Ijue Kibera- Nairobi, Kenya:- Moja ya makazi duni ya mabanda (slums) makubwa 10 katika dunia

Bongo pia yapo maeneo ya hivyo ila kwa sasa wengi wamewaandikisha TASAF na kuwajengea nyumba za kisasa hio ndio imekua ponapona yao bila hivyo msingekua mnaicheka Kibera wakati kwenu pia ndio hivyo hivyo
Umaskini upo Tanzania lakini siyo kwa kiwango cha Kenya.

Wewe iulize Google ikupe "Top 5 largest slums in the world" , utaikuta Kibera ya Kenya ni namba 2.

Tanzania haina slums za sampuli ya Kibera
 
Zipo ila TAFAS imeokoa Jahazi sasa hivi wanajengewa kaya masikini
 
Iko Nairobi yapata km 10 kutoka CBD ya Nairobi;-
View attachment 3335056

Kibera inajulikana kwa umaarufu wake kama moja ya mitaa ya mabanda mikubwa na maskini zaidi duniani. Hakuna idadi kamili ya watu wanaoishi Kibera, lakini makadirio yanatofautiana kutoka watu 700,000 hadi milioni moja. Katika Kibera, msongamano wa watu ni wa kawaida na hali za maisha ni duni. Katika kitongiji hiki kikubwa zaidi cha mabanda barani Afrika, hali za makazi na vyoo ni duni na visivyo salama kiafya, matumizi ya pombe kupindukia na uhalifu ni hali ya kila siku, na upatikanaji wa umeme pamoja na maji safi ni mdogo.

View attachment 3335060

Wakazi wa Kibera wanaishi katika vibanda vidogo vilivyotengenezwa kwa kuta za tope na paa za mabati. Kila kibanda kina ukubwa wa futi 12 kwa 12 na kinaweza kukaliwa na watu hadi wanane kwa pamoja. Vibanda hivi hukusanywa pamoja kwenye viwanja (plots), na viwanja vingi havina vyoo. Kwa kuwa wakazi wengi wa Kibera hawana huduma ya vyoo, hulazimika kujisaidia barabarani au kando ya reli kuu inayopita katikati ya mtaa huo wa mabanda. Hali hii husababisha matatizo makubwa ya usafi wa mazingira.

Mifereji ya wazi ya majitaka pia ni jambo la kawaida. Ikiwa kiwanja ni kikubwa zaidi, ambacho kawaida huhusisha familia 50, basi kutakuwa na choo kimoja cha pamoja kwa kiwanja kizima. Mara choo kinapojazwa, wavulana huajiriwa kukisafisha na kukitoa taka. Kazi hii hufanyika kwa kuchukua kinyesi na kukimwaga mtoni. Mbinu hii si salama kiafya kwa wanaokusanya taka hizo, na pia huchafua vyanzo vya maji vilivyo karibu.

Angalizo:
Wakenya wakiona Magorofa ya CBD Nairobi hawakumbuki kuwa wanaishi Kibera au Mathare au Mukuru kwa Njenga
Kwenye chaguzi kubwa hapo Kenya hii ni moja ya maeneo yanayokumbwa mno na machafuko ya kisiasa au magenge ya uhalifu kama vile Mungiki.
 
Siyo kweli, umeng'ang'ana na tasaf, tasaf wamejenga nyumba wapi,hela ya tasaf unaijua!?..hela ya kununua kuku mmoja ufuge!!.. tanzania hakuna slams, manzese palikua slams sasa hivi pamejaa maghorofa
Ndio maana nakwambia wanaziboresha km hujui kuhusu TASAF kaa hivyo hivyo na km hujaona waliojengewa vibanda vyao sasa hivi wanaishi kwenye nyumba za kisasa basi kaa hivyo hivyo au unataka tukuwekee picha na video za before and after?
 
Iko Nairobi yapata km 10 kutoka CBD ya Nairobi;-
View attachment 3335056

Kibera inajulikana kwa umaarufu wake kama moja ya mitaa ya mabanda mikubwa na maskini zaidi duniani. Hakuna idadi kamili ya watu wanaoishi Kibera, lakini makadirio yanatofautiana kutoka watu 700,000 hadi milioni moja. Katika Kibera, msongamano wa watu ni wa kawaida na hali za maisha ni duni. Katika kitongiji hiki kikubwa zaidi cha mabanda barani Afrika, hali za makazi na vyoo ni duni na visivyo salama kiafya, matumizi ya pombe kupindukia na uhalifu ni hali ya kila siku, na upatikanaji wa umeme pamoja na maji safi ni mdogo.

View attachment 3335060

Wakazi wa Kibera wanaishi katika vibanda vidogo vilivyotengenezwa kwa kuta za tope na paa za mabati. Kila kibanda kina ukubwa wa futi 12 kwa 12 na kinaweza kukaliwa na watu hadi wanane kwa pamoja. Vibanda hivi hukusanywa pamoja kwenye viwanja (plots), na viwanja vingi havina vyoo. Kwa kuwa wakazi wengi wa Kibera hawana huduma ya vyoo, hulazimika kujisaidia barabarani au kando ya reli kuu inayopita katikati ya mtaa huo wa mabanda. Hali hii husababisha matatizo makubwa ya usafi wa mazingira.

Mifereji ya wazi ya majitaka pia ni jambo la kawaida. Ikiwa kiwanja ni kikubwa zaidi, ambacho kawaida huhusisha familia 50, basi kutakuwa na choo kimoja cha pamoja kwa kiwanja kizima. Mara choo kinapojazwa, wavulana huajiriwa kukisafisha na kukitoa taka. Kazi hii hufanyika kwa kuchukua kinyesi na kukimwaga mtoni. Mbinu hii si salama kiafya kwa wanaokusanya taka hizo, na pia huchafua vyanzo vya maji vilivyo karibu.

Angalizo:
Wakenya wakiona Magorofa ya CBD Nairobi hawakumbuki kuwa wanaishi Kibera au Mathare au Mukuru kwa Njenga
Nenda lost city iliyopo mexico city, mexico au dharavi slum ilyopo mumbai/bombay india ndiyo utapata tafsri halisi ya slum.

Hiyo kibera slum mbona ni uzunguni?
 
Bado Kibera iko kwenye top 3; angalia Google hapa;
Screenshot_20250516_213934_Google.jpg
 
Bado Kibera iko kwenye top 3; angalia Google hapa;
View attachment 3336443
Kwa takwimu mpya zinataja Kibera kuwa ndiyo numero uno kwa sasa duniani. Watu wengi hasa watanzania hudhani slums Kenya ni Kibera pekee kumbe sio kweli, Nairobi pekee ina ma slums zaidi ya 100 na mengine makubwa kuliko Kibera, Kenya ni nchi ya hovyo mno zaidi unavyoweza kufikiri.
 
Back
Top Bottom