Ijue Historia ya muasisi wa TANU, Ally Kleist Sykes (1926 - 2013)

Ijue Historia ya muasisi wa TANU, Ally Kleist Sykes (1926 - 2013)

Ilongailunga,

Ni kweli usemayo ndugu yangu.

Ukiangalia mifano ya wenzetu khasa nchi za Ulaya Magharibi,wanatunza na kuenzi mno Historia zao na Wazee/Mashujaa wao.

Kuna Vizee vya nchi hizo,baadhi yao walikua ni maaskari kwenye WWII. Lakini hata mistari ya mbele ya vita hawakufika,labda walikua ni wapishi, makarani au wengine walikua ni Makuwadi tu wa kuwatafutia Vibinti vya kujipumzishia wale walokua Majemedari wakubwa.

Lakini ukiona hizo hishma na taadhima wapewazo utastaajabu.

Sasa huyo Bwana Ali Sykes,alikua ni mmojawapo wa waasisi wa Chama kilicholeta Uhuru kwenye Taifa/Nchi. Tena si yeye tu peke yake,ni Family yao woote....yaani Baba yao na Wanae/watoto wake woote.

Afrika/Tanzania inasikitisha mno.

Shukran.

Cc;Ritz

Kuna mfuasi wa Chadema anaitwa dudus, anasema Ally Sykes hana mchango wowote nchini kama huo msiba ni wa familia yake siyo taifa.

Bahati mbaya Watanzania hawajuhi chochote kuhusu historia ya Tanganyika.

Inasikitisha sana...
 
Huyo hapo chini anaezungumza ni Ally Sykes nakuomba msikize msome kwa makini sana:

''In 1953 the TAA leadership elected him (Nyerere) to stand against the incumbent President, my brother Abdulwahid. On 17 April 1953 election was held at Arnautoglo Hall between Abdulwahid and Nyerere. Abdulwahid lost the election by a very narrow margin. In June we announced our executive committee: J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and I was Assistant Treasurer. Committee members were Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1] Nyerere became TAA President and Abdulwahid became his Vice-President.''

How much is the narrow margin? kwa nini isitajwe tu.

Hata maalim Seif anasema hivyo huko zanzibar, angalau tunajua ni 49% CUF kwa 51% CCM
 
Kuna mfuasi wa Chadema anaitwa dudus, anasema Ally Sykes hana mchango wowote nchini kama huo msiba ni wa familia yake siyo taifa.

Bahati mbaya Watanzania hawajuhi chochote kuhusu historia ya Tanganyika.

Inasikitisha sana...

Shariff Ritz,

Kama kuna ndugu zetu wa aina hiyo ni uzuri kuwa nao karibu na kuwaelewesha majambo kwa kituo na utuvu.

Kwani mbona Yericko Nyerere,pamoja na "matata yake" yoote lakini tupo nae na tunakwenda nae taratibu kwa hila,maarifa na utuvu na sasa aelekea kunyooka,kufahamu na kukubali japo kwa shingo upande; Historia anayofundishwa na Maalim Sheikh Mohammed Said.

Kwa hiyo mimi nashauri tusiwatupe au kuchoka kuwafahamisha na kuwasomesha ndugu zetu hawa Historia yao ya Tanganyika na Zanzibar ilokua imefichwa makusudi kwa miaka mingi mno.

Waswahili tuna msemo;"Tikiti bovu li Shambani mwako".

Ahsanta kwa kunisikiza.
 
Inasikitisha namna vyombo vya habari vilivyoupuuza msiba huu, Hii ni ishara ya upofu uliogubika Historia ya Nchi yetu.

Historia ya nchi yetu haiwezi kutukuzwa kama tutaendelea kuwashindanisha wapigania uhuru kwa ubora. Ni wengi wetu tumesahau mchango wa machifu wengi tu waliopigana na mkoloni na kuwaona wa maana waliopambana na mkoloni siku za miaka ya mwisho ya kuelekea uhuru. Nani anawakumbuka akina Mkwawa, mangi, Kingeketile, Abushiri????????

Wangapi sasa wanamkejeri nyerere ili wapate mshindani wake???? ni kwa nini tusichambua historia ya kila mmoja na kuwaacha wananchi watambue mchango wao????

