko katika kadi ya TANU ya Baba wa Taifa, amefariki Nairobi Jumapili iliyopita alikokwenda kwa ajili ya matibabu.
Siku ile ile ya Jumapili milango ya mchana mchana kabisa kabla ya adhuhuri taarifa ikawasili Dar es Salaam kuwa Ally Sykes amefariki dunia. Ghafla mji wa Dar es Salaam alikozaliwa na akaendesha harakati zake dhidi ya ukoloni wa Waingereza uligubikwa na simanzi. Kila simu iliyokuwa ikipokelewa na wengi ilikuwa ni kutaka kuthibitisha kifo kile. Binafsi simu zikaanza kumiminika kwangu za kunipa pole.
Hadi kufika jioni habari zikawa zimeenea mji mzima kuwa ni kweli Ally Sykes hayuko tena duniani. Haukupita muda siku ile ile maiti ya Ally Sykes ikawasili Dar es Salaam kwa ndege ya kukodi ikiwa imesindikizwa na mkewe Bi Zainab na baadhi ya wanawe wakiongozwa na mtoto wake wa kwanza wa kiume Abraham Sykes. Siku ya pili Jumatatu magazeti yote yalikuwa yametoka yakiwa hayana taarifa yoyote ya kifo cha Ally Sykes. Hii iliwashangaza watu wengi sana isipokuwa mimi. Sikushangaa kwa kuwa nilikuwa najua siasa za historia inayomzunguka Ally Sykes kwa miaka mingi hususan kuhusu mchango wake binafsi na wa kaka yake marehemu Abdulwahid Sykes katika harakati za kuasisi TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.
Historia ina kawaida ya kijurudia. Haya ya kupuuza kifo cha Ally Sykes yalimkuta pia kaka yake Abdulwahid alipofariki mwaka 1968.
Ally Sykes alikuwa mtu maarufu kupita kiasi. Alikuwa kwanza ana umaarufu wa kuzaliwa. Kazaliwa Dar es Salaam Gerezani, mtoto wa mjini. Kisha alikuwa maarufu kwa nasaba. Baba yake Kleist Sykes alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika siasa zote za Dar es Salaam katika miaka ya ya mwanzo ya 1900 hadi alipofariki mwaka 1949. Baba yake alikuwa maarufu kwa kuwa alilelewa na Affande Plantan askari kiongozi katika jeshi la Wajerumani lilokuja Tanganyika na Herman Von Wissman wakati Wajerumani walipoingia kuitawala Tanganyika. Kleist alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Association mwaka 1929 chama kilichokuja baadae kujibadili na kuwa TANU Ally Sykes akiwa mmoja wa hao waasisi. Baba yake Kleist aliasisi Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na kupitia jumuia hii akajenga shule ya kwanza ya Kiiislam Dar es Salaam, shule ambayo ilisomesha Qur’an pamoja na masomo ya kisekula. Hii Al Jamiatul Islamiyya ndiyo iliyotoa viongozi wa kwanza kuiendesha TAA na baadae TANU katika harakati za kudai uhuru. Ally Sykes kwa mazingira na makuzi haya akawa maarufu kama alivyokuwa baba yake. Lakini kubwa zaidi na hili ndilo kwa bahati mbaya ndilo linalojulikana zaidi kwa sasa ni utajiri ambao Allah alimruzuku toka akiwa kijana mdogo sana katika miaka ya 1950 alipoanza biashara kwa kuanzisha kampuni yake binafsi iliyoitwa Sykes Sales Promotion Consultancy.
Inajulikana na wengi Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndiyo watu wa mwanzo kumpokea Julius Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952. Nyerere alifika nyumbani kwa akina Sykes kwa utambulisho na hii ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa udugu mkubwa wa mapenzi ya dhati si baina yao tu bali hata kwa wake na mama zao. Mama yake Nyerere Bi Mugaya hakuwa akipungua nyumbani kwa Mama Abdu Bi Mruguru biti Mussa Mtaa wa Kirk. Halikadhalika Maria Nyerere hakuwa akipungua nyumbani kwa aidha kwa Bi Zainab mkewe Ally Sykes Mtaa wa Kipata au kwa Bi Mwamvua mkewe Abdulwahid Sykes Mtaa wa Aggrey. Wakati huu Abdulwahid ndiye akiwa rais wa TAA na harakati za kuanzisha TANU zimepamba moto achilia mbali hila na fitna za Waingereza kuwatokomeza viong
 
Naanza kushawishika kujua ukweli wa hawa akina Sykes, nini hasa kilikuwa kikwazo cha wao kujumuishwa kwenye serikali ya Tanganyika baada ya Uhuru? Nini kilitokea kati yao na Nyerere hadi kuwepo na hizi fununu kwamba ‘walifutwa’ kwa makusudi kwenye historia ya Uhuru wa Tanganyika....bado natafakari.
 
