Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Ukiamini hizi mambo unakuwa kama mtumwa yani,unaweza usitoke kwako kisa umeambiwa Leo utakutana na balaa....
ukikuta kuna mtu anasema hivyo huyo kapapasa tu hivi mambo hajui chochote anachanganya na za kwake

Rakims
 
Nifanye nini ili nisafishe nyota yangu?
kuna mafusho hapo ili kuweza kusafisha nyota yako lazima ujue asili yake ni ipi na siku yake na mambo mengine ambayo nimeelezea hapo japo kuwa hapo kuna mafusho lakini jihadhari kununua fake

Rakims
 
Kiongozi kama ulipozaliwa ulipeowa jina fulani lakini baadae ukabadilisha jina ukaitwa jina jingine! Inakuaje hapo kwa suala la nyota?
Hapo unakuwa umegeuziwa mfumo mzima wa maisha ndio mfano nilioutoa hapo juu kwamba mtu akigeuza betri. nuksi zingine za kujitakia

Rakims
 
Asante sana
 

Unaweza kuitoa vipi elimu ya nyota kwa mtindo huu na ushirikina ?

Je Uislamu unaiweka mahala gani elimu hii nyota ?

Je unakubali kama elimu ya nyota au nyota zina kazi tatu tu ?

Nipo ....
 
Mfano na swali :
Kama nyota ya kaa ni july 21 na 20 au jina Herufi A,
Je akizaliwa 21 july na jina herufi Q atafuata ipi?
Herufi au tarehe?
Siri ya kujua nyota yako thabiti mkuu ni kupata thamani ya hayo mambo manne niliyoeleza kama mifano ninayowafanyia baadhi ya member

Rakims
 
Unaweza kuitoa vipi elimu ya nyota kwa mtindo huu na ushirikina ?

Je Uislamu unaiweka mahala gani elimu hii nyota ?

Je unakubali kama elimu ya nyota au nyota zina kazi tatu tu ?

Nipo ....

Watu kama wewe tumewazoea humu mkuu, pita uende au mwaga upupu wako kisha upite kaanzishe Thread kwenye jukwaa la Dini kule, Halafu kuuliza swali hali ya kuwa unafahamu jibu lake ni ujinga cha msingi weka maelezo hayo unayotaka uyatoe baada ya mimi kukujibu swali hata kama niko sahihi utataka ukosoe, pita pembeni mkuu hakuna haja ya kumjibu mtu mwenye kujifanya kila kitu anajua. Shida yako hapa ulete udini ili watu wenye kusoma uwavuruge waje na wenzio wa makanisani mlete maneno yenu ya kukosoa kila jambo, acha chokono mkuu kuna Jukwaa za dini zinakufaa.

Rakims
 
Mkuu nikiangalia mambo nnayo yapenda hayauwiani na nyota yangu hapo
Jina langu lina anza na J
 
Ng'e na Mapacha vipi hiyo couple
Ng'e na mapacha hapa Ng'e huvutiwa zaidi na Mapacha. nae mapacha huwa anavutiwa sana na upendaji wa kufanya Ngono mara kwa mara kusiko kuwa na kikomo lakini baadae maacha huwa anajitahidi sana kubadilisha mwenendo wa ng'e kwa sababu mapacha huwa ni watu wa kukinai kila kitu mapema sana. Pia mapacha huwa ananguvu sana ya kutafuta maendeleo, wakati Ng'e hujikuta anapenda sana kutawala kipato hicho na kuweka ubinafsi wa kisiri siri. Ng'e hupenda sana maisha ya upweke pweke wakati Mapacha hupenda sana kuongea na kukutana na watu wa kijamii tofauti. wataishi pamoja lakini interest ya Mapacha kwenye mahusiano na mtu mpweke pweke huja kuisha na kuanza kutafuta njia ya kujitoa

Rakims
 
Kwahyo Rakims wewe una weza kusafidha nyota ya mtu ingae?
Alikua hana wateja, sasa wapange folen; hakubaliki akubalike; uongoz uwe fresh, akifuga apate sawasawa, akilima kitu kichipue mana nasikiaga kuna mtu akilima hatapata chcht ila mwingn akilima anapata, yan wanasema fuln ana mkono mzur!!
 