Binafsi sitaona tofauti yoyote kati ya Nyerere, Sykes na machifu wetu waliopigania ukombozi wa taifa hili kila mtu kwa zama yake. Lakini naamini bila msingi wa mapambano dhidi ya mkoloni uliowekwa na machifu na watemi, Wapigania uhuru wa enzi za Nyerere, Sykes na wenzao wangekuwa na kazi kubwa na ngumu ya kupata uhuru mwaka 1961.
 
Ha ha ha! Nimeshauri mambo ya familia yaishie kwenye familia. Ally Sykes ni mtu mdogo sana kwenye siasa za nchi hii; huo ndio ukweli hata kama hupendi kuusikia. Tunatoa pole kwa sababu ni binadamu mwenzetu katutoka lakini sio kwa kuwa ni maarufu kihivyo. Natumaini umeelewa.

If I may ask........mzalendo na mwanasiasa wanatofauti gani?????
Akifa mtu mkubwa kwenye siasa za nchi hii wewe ndo utaona ni sawa kuwekwa taarifa hapa!!!!?????

Acha sisi tunaothamini uzalendo wa kweli juu ya uanasiasa tushughulike na uzi na kifo hiki
 
Ilongailunga,

Ni kweli usemayo ndugu yangu.

Ukiangalia mifano ya wenzetu khasa nchi za Ulaya Magharibi,wanatunza na kuenzi mno Historia zao na Wazee/Mashujaa wao.

Kuna Vizee vya nchi hizo,baadhi yao walikua ni maaskari kwenye WWII. Lakini hata mistari ya mbele ya vita hawakufika,labda walikua ni wapishi, makarani au wengine walikua ni Makuwadi tu wa kuwatafutia Vibinti vya kujipumzishia wale walokua Majemedari wakubwa.

Lakini ukiona hizo hishma na taadhima wapewazo utastaajabu.

Sasa huyo Bwana Ali Sykes,alikua ni mmojawapo wa waasisi wa Chama kilicholeta Uhuru kwenye Taifa/Nchi. Tena si yeye tu peke yake,ni Family yao woote....yaani Baba yao na Wanae/watoto wake woote.

Afrika/Tanzania inasikitisha mno.

Shukran.

Cc;Ritz
\
Tunayoona leo kwa Ally sykes na Nyerere baada ya kifo chake tutayaoona kwa wengi tu ni matokeo yetu wote kuwapuuza wapigania uhuru kwa misingi ya dini zetu. Kila mmoja wetu anataka kuutambua upigania uhuru kwa misngi ya dini na matokeo yake ipo siku taifa hili litakosa historia moja ( single history) ya wapigania uhuru.

Ni nini kama sio makusudi kuuzika mchango wa machifu na watemi ambao wengi wao hawakuwa na dini? ama waliabudi dini za jadi.
 
Kuna mfuasi wa Chadema anaitwa dudus, anasema Ally Sykes hana mchango wowote nchini kama huo msiba ni wa familia yake siyo taifa.

Bahati mbaya Watanzania hawajuhi chochote kuhusu historia ya Tanganyika.

Inasikitisha sana...
.

Je, umeawahi kukutana na watu hapa JF wanasema Nyerere hakuwa na mchango wowote? na wala si baba wa Taifa? Ni wengi tu. Kama tumeruhusu kumtukana Nyerere huku tukiamini tunatengeneza njia sahihi ya kutowatukana wengine ni kujidanganya. Nyerere hawezi kutukanwa ili kuandika historia sahihi ya Sykes family bali historia ndio inaweza kusahihishwa ili kuinyoosha kwani kwa sasa Nyerere na Sykes hawapo tena. Mwendelezo wa kuwabeza wapigania uhuru utaendelea hadi pale ambapo watanzania tutawaona kwamba walijitolea damu na jasho lao kwa niaba ya watanzania wote na si imani au dini zao.

Ritz, tuwe wakweli hali hii itaendelea na mwisho kizazi kijacho kitasema Nyerere na Sykes so what? watoto wetu watasema wafu waache wazikane na walio hai waache waangalie dunia yao.
 
