Ijue sababu ya marafiki wa DSM kuwakimbia na kuanzisha visingizio pale inapofika mda wa kupokea washkaji zao wa mikoani


😂😂
Nikija naomba na Mimi unipelekee Kariakoo
 
Hii sasa mnajipendekeza wenyewe.
 
Bwana ni kweli kwanza najua unanilenga mimi shida moja wa mikoani wanakaa Sana mtu anamaliza wiki 3, yupo tu, jamaa ku husu msosi hata sikumoja hajiongezi mimi huwa nawakwepa
Ila ukienda mikoa mingine hasa vijijini mtu anaweza kukuhifadhi kwa mwezi mzima kwa gharama zake. Hapo ndo ujue "Rural life is better than urban life"
 
huuu uzi naona kama una viashiria vya kuliwa mtu kimasihara🤔🤔
 
Ila kusema ukweli kwa maisha ya sasa kufikia kwa mtu ni tatizo labda kama wewe ni mwanafunzi,lakini kama una kazi yako na familia yako unafikiaje kwa mtu!?
Huwa tunafikia lodge/hotel na kama kazi muda mrefu kuanzia mwez na kuendelea huwa tunapanga nyumba nzima...

Watu wengi wa Dar wana hako katabia...maana km mnasema mnataka privacy life ya maeneo mnayoishi...sasa mbona ndio huwa mnaongoza kwa kujieleza mkipigaga simu..mara ooh ndugu yangu nimekwama wife hali tyt ana ichi na ichi,mara hali mbaya madogo wako home ada..mara ooh biashara now hali tete ni boost nitakurefund...yaan mnajieleza hata mambo ya sirini ambayo hatupaswi kuyajua...Na tunawaasaidia bila hata kujua mnapoishi....

Yaani kuna mmoja fala kweli kweli yaani nlimwambia mwezi flan nitakuja kuna kazi huko tunakuja kufanya sehemu flani hivyo fanya kutusaidia kupata nyumba safe yenye uzio tutakaa almost miez mitatu hivyo ukipata ya anaetaka sita hamna shida...

Ila huwez amini mwamba alituhakikishia jion kaipata na picha katuma kabsaa daah watu hao na safari ikanza huko me nikiaminiwa kurahisisha kazi na jamaa wa ofisini....Mwamba kufika picha limeanza simu hapokei..piga na piga holla..tuma sms atupe namba ya dalali holaa!!!

Nashukuru Mungu tulienda siku nne kabla ya kuanza kazi..Yaani nlianza saka madalali siku hiyo ili huu msalaba wa ofisi niutue daah....hahahah ila alinipa funzo aisee yaan sasa hivi ninazo namba za madalali wa nyumba kuanzia Mwanza,Arusha na kwa mwamba ndio ninazokibao ....

Nikicheck nlivyokuwaga namsupport mwamba issue kibao tena zile za kifamilia aisee ....Af Kala na jiwe la hiyo kazi niliyompa alafu daah ni mtumishi wa serikali..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…