Wazalendo wa nchi yetu ambao wamesahaulika.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi,ipo siku historia halisi ya Tanganyika itafunuliwa kwa wote waone na waisome.tusikate tamaa tunaopenda ukweli na haki usimame mbele daima
 
Thread imeharibika kwa propaganda na kumaliza kabisa legacy yake badala ya kui cherish.
 
labda mwandishi wa thread hii angeongeza uhondo kwa kusema what went wrong hadi akafutwa kwenye historia kwani muandishi wa thread anaonekana anamjua vizuri sana huyu bwana sykses!!! ila sijaelewa inaposemekana kua hawa kina sykes wamefutwa ktk historia si hadi 90's kuna sykes alikua ni mkuu wa mkoa wa dar au ni kukumbukwa kupi kunako zungumziwa??
 
mkuu kitendo cha hata kutokumbukwa kama mashuja wa nchi,kwani ni kati ya waliopigania uhuru wakiwa mstari wa mbele ni kielelezo
na ukiangalia siku ya uhuru desemba 9 kunakuaga na kumbukumbu na tunapewa historia kuhusu nchi yetu kwenda uhuru,hutosikia akitajwa na wenzake wengi waliokua wakipigana bega kwa bega na Nyerere kudai uhuru.katika historia ataonekana kama nyerere alisimama peke yake mpaka akawashinda wakoloni kitu ambacho si kweli
hii nadhani kuna haja ya kurekebisha hii kitu
 
Mwandishi umejitahidi sana kutujuza historia ya Ally Skyes na mchango wake. Ninapata shida kukuelewa ni kwa jinsi gani familia hii imepuuzwa, maana umeorodhesha majina mengi tu kama vile kina Vedasto ambao leo hii ndo tunaanza kusikia habari zao katika mchango wao wa kutafuta uhuru wa watanzania. katika mjumuisho wako umezungumzia tu Skyes kama mtu aliye sahauliwa je kina vedasto una waweka kundi lipi na kwa nini nao pia usiwazungumzie kinaga ubaga kama bwana sykes?.

Nina wasiwasi kuwa propaganda unayoiendesha ina ajenda ya siri, Sisi watanzania tunawaenzi wote waliotutafutia huu uhuru na mwisho " siku zote binadamu hajitengenezei jina wala umaarufu bali matendo yake yanalitengeneza jina lake hata akifa anakuwa bado anaishi" hivyo basi kwa simulizi uliyotoa ninaimani sykes hajafa anaongea.
 
We kahinda rejea kichwa cha habar cha hii thread inahusu nini sio unaongea tu bila kuelewa umesoma nin kama angeandika kuhusu vedasto angeandika makala yake, hakuna ajenda ya siri hapo ni matatizo yako binafsi ya kutafsiri mambo knyume na kwa mtazamo huo mambo mengi utayatafsiri kinyume na utapotosha mengi...
Topic ni; Ally kleist sykes sio vingine
 
Hawa ndio wale mashujaa waliofunikwa majina yao na sifa zao na MFUMO KRISTO!
Mungu awalaani waanzilishi wa mfumo kristo TZ!
AMIN.
 
subhanallah.mungu amjaze rehma.duh kumbe siijui tanzania japo nimekaa darasani mpaka nikawa na degree.Ally sykes from today on wards nimekuingiza kwenye memory cells zangu.nimexoma historia ya tanzania university duh huwezi amini wanaogelea uchumi tu.mkuu mohamed said naomba utuletee sababu ya uhasama mbaya na Nyerere.kumbe hata nyerere simjui vyema
 
Akhi l kareem ubaya aliokuwa nao Ally sykes na mashujaa wenzake ni KUWA WAISLAMU TU! baaas!
Yule muasisi wa mfumo kristo alichukia waislamu toka amezaliwa huko butiama mpaka siku anakufa!
Laana tullaah!
 
Back
Top Bottom