Kabla ya kufananisha unapaswa ujiulize hiyo miji ilijengwa lini na sera na sheria zao za ujenzi vipoje?
Unawwza ukaenda Zanzibar pale mji mkongwe ukaanza kusema ni pa kishamba na mji umekaa kizamani wakati pale panahitajika kuendelea kuwa vile na pana sera na sheria kabisa kuhakikisha hapaharibiwi muonekano wake.
Au, utarajie miji inayojengwa hivi sasa China na Afrika kwa teknolojia na ubunifu wa kisasa utaka kuifananisha na London ambayo hata mtu aliyefariki miaka ya 1800 huko akirudi leo hii hatapata shida sana kuutambua mtaa na nyumbani kwao and they are proud.