Dar-Kigoma, Dar- Bukoba, Dar- Sumbawanga kama ilivyo Dar- Kigali/Lusaka/Bujumbula na Dar- Kampala ni safari ndefu inayokaribia au kuzidi kilometa 1000, Safari yake siyo ya kitoto hata kwa abiria na ni lazima gari lilale mahali fulani ili kuendelea na safari kesho yake. Safari hii inachosha kwa abiria na madereva na uchakavu wa gari hata kama ni jipya huonekana wazi baada ya kwenda na kurudi!. Hakuna uchawi hapo ila hao kina Saratoga na Adventure ni maveterani wa usafirishaji tangu miaka ya sitini..... wana uzoefu wa kufa mtu hao!.