Mkuu nikiangalia mambo nnayo yapenda hayauwiani na nyota yangu hapo
Jina langu lina anza na J
Hapo kuna kuja sasa kwenye uwiano wa nyota iliyokuchomozea wakati unazaliwa na nyota ya mwezi ilikuwa vipi hapo ndio utajua kwa ufasaha sababu ni nini na hii kuna muda mtu husema mbona kama nyota kama tatu naendana nazo,

Rakims
 
... Nimezaliwa 1_4 ila bado siuwiani na tabia hizo
Mfano. Sipendi mambo ya uongozi wala mambo ya kutumia nguvu
 

Hili unalolizungumzia linahusiana na dini na mimi nakuonea huruma juu ya hili,ubatakiwa umuogope Mola wako kwa kuipoteza nafsi yako na kupoteza wenzi wako,najua huwa unatumia hili la haramu kupata ugali,ila nakuhusia wewe na kuihusia nafsi yangu tumche Allah.

Nyinyi mko wengi na mkikumbushwa huwa mnahisi watu wanataka kuwaharibia biashara zenu,ila ukweli uko dhidi yenu na hili ni ovu linatakiwa kukemewa,mwenye kujua ghaibu ni Allah pekee.

Hakuna anae jua kila kitu ila haki lazima isemwe.
 
Ni kweli hiyo ya kulima hutokea pale mtu anakuwa na nyota ya moto anaenda kulima huyu atazeeka analima hana atakalo pata, nyota ya kulima ipo namba 2 thabiti na namba 6 basi wengine watajaribu tu unless wawe kidogo wamechomoza kwenye nyota hizo ndio wataona kidogo vinginevyo 0% ya mafanikio,
na kuhusu kusafisha nyota hivyo ulivyoelekeza ndio na ndio moja kati ya shughuli ninazofanya isipokuwa kuna nyota za watu huwezi kung'arisha kwa maana hawajulikani ili uweze kumsafisha mtu nyota lazima awe na vielelezo vyote hitajika hapo juu.akikosea kidogo tu unatwanga maji kwenye kinu mkuu

Rakims
 
... Nimezaliwa 1_4 ila bado siuwiani na tabia hizo
Mfano. Sipendi mambo ya uongozi wala mambo ya kutumia nguvu
Mkuu hiyo hutokea pale tu ambapo mtu akikinzana na nyota iliyochomoza wakati anazaliwa

Rakims
 

Uko wapi wewe na maneno haya ya mtume ? Utamwambia nini Mola siku ya hukumu au unataka kusema mtume amani ya Allah alifanya hiyana katika kufikisha ujumbe ?

Uko wapi wewe na hadithi hizi ?

Haramisho la kutazamia kwa unajimu ni katika Hadiyth:

Amehadithia ‘Abdullaah bin ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayejichumia tawi katika ujuzi wa unajimu, atakuwa amejichumia tawi katika sihri, na itaendelea kuzidi na kuzidi.” [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

Kusoma elimu hiyo na kuamini ni ushirikina na hivyo dhambi kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimza sana tusiwe ni wenye kwenda kwa wapiga bao, ramli au kutizamia kwa kutumia nyota au mkono kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa amekufuru kwa aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemwendea kahini au mpigaji ramli akamuamini asemayo, basi atakuwa ameshakufuru yale aliyoteremshiwa nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).” [Ahmad, na Aswhaabus-Sunan wanne, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (3047)

Na pia:

((Atakayekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)) [Muslim]


Na Allaah Anajua zaidi
 

Nyinyi ndio mnaofanya uislamu utukanwe na kuonekana dini ya kishirikina.

Hili deni utakuja kulilipa tu.
 
Mimi nimezaliwa siku ya Jumatano tarehe 20 June, nyota ni mapacha na jina linaanza na C, tabia zangu sizielewi, sidumu kwenye kazi, hata kama sitafukuzwa nitaacha, yaani natamani mambo makubwa tu, sina wazo la wastani yaani nawaza makubwa ambayo hayajatimia mpaka leo, shida nini hapo? @Raskims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…