Ijue Siri: Kwanini Njia ya Kigoma - Dar haina mabasi mengi ya ( luxury )

Ijue Siri: Kwanini Njia ya Kigoma - Dar haina mabasi mengi ya ( luxury )

Acha uongo.
Sumbawanga abiria sio wengi huu mkoa kwa asili watu wake sio watu wa kusafirisafiri .
Kama sijakosea zipo bus kama 4 hivi from Swanga to Dsm daily.
Luxury ipo new force.
 
Biashara ya mabas lazma ujipange Sio yakukurupukia. Kamuulize ZUBERI ndio anajua kilicho mkuta huko.

Hata njia ya mwanza - musoma kuna kijiji kipo katikat hapo kabla ujafika magu ukiwa unatoka musoma, pale bas uwa aitakiwi kusimama ila kama kwenye bas kuna abiria anashukia hapo inabid mkubari kumshushia hapo las hvyo hamtafika mnapoenda yan pale ukigonga ata kuku shuka umtafte mwenye nayo umuombe samahan mbali na hapo utofika unapo enda salama, yan kama upo stend alaf ukamwambia konda unaenda kwenye hcho kijiji unaweza usipate ticket kabsa maana wanapaeshim mno kwa uchawi

Unazungumzia nasa?
 
WAHA MNAPENDA UBISHI SANA, Brother kwani hapa tunabishana au! JIULIZE Kwanini mabasi Ni MACHACHE kigoma! kwanini hakuna luxury bus kigoma! ACHENI TABIA ZENU ZA UBISHI, Kwanza WABUNGE WANAOGOMBEA KIGOMA , ITISHENI KIKAO CHA KIMILA ILI MUWAELIMISHE WASHIRIKINA UMHIMU WA MAENDELEO WA WATU NA VITU IKIWEMO MABASI NA MIUNDOMBINU...ili wasiroge
Kwanza mimi sio Mkigoma nlienda kikazi
Pili barabara ya Manyoni - Itigi - Tabora hadi Kigoma bado kuna vipande kibao bado havihakamilika. (ukianzia Uvinza kuitafuta Kaliua hadi Tabora Vumbi tupu, Nlienda mwaka jana Mei)

Dom - Iringa kulikua na Kingcross inatamba baada ya lami zimekufa saivi zinatamba Coaster
 
Haa😀😁😄😃😅😂
Mtama Wabhonye!!!
Aho Lelo!!!


Kidono, Nyamnyusi
 
Hivi ni kweli uchache wa mabasi unachngiwa na ushirikina au ni muindombinu, umbali na uapatikanaji wa abiria? kwa mfano, Mwanza - Dar , Ar- Dar nahat Ar- Dom kuna abiria wengi sana. jE, Vipi kwa njia ya Dar- Kgm au Dar - Swng?
 
Kayengeyenge, Mvullah, Kidia One, Coastline hayo yote ni mabasi ya Kigoma
 
na kwelii walikuja
OTA yakawashinda
ARIZONA wanapumulia mashine
wajanja ni hao ndugu wawili wa kiarabu Adventure na nduguye Saratoga
 
Ukweli utabakia pale pale.
Nilifungua Saloon ya kiume mwezi wa pili mwaka huu 2020,changamoto ikawa kupata kinyozi.

Japokuwa nilikubaliana na kijana mmoja alifanya kazi wiki moja tu akaondoka kwa kuona hakuna wateja.

Nikafunga ikapita miezi mitatu nimefunga, baadae akaja kijana mmoja kinyozi akaiona Salon akaniambia naomba afanye kazi hapo.

Lakini nilimweleza changamoto ya hapo ya kutopata wateja. Kijana akaniambia usijali bro nakuomba unipatie Elfu 27 tu kuna mtaalam naenda kumuona atapasafisha.

Kweli aisee kijana akaondoka siku ya Alhamisi akarudi juma mosi saa 12 hivi jioni nikamkabidhi funguo akafanya yake.

Wakati anafanya usafi tu wakaja wateja 3 kitu ambacho kilinishangaza sana hyo ndyo ilikuwa hesabu ya kutwa jamaa ameingiza ndani ya nusu saa tu.

