Huyo shetani kwa wazungu hayupo?
Siyo Kwa wazungu tu. Yuko duniani kote na kila nchi. Waliofanikiwa kupata ufahamu huu, walishamdhibiti na hawasumbui kama afanyavyo kwenye baadhi ya mataifa walio bado gizani, Tanzania ikiwemo!
Mijitu myeusi ni hasara tupu.
Umesema wewe. Na hasara hiyo uliyojitamkia mwenyewe na iwe kwako peke yako.
Sisi wengine tuna uelewa na ufahamu na ndiyo maana nimekufunulia siri hii
Po pote pale duniani mambo ni yale yale tu - ubinafsi, uvivu, ufisadi wa kinyama, ushirikina...and the list goes on and on.
Haya ndiyo matokeo (products) ya uwepo wa nguvu hiyo inayotawala nchi au taifa fulani
Halafu badala ya kutafuta suluhisho mtambuka unakuja na ngonjera za mapepo na shetani.
Suluhisho ndilo hilo. Kama huamini kuwa hilo ndilo suluhisho, basi wewe chukua bunduki kapambane na hao wanaofanya maamuzi tusiyoyapenda na tunayoyalalamikia uone kibano utakachokipata na bado utaendelea kutawaliwa na wao na kukufanya watakavyo..!
Huko nchi za Scandinavia hakuna mapepo? Walioendelea na kujenga transparent societies wakaushinda ufisadi huko shetani hayupo na mapepo hayafiki? Kwamba hawa wanaochota haya matrilioni siyo wao bali ni shetani na mapepo? Jizazi 😳😳😳
Nisome huko☝️☝️☝️ juu nimeeleza kwa ufasaha na Kwa lugha rahisi.
All in all, ninachokiona kwako ni "
ujinga wa kiroho" ndio unaokusumbua.
Unahitaji shule kubwa ili uelewe uhusiano uliopo kati ya
ulimwengu wa roho (spiritual realm) na
ulimwengu wa mwili (physical world)..
Kwa kifupi tu ni kuwa, ukishadhibitiwa ktk ulimwengu wa roho kuwa vile utakavyo, hakuna utakachofanya ktk ulimwengu wa mwili kikawa..!
Fanya utafiti ktk nchi zilizokwishapiga hatua za maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Utagundua kuwa walishaigundua siri hii miaka mingi iliyopita na kuifanyia kazi...
Kama ni hivi basi hakuna matumaini kwa mtu mweusi aisee - iwe ni Afrika, visiwa vya Caribbean, Australia, Haiti na kwingineko!
Matumaini yapo..
Kubali tu na kisha tii
kanuni na
taratibu za ki - Mungu na kufanya sawasawa na anavyoelekeza...
Tupambaneni na shetani na mapepo ili kutokomeza ufisadi !!!
Absolutely, big YES..!
Unaonekana kama umeandika na kutamka kimzaha lakini nikuhakikishie kuwa,
hili ndilo jibu..
Ufisadi ni
tendo na ni
tabia ya kishetani. Na Kila afanyaye hilo, basi huyo ni wa shetani.
Na kwa hiyo kama wewe au baba yako au mama yako au nduguyo au rafikio yeyote anafanya ufisadi, basi tambueni kuwa nyie nyote baba yenu ni shetani..!!
Bila shaka umenielewa sasa, au siyo Mr
Shimba ya Buyenze??