Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani

Hapana asee.....

1: kuna mmoja alitoka mkoa anaomba nimepeleke kutafuta shela, siku hiyo nlikua na buku tu mapema asubuhi nikatoka home tembea sinza yote tangu saa nne asubuhi hadi kumi na moja jioni, njaa balaa nauli nshatumia jero imebaki jero...kumi na moja akatoa 1m akalipa kisha akaniambia kwaheri yani kuzunguka kote asiseme hata tukae tule hata chips kavu 😏😏 nikarudi home na njaa na mchoko nikasema sirudii

2: akaja mwingine nipeleke kariakoo bwana weeeh zunguka mno nipeleke kwenye viatu, kwenye pochi, kwenye vyupi, maduka ya nini sijui kabeba mamfuko hayooo hata kusema basi mwenyeji wangu nae nimchukulie hata kyupi hakunaaa😏😏😏

Nimeshakoma mi siwezi kwenda na mtu shopping tena kanipeleka nisiache kumnunulia chochote haipo....japo sio kwamba ndio inalipa muda wa mtu ila ina maana hata kama ni kitu kidogo. kwahiyo watu wa mikoa kwahilo wasahau pambafff

😂😂
Nikija naomba na Mimi unipelekee Kariakoo
 
Jambo hili lipo hata kwa wafanyakazi..yaani wafanyakazi wa Dar wakija mikoani unawatafutia sehemu ya kulala japo atalipa mwenyewe..utakuwa nae kwenye mizunguko baada ya kazi nk.
Nenda wewe Dar..mtakutana kwenye kikao/mkutano na baada ya hapo kila mtu kivyake vyake.
Hii sasa mnajipendekeza wenyewe.
 
Bwana ni kweli kwanza najua unanilenga mimi shida moja wa mikoani wanakaa Sana mtu anamaliza wiki 3, yupo tu, jamaa ku husu msosi hata sikumoja hajiongezi mimi huwa nawakwepa
Ila ukienda mikoa mingine hasa vijijini mtu anaweza kukuhifadhi kwa mwezi mzima kwa gharama zake. Hapo ndo ujue "Rural life is better than urban life"
 
Hivi mwanaume unapata wapi ujasiri wa kutembelea mkoa fulani na kutaka ufikie/ulale kwa mwanaume mwenzio?
Hebu acheni unafiki kuna thread nyingi humu wengine mnasema hamruhusu hata ndugu zenu wafikie kwemye nyumba zenu kwasababu hamuamini mtu na watoto wenu,leo tena mnalialia mmekataliwa kufikia kwa wanaume wenzenu.
huuu uzi naona kama una viashiria vya kuliwa mtu kimasihara🤔🤔
 
Ila kusema ukweli kwa maisha ya sasa kufikia kwa mtu ni tatizo labda kama wewe ni mwanafunzi,lakini kama una kazi yako na familia yako unafikiaje kwa mtu!?
Huwa tunafikia lodge/hotel na kama kazi muda mrefu kuanzia mwez na kuendelea huwa tunapanga nyumba nzima...

Watu wengi wa Dar wana hako katabia...maana km mnasema mnataka privacy life ya maeneo mnayoishi...sasa mbona ndio huwa mnaongoza kwa kujieleza mkipigaga simu..mara ooh ndugu yangu nimekwama wife hali tyt ana ichi na ichi,mara hali mbaya madogo wako home ada..mara ooh biashara now hali tete ni boost nitakurefund...yaan mnajieleza hata mambo ya sirini ambayo hatupaswi kuyajua...Na tunawaasaidia bila hata kujua mnapoishi....

Yaani kuna mmoja fala kweli kweli yaani nlimwambia mwezi flan nitakuja kuna kazi huko tunakuja kufanya sehemu flani hivyo fanya kutusaidia kupata nyumba safe yenye uzio tutakaa almost miez mitatu hivyo ukipata ya anaetaka sita hamna shida...

Ila huwez amini mwamba alituhakikishia jion kaipata na picha katuma kabsaa daah watu hao na safari ikanza huko me nikiaminiwa kurahisisha kazi na jamaa wa ofisini....Mwamba kufika picha limeanza simu hapokei..piga na piga holla..tuma sms atupe namba ya dalali holaa!!!

Nashukuru Mungu tulienda siku nne kabla ya kuanza kazi..Yaani nlianza saka madalali siku hiyo ili huu msalaba wa ofisi niutue daah....hahahah ila alinipa funzo aisee yaan sasa hivi ninazo namba za madalali wa nyumba kuanzia Mwanza,Arusha na kwa mwamba ndio ninazokibao ....

Nikicheck nlivyokuwaga namsupport mwamba issue kibao tena zile za kifamilia aisee ....Af Kala na jiwe la hiyo kazi niliyompa alafu daah ni mtumishi wa serikali..
 
Back
Top Bottom