Sasa hivi inawiki ya pili ila ni gumzo mtaani na watu wanapanga foleni..

Haya mambo yapo Bwana.
Anasema ana iman! Imani unaweza ukawa nayo lakini je kwenye matendo imo? gari unaimwagia maji ya baraka na maombi lukuki lakini ukikamatwa njiani Unatoa Rushwa ili mzigo ufike, Kama rushwa Ni dhambi Ni Mungu gani atakurindia Mali yako! hapo ndipo Washirikina WANAPITA NA ROLI LAKO HIVI 😵😵😵
Bila capacitor biashara utajisikia tu
 
Hiyo barabara ya lami Tabora kigoma au manyoni Tabora ilikamilika lini? Why mnapenda kuongea vitu msivyovijua? Kigoma AtC inaenda three times a day,huko kwenu kusipo na ushirikina inaenda Mara ngapi kwa siku? Au kwako basi ni Bora kuliko ndege?
 
Njia ya Dar-Sumbawanga Ni miongoni mwa njia chache Sana ambazo ukiomba kibari Cha njia (TLB ) Kutoka SUMATRA hutasumbuka hata kidogo!

Hii inatokana na dhana ya uhaba wa mabasi kwenda maeneo hayo!

Swali hapa je; kwanini Ni machache?
  • wengi wanadhani uhaba wa mabasi unachangiwa na uwepo wa Gari Moshi!
Mwenye Basi jipya akithubutu njia hizo bila kufunga capacitor ajiandae na mapigo Kama;
  1. kwanza kabisa Basi jipya likianza Safari njia hizo hata ukitumia dreva mwenyeji- Ni pigo la kupotea njia ( yaani utaondoka Dar vizuri lakini huko mtauliza Sana njia kwa kupotea potea

Haiwezekani wewe kuwa Mtanzania au umeishi Tanzania!
 
Hata njia ya kusini enzi hizo walisema hivihivi wakina Akidas na wenzake walikuwa wanatawala njia yote Mtwara,Lindi na vijiji vyake. .lakini siku hizi kuna basi za maana..Kigoma kunafunguka taratibu..barabara ikiwa safi vyuma vya maana viataenda!

Kule Sumbawanga pia walisema hayo..lakini New force kaenda na anafanya kazi nzuri wanapelekeshana na saibaba na Majinja..ni nyakati tu mkuu zitapita!
 
Saratoga adventure wakfkaga kakonko huwa wanaongeza speed lakin sjawah kusikia wameanguka,hasa adventure wana madreva wazoefu
 
Tanga kwenda Mbeya basi ni moja tu miaka nenda miaka rudi, na limechoka kweli siku hizi linaitwa Mbeya City zamani No Challenge aka Air Shengena. Linaweza safiri siku 2 kwenda Mbeya. Story ni kama hizohizo za Kigoma, ulozi.
 
Ukweli utabakia pale pale.
Nilifungua Saloon ya kiume mwezi wa pili mwaka huu 2020,changamoto ikawa kupata kinyozi.

Japokuwa nilikubaliana na kijana mmoja alifanya kazi wiki moja tu akaondoka kwa kuona hakuna wateja.

Nikafunga ikapita miezi mitatu nimefunga, baadae akaja kijana mmoja kinyozi akaiona Salon akaniambia naomba afanye kazi hapo.

Lakini nilimweleza changamoto ya hapo ya kutopata wateja. Kijana akaniambia usijali bro nakuomba unipatie Elfu 27 tu kuna mtaalam naenda kumuona atapasafisha.

Kweli aisee kijana akaondoka siku ya Alhamisi akarudi juma mosi saa 12 hivi jioni nikamkabidhi funguo akafanya yake.

Wakati anafanya usafi tu wakaja wateja 3 kitu ambacho kilinishangaza sana hyo ndyo ilikuwa hesabu ya kutwa jamaa ameingiza ndani ya nusu saa tu.

Sasa hivi inawiki ya pili ila ni gumzo mtaani na watu wanapanga foleni..

Haya mambo yapo Bwana.
Waache tu wakubishie, hayajawakuta
 
Thread za ushirikina zimekuwa nyingi mno.....
Watu wanajiongeza kwa kalumanzila au vp
 
Back
Top Bottom