Shariff Ritz,

Kama kuna ndugu zetu wa aina hiyo ni uzuri kuwa nao karibu na kuwaelewesha majambo kwa kituo na utuvu.

Kwani mbona Yericko Nyerere,pamoja na "matata yake" yoote lakini tupo nae na tunakwenda nae taratibu kwa hila,maarifa na utuvu na sasa aelekea kunyooka,kufahamu na kukubali japo kwa shingo upande; Historia anayofundishwa na Maalim Sheikh Mohammed Said.

Kwa hiyo mimi nashauri tusiwatupe au kuchoka kuwafahamisha na kuwasomesha ndugu zetu hawa Historia yao ya Tanganyika na Zanzibar ilokua imefichwa makusudi kwa miaka mingi mno.

Waswahili tuna msemo;"Tikiti bovu li Shambani mwako".

Ahsanta kwa kunisikiza.

Historia haiwezi kusemekana kuwa imefichwa kama haipo iliyoandikwa na kupotoshwa. Ni ipi iliandikwa ikapotoshwa?

Kimsingi, siamini kwa hakika kwamba hata historia ya Nyerere imeandikwa. kazi za nyerere zaidi ya 75% haziko kwenye maandishi na bahati mbaya hakuwahi kuweka document ya mikono yake ambayo pengine ingekuwa msingi wa yeye kutotambua mchango wa wenzake au kumlaumu kwamba hakuweka sawa au alipotosha historia ya wengine.

kinachotusumbua hapa watanzania ni dini zetu si upigania uhuru. kama ingekuwa ni upigania uhuru tungeanza kumlaumu Nyerere kwa kupuuza mchango wa watemi na machifu wetu katika mchango wao kupambana na wakoloni. wapo Watemi na machifu waliotoa uhai wao waliojinyonga au kufa katika vita hivyo lakini leo hii yule aliyetoa nyumba ya kuishi nyerere au aliyetoa mchango wa gari la kupigania uhuru ndiye anatukuzwa pekee. Hii yote mwisho wake historia ya baba na mama zetu waliopigania uhuru haina mwisho mwema.
 
R.I.P,Ina llilaha waina illah rajuun,nitakukumbuka kweli na vimbwanga vyako vya pale ofcn
 
Kungekua na matunda ya uhuru asingefia Nairobi kwenye hospitali za kigeni. Angefia Muhimbili au Lugalo. Matunda ya uhuru ni pamoja na hospitali bora.

R.I.P Muasisi.

Matunda ya uhuru mlioupigania tunayaona na kuyathimini.

Tutawaenzi kwa kuulinda uhuru siku zote.
 
Waliopo karibu watuambie saa ya kuelekea makaburini Kisutu ili wengine pia tusogemee kushiriki na waombolezaji wenzetu. Mimi nikiwa mmojawapo.
 
Mkuu Ritz nami nitumie ukumbi huu kufikisha pole zangu kwa msiba wa huyu mzee. Hawa ni baadhi ya makamanda waliobaki ambao naona wanaishia kila kukicha na bahati mbaya sioni makamanda wengine wakija kuchukua nafasi zao.
 
Last edited by a moderator:
.

Je, umeawahi kukutana na watu hapa JF wanasema Nyerere hakuwa na mchango wowote? na wala si baba wa Taifa? Ni wengi tu. Kama tumeruhusu kumtukana Nyerere huku tukiamini tunatengeneza njia sahihi ya kutowatukana wengine ni kujidanganya. Nyerere hawezi kutukanwa ili kuandika historia sahihi ya Sykes family bali historia ndio inaweza kusahihishwa ili kuinyoosha kwani kwa sasa Nyerere na Sykes hawapo tena. Mwendelezo wa kuwabeza wapigania uhuru utaendelea hadi pale ambapo watanzania tutawaona kwamba walijitolea damu na jasho lao kwa niaba ya watanzania wote na si imani au dini zao.

Ritz, tuwe wakweli hali hii itaendelea na mwisho kizazi kijacho kitasema Nyerere na Sykes so what? watoto wetu watasema wafu waache wazikane na walio hai waache waangalie dunia yao.

