Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakati mwingine bora uwe msomaji unaweza kujifunza kitu kuliko kuropoka ovyo hawa wazee baada ya TANU wakapunzika baada ya historia kuwafuta.Huyu ana bahati chama kinakufa naye anakufa kuzikwa ndo yeye atatangulia. Rip ccm rip skykes
kipindi kirefu nilikuwa najiuliza chimbuko la Cleist Sykes wakati wao ni waislamu kumbe inaonekana babu yao wa kabila la wazulu alipofika Tanga na kumwoa Mnyaturu alibadilisha dini kutoka ya jadi au kiristo kwenda Uislamu ama kutoka mpagani kwenda Uislamu. Tangu hapo majana yao ni mchanganyiko wa majina ya kiislamu na kikristo.
Huyo hapo chini anaezungumza ni Ally Sykes nakuomba msikize msome kwa makini sana:Wasifu wa marehemu ni muhimu sana hususan kipindi hiki alichofariki Ally Sykes kinaweza kutumika vema kusahihisha historia iliyopotoshwa?
Tukumbuke waombolezaji wengi hufuatilia kwa karibu wasifu wa marehemu yeyote kipindi cha maandalizi ya mazishi.
YERICKO NYERERE yuko sahihi kabisa kuionyesha historia anayoijua. Kufa kwa mtu hakutakiwi kuacha makovu ya historia ndio sababu wasifu wa marehemu husomwa mbele ya watu wengi ili kama kuna uongo utazungumzwa na kusahihishwa.
Innalilah Wainnalaihy Rajuun ( IWR) ....ALLY SYKES.
Amen. Njia iliyobaki ya kuwaenzi wazee hawa ni kuihuisha TANGANYIKA basi.Apumzike anapostahiri.
Inasikitisha namna vyombo vya habari vilivyoupuuza msiba huu, Hii ni ishara ya upofu uliogubika Historia ya Nchi yetu.
Nafikiri tujikite kutoa Pole na kufuatilia kujua taratibu za msiba n.k. Haya ya uraia nk tuyaache.
Na huu ndiyo utamaduni wa Kiafrika, msiba ukiisha tuyajadili na mengine.
Nafikiri tujikite kutoa Pole na kufuatilia kujua taratibu za msiba n.k. Haya ya uraia nk tuyaache.
Na huu ndiyo utamaduni wa Kiafrika, msiba ukiisha tuyajadili na mengine.
Ilongailunga,
Ni kweli usemayo ndugu yangu.
Ukiangalia mifano ya wenzetu khasa nchi za Ulaya Magharibi,wanatunza na kuenzi mno Historia zao na Wazee/Mashujaa wao.
Kuna Vizee vya nchi hizo,baadhi yao walikua ni maaskari kwenye WWII. Lakini hata mistari ya mbele ya vita hawakufika,labda walikua ni wapishi, makarani au wengine walikua ni Makuwadi tu wa kuwatafutia Vibinti vya kujipumzishia wale walokua Majemedari wakubwa.
Lakini ukiona hizo hishma na taadhima wapewazo utastaajabu.
Sasa huyo Bwana Ali Sykes,alikua ni mmojawapo wa waasisi wa Chama kilicholeta Uhuru kwenye Taifa/Nchi. Tena si yeye tu peke yake,ni Family yao woote....yaani Baba yao na Wanae/watoto wake woote.
Afrika/Tanzania inasikitisha mno.
Shukran.
Cc;Ritz
huyu ndo baba ake na Dully sykes.........
R.I.P mzee Ally
...salute..! sijui kuna kitu gani baina yako na ritz..lkn nimeguswa mno na hii posting yako..that was Malcom X way..!....na ni kihivi tutaleta second liberation ya motherland..! kwa mara ingine tena..salute..!you, ritz and all of us, let almight guide and guard us in a way which is of less confrotation...!...stay blessed bro!
Ee m/mungu msamehe na umrehemu na makazi yake yawe peponi, ee m/mungu ikiwa marehemu ni mwema basi mzidishie katika wema wake na akiwa ni muovu amfanyie wepesi katika maovu yake.