Ijue Kibera- Nairobi, Kenya:- Moja ya makazi duni ya mabanda (slums) makubwa 10 katika dunia

Ijue Kibera- Nairobi, Kenya:- Moja ya makazi duni ya mabanda (slums) makubwa 10 katika dunia

Shida yetu wa Tz tunaamini kila kitu kibaya kipo Tanzania hata kama sio kweli.

Sisi hata Top 20 hatuingizi Slums yoyote ile

Sababu kubwa ni kuwa ardhi inamilikiwa na Serikali sio mtu binafsi.

Kenya hata nyumba za kupanga ni bei sana na Qulity ni ya kawaida mno.

Ukisema mazense unachoongelea ni msomgamano wa nyumba na sio Mabati au nyumba za mbao.
Na hayo maneo unayotaja ya hapa tanzania ni maeneo madogo sana katika hako ka eneo
Mfano ukitaja Mazense ni kaeneo kadogo vibaya mno ambako ni vijumba vidogo ila maneo mengi nyumba zipo za kawaida hadi hotel za nyota nne zipo
Watu hawajui slums n nini. Halfu wanadhani Manzese ya miaka 1980 ndiyo Manzese ya sasa. Manzese ina barabara za lami, Manzese ina mahoteli ya kisasa. Huwezi kulinganisha na Mathare au Kibera ya Nairobi hata kidogo.

Tanzania ni nchi ya fursa ambayo hata mtoto wa maskini anaweza kubadilisha maisha yake kwa kuwa ardhi ni mali ya Serikali, sisi tunakodishwa tu. Isitoshe ardhi yote ya Tanzania ni ardhi yenye rutuba. Wenzetu Kenya ardhi ni ndogo kwa kuwa kule kaskazini Turkana ni semi desert hivyo ardhi ya maana iko pwani, central province na Rift Valley. Na ardhi hiyo hiyo iko mikononi mwa wachache
 
mkuu angalia usipigwe humu, hela ya tasaf ijenge!?,yani unamaanisha laki 1,elfu 80,wengine mpaka elfu 50 ndo zijenge.watoaji wenyewe wanachowasisitiza wapokeaji ni kwamba wanunue mifugo ...
Mtu mmoja TASAF anapata 24,000 kila baada ya miezi 3.

Akiwa na wanafunzi ndio anafikisha Laki na nusu
 
Kenya ni uwanja wa mafisadi, na wana nguvu. Hakuna tajiri amewahi kushindwa kesi.
Ninakubaliana na wewe.
Just imagine, viongozi wa kisiasa badala ya kutuliza akili na kuona jinsi gani ya kuboresha maisha ya wananchi, wao wameshaanza kampeni za uchaguzi wa 2027.
 
Ninakubaliana na wewe.
Just imagine, viongozi wa kisiasa badala ya kutuliza akili na kuona jinsi gani ya kuboresha maisha ya wananchi, wao wameshaanza kampeni za uchaguzi wa 2027.
Ni ngumu sana kuboresha maisha ya Kenya.

Ile ni nchi ya Kibepari tangu enzi za Nyerere, watu walishagawana kila kitu.

Usitegemee Mkenya ambaye kazaliwa hana kitu atafanikiwa kutoka.

Labda apate bahati, ya kipaji au akatafute maisha nje ya nchi.
 
Kuna muda naamini bora Ardhi iwe mali ya serikali sio mtu binafs..
Mabepari hili swala hawalitaki ila watanzania tuna bahati na hicho kitu. Siku Ardhi inakuwa mali ya mtu kabisa Tutafikia hiyo hali na sisi
Kuna watu huwa wakiona maghorofa Kenya, bila kujua ni ya kina nani wanamponda Nyerere.

Nyerere alifanya kazi ya kitume sana nchi hii.
 
MK254 alikuaga na ubishi wa kishamba between TZ na kenya humu jf
Hasa enzi za COW, wakaunda ka umoja kao, Kenya, Uganda na Rwanda.

Agenda zao za SGR na EACOP zimekufa.

Wamebakiza Tourist visa na Ulinzi na usalama.