Hakuna anayepinga mchango wa Nyerere kwenye TAA, TANU, CCM, kafanya mengi mazuri kwa sehemu yake mchango wake unajulikana, lakini bahati mbaya hawa wenzake historia zao zao zimewatupa.

Kuhusu machifu mbona mchango wao unajulikana katika harakati za uhuru.

Chifu Kidawa, Chifu Mariale, Chifu Makwaiya.
 
Mkuu Ritz nami nitumie ukumbi huu kufikisha pole zangu kwa msiba wa huyu mzee. Hawa ni baadhi ya makamanda waliobaki ambao naona wanaishia kila kukicha na bahati mbaya sioni makamanda wengine wakija kuchukua nafasi zao.

Mkuu Kimbunga,

Huu msimba ni wetu sote tumuombee mzee wetu, Ally Sykes.

Amebakia Balozi Abbas Sykes naye umri umekwenda sasa.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna anayepinga mchango wa Nyerere kwenye TAA, TANU, CCM, kafanya mengi mazuri kwa sehemu yake mchango wake unajulikana, lakini bahati mbaya hawa wenzake historia zao zao zimewatupa.

Kuhusu machifu mbona mchango wao unajulikana katika harakati za uhuru.

Chifu Kidawa, Chifu Mariale, Chifu Makwaiya.

Tuwe wakweli, wapo wanaobeza mchango wa Nyerere hata kudadisi ni nani alimpatia ubaba wa taifa na ndivyo watabeza wa wengine wote. Hakuna atakayesalimika kubezwa kwa hali ninavyoiona. Nisieleweke vibaya sina maana hata kidogo kuwa Nyerere hakuwahi kukosea kama ambavyo wapo ambao hawataki kudadisi ni nini kilimkosanisha Nyerere na baadhi ya wapigania uhuru wenzake kama akina Oscar kambona na wengine. Tumekuwa tunajadili zaidi mfarakano wa wapigania uhuru kuliko chanzo cha kufarakana. kuanzia hapo ndipo tunaegemea upande.

Ritz, Familia za hao machifu zikoje hivi sasa baada ya uhuru pamoja na mchango wao mkubwa uliochangia kutoa uhai wao? siwasikii watoto au wajukuu wa akina mirambo, abushiri na wengine kwenye siasa za nchi, kwenye biashara wala utajiri au kupewa madaraka na serikali kwa ajili ya kuenzi mchango wa babu zao. Darasani vitabu vimewasema kwa uchache sana ukilinganisha na kazi ngumu waliofanya machifu na watemi wakati wa kupigania uhuru.

Ritz, kuna mzee Secil matola tunaambiwa ni kiongozi wa kwanza wa African Association ( 1929 - 1933) na Dr. Vedasto Kyuruzi ( 1948 - 1950). kwa mara ya kwanza nimesikia hapa JF kwa YERICKO NYERERE mbona historia zao pia kwa wanaoamini 'zimefichwa' lakini wanaopiga kelele za akina Sykes hawasemi kitu kuhusu hawa? walikwenda wapi hata kwenye vitabu vya shule sijawahi kuwasikia? naomba kukumbushwa ni vitabu vya darasa la ngapi vimetoa historia hii pengine nilikuwa kilaza.
 
Okoo Wa sykes umetengwa wanaokula matunda ya uhuru wengine

Ukitaka kuhakiki kwa kina kutengwa kwa mpigania uhuru ni lazima kuwapitia wote bila ubaguzi acha Nyerere aliyekuwa juu kwani yeye kwa nafasi yake alisikika zaidi. Utakuta si familia ya sykes tu na pengine wapo waliokuwa hali mbaya kuliko hao akina sykes.

Unajua ziliko familia za akina SECIL MATOLA na DK. VEDASTO KYARUZI. Je, umewahi hata kuzisikia? Yumkini sykes wamesikika japo kwa mbali kuliko hao?

Wazee wetu wa zamani walikuwa wanatoa maisha yao kwa taifa kuliko familia zao, dini zao au kabila zao na ndio maana wengi hujawasikia wakipaza sauti sana kulalamika. hatujasikia wajukuu wa watemi na machifu wakidai fidia za babu zao waliokufa vitani kulikomboa taifa letu. HII NAYO NI HOJA.
 
Back
Top Bottom