Aisee mtaalam kwa mara ya kwanza kabisa naanza kuamini haya mambo ya nyota.
Hivi mwanaume akiwa ndoo alafu mwanamke simba wanaweza kuoana na kuishi kwa furaha ..maana mimi nna mpenzi wangu yeye simba alafu tuna migogoro sasa hivi?
Karibu mkuu, ndoo na simba ipo hivi:
Simba hupendezewa zaidi na matendo ya Ndoo kingono. Na ndoo huvutika zaidi kwa moto wa simba kimaisha hizi ni nyota mbili fahamu ya kuwa zina asili tofauti Moto wa mkaa kwa upepo wa kimbunga, lakini pia hali inaweza kuwa sawa ikiwa ndoo hawezi kuwa mkali kwa simba maana atavurugua maisha ya simba imagine umeweka jiko la mkaa ukaja upepo wa kimbunga, moto utawaka ikiwa upepo utakuwa wa kawaida na utawaka zaidi ikiwa utaongeza nguvu kidogo, lakini ukizidisha. Dunia itajua wameshindwana
Basically Simba huwa ni physical na Ndoo huwa ni mental simba hawezi kushilikiana na kutamani matakwa ya ndoo kwa sababu huona anamuharibia mipango na ndoo hapendi mabavu ya simba kupelekeshwa.
Wote ni wapenda ukubwa kwa sababu Ndoo ni King Jumamosi na Simba ni King jumapili sasa wafalme wawili hawawezi kukubali kuwa chini ya mwenzie
Ufalme wa Ndoo ni Uhuru na Mambo mapya ndio principle zake. Sasa simba ni Kupelekesha, ufahari na mabadiliko ya mitindo ya maisha pamoja na starehe,
Ndoo hupendelea watu wote.
Simba hujipendelea mwenyewe.
Hakuna maendeleo hapo ya ndoa zaidi ya baadae kusikia kila mtu ashike njia yake na hakuna ndoa hapa.
Labda muwe wachamungu na mwenyezi Mungu awanusurie. Lakini kama ibada za kudokoa na imani haba na uvumilivu hakuna, usijisumbue
Rakims