Ulinzi na Usalama sisi tuko SADC na Tourist visa hatuitaki.

SGR yetu iko FIRE na Bomba la Mafuta la Uganda, linakaribia kumalizika Tanga, mwisho wa mwaka huu.

Wametepeta.
 
Hasa enzi za COW, wakunda ka umoja kao, Kenya, Uganda na Rwanda.

Agenda zao za SGR na EACOP zimekufa.

Wamebakiza Tourist visa na Ulinzi na usalama.

Ulinzi na Usalama sisi tuko SADC na Tourist visa hatuitaki.

SGR yetu iko FIRE na Bomba la Mafuta Uganda, linakaribia kumalizika Tanga, mwiaho wa mwaka huu.

Wametepeta.
Kipindi iko anajiita lawmaina,now argues zote za kenya na TZ kaziacha,yupo kwenye masuala ya vita na udini
 
Kipindi iko anajiita lawmaina,now argues zote za kenya na TZ kaziacha,yupo kwenye masuala ya vita na udini
😅😅

Halafu hawa wahuni walikuwa wanatumia PLANS na renders tu.

Hawajawahi kuleta mradi serious humu kwenye debate.

Na wakati huo tulikuwa hatuijui Kenya vizuri. Walikuwa wanatuokota na GDP yao ya mchongo😅
 
Kuna watu huwa wakiona maghorofa Kenya, bila kujua ni ya kina nani wanamponda Nyerere.

Nyerere alifanya kazi ya kitume sana nchi hii.
Kweli mkuu, JKN ashukuriwe kwa sera yake ya ardhi, ujamaa na Kiswahili. Hivi vitu vimeifanya Tanzania kuwa unique, no matter what.
 
Iko Nairobi yapata km 10 kutoka CBD ya Nairobi;-
View attachment 3335056

Kibera inajulikana kwa umaarufu wake kama moja ya mitaa ya mabanda mikubwa na maskini zaidi duniani. Hakuna idadi kamili ya watu wanaoishi Kibera, lakini makadirio yanatofautiana kutoka watu 700,000 hadi milioni moja. Katika Kibera, msongamano wa watu ni wa kawaida na hali za maisha ni duni. Katika kitongiji hiki kikubwa zaidi cha mabanda barani Afrika, hali za makazi na vyoo ni duni na visivyo salama kiafya, matumizi ya pombe kupindukia na uhalifu ni hali ya kila siku, na upatikanaji wa umeme pamoja na maji safi ni mdogo.

View attachment 3335060

Wakazi wa Kibera wanaishi katika vibanda vidogo vilivyotengenezwa kwa kuta za tope na paa za mabati. Kila kibanda kina ukubwa wa futi 12 kwa 12 na kinaweza kukaliwa na watu hadi wanane kwa pamoja. Vibanda hivi hukusanywa pamoja kwenye viwanja (plots), na viwanja vingi havina vyoo. Kwa kuwa wakazi wengi wa Kibera hawana huduma ya vyoo, hulazimika kujisaidia barabarani au kando ya reli kuu inayopita katikati ya mtaa huo wa mabanda. Hali hii husababisha matatizo makubwa ya usafi wa mazingira.

Mifereji ya wazi ya majitaka pia ni jambo la kawaida. Ikiwa kiwanja ni kikubwa zaidi, ambacho kawaida huhusisha familia 50, basi kutakuwa na choo kimoja cha pamoja kwa kiwanja kizima. Mara choo kinapojazwa, wavulana huajiriwa kukisafisha na kukitoa taka. Kazi hii hufanyika kwa kuchukua kinyesi na kukimwaga mtoni. Mbinu hii si salama kiafya kwa wanaokusanya taka hizo, na pia huchafua vyanzo vya maji vilivyo karibu.

Angalizo:
Wakenya wakiona Magorofa ya CBD Nairobi hawakumbuki kuwa wanaishi Kibera au Mathare au Mukuru kwa Njenga
Kibera inaonyesha sura ya uroho na roho mbaya za viongozi wa Kenya wanaotembea kwa helkopta kwenda pale kusaka kura kana kwamba hawana macho. Shame on them.
 
Back
Top Bottom