Pamoja nakuwa ulikusudia kuuhabarisha umma juu ya msiba huu,
Lakini upotoshaji wa aina hii usiachwe upite bila kusahihishwa!
AA imeundwa 1929 chini ya Mwalimu Cesil Matola,
1933 AA ilimkasimisha madaraka katibu wake bwana Klest Sykes, hii ni baada ya Matola kufariki,
Mwaka 1948 Klest Sykes anaasisi TAA, na mwaka huohuo anapinduliwa na Daktari kijana Vedasto Kyaruzi anashika urais wa TAA,
Katibu anakuwa Abdul Sykes kaka wa Ally Sykes,
Mwaka 1950 Dr Kyaruzi anahamishwa kikazi kwa nguvu na muingereza nakupelekwa Nzege hiyo ikiwa ni mikakati ya mkoloni kukidhoofisha chama cha TAA, baada ya hapo nafasi ya urais inakaimiwa na Abdul Sykes.
Mwaka 1953 uchaguzi unafanyika na Julius Nyerere anamshinda Abdul Sykes katika uchaguzi huo, hivyo Julius anakuwa rais wa TAA,
Mwaka unaofuata yani 1954 TAA inabadilishwa jina nakuwa TANU na uchaguzi unafanyika tena, Julius Nyerere na Abdul Sykes wanashindana katika kinyang'anyiro hicho na Julius Nyerere anaibuka kidedea hivyo kuwa rais wakwanza kwa TANU,
Hilo likaenda mpaka 1958 katika uchaguzi maarufu kama kura tatu, uliofanyikia jimbo la magharibi (Tabora) Nyerere tena akashinda,
Baada ya hapo Abdul Sykes alijitenga na siasa na kuanzisha chuki dhidi ya viongozi wa TANU hasa Julius Nyerere,
Baada ya uhuru kupatikana, kundi lililokuwa likimuunga mkono Abdul Sykes lilianzisha UASI dhidi ya serikali halali ya TANU,
Kundi hilo lilikuwa na watu wengi walitoka TAA na TANU hasa Shehe Takadir, Shehe Hassan Bin Amir, na wengine wengi!
Kundi hilo baada yakufeli mission yao kisiasa sasa liliamua kutumia misikiti kupandikiza chuki yao,
Chuki hiyo ndio inayoliathiri taifa mpaka hii leo na Ritz ukiwa ni muathirika wayo!
Kufuatia hali hiyo, mkono wa dola ukaanza kuwaandama tena kwa nguvu hii ilifuatiwa na kuunda sheria ya kuweka mtu kizuizini ya mwaka 1962,
Sasa kusema Ally Sykes ndie muasisi wa TAA na TANU ni UONGO
Ally Sykes katika uhai wake hajawahi kushika nyadhifa yoyote ya kisia, kikundi ama jumuiya!
Neno zuri lakutumia nikama ulivyoanza na kichwa cha taarifa hii kuwa MMOJA wa waasisi wa TANU na sio TAA