Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Sasa ni zamu ya Ukanda WA pwani, Mawaziri/naibu Waziri Wengi ni Kutoka Ukanda wa Pwani.
-
 
Tamzania wikipedia
Christians 63.1%
Islams 34.1%
Screenshot_20230302-032830_Chrome.jpg
 
Hizi ni taarifa za malalamiko ya siku nyingi sana, sihitaji kukumbushwa juu yake; nimeshuhudia matokeo ya kazi za taasisi hiyo. Ni malalamishi ambayo hayakuwa na msingi wowote, bali kuwa na madhumuni ya kusukuma ajenda tu.
Kalamu,
Jibu hilo lingetoka serikalini Waislam wangefarajika sana.

Wangefarajika kwa kuwa shutuma zimeelekezwa kwao kwa miaka mingi.

Lakini Serikali wanaliogopa sana hili na ndiyo sababu ilipiga marufuku kitabu cha Hamza Njozi, "Mwembechai Killings..." (2002).
 
Tamzania wikipedia
Christians 63.1%
Islams 34.1%
View attachment 2534301

Ozark,
Nilifanya mhadhara University of Iowa, Iowa City mwaka wa 2011 na nilipewa takwimu za CIA kuhusu ''Tanzania Religious Distribution.''

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Waislam ni ''minority'' Tanzania.
Jibu langu nililotoa mfano wake ni kama huo hapo chini:

"Mtu akikuwekea mbele ya macho yako fimbo iliyopinda na akaitangaza kote kuwa fimbo hiyo imenyooka jibu lake ili lieleweke vyema ni kuweka fimbo iliyonyooka pembeni ya fimbo iliyopinda.

Macho hayadanganyiki.
Clip imeonyesha kuwa Tanganyika ni nchi ya Kikristo.

Zanzibar haina ubishi kuwa ni nchi ya Kiislam lakini ili kunogesha kilichokusudiwa imewekwa picha ya kanisa.

Wamishionari wamefika Tanganyika miaka ya 1800 na kufuatiwa na wakoloni na wamewakuta Waislam na Uislam uko zaidi ya miaka 1000.

Hapa tunacheza na picha na sauti ya fimbo iliyonyooka dhidi ya fimbo iliyopinda.

Mmishionari Johann Krapf kafika Vuga kwa Chief Kimweri mwaka wa 1848 kamkuta anatawala raia Waislam na wanajua kuandika, kusoma na kuhesabu.

Tunaweka picha ya Kimweri kavaa kanzu, juba na kapiga kilemba yuko katika baraza lake anaamua kesi akiandika kwa herufi za Kiarabu.

Krapf kaukuta Uislam Zanzibar na kaukuta Uislam Milima ya Usambaa.

Wajerumani wamefika Kilwa wamewakuta wenyeji wake wote Waislam na kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Waislam wakiongozwa na Hassan Omari Makunganya.

Tunaweka picha ya Msikiti Mkuu wa Kilwa na picha ya Makunganya aliyenyongwa na Wajerumani mwaka wa 1895.

Tunaweka pia picha ya mnara wa kumbukumbu ya Waislam wa Kilwa walionyongwa na Wajerumani kwa kunyanyua silaha kuipigania nchi yao.

Vita vya Abushiri na Wajerumani viliitikisa utawala wa Wajerumani.

Abushiri alinyongwa Pangani mwaka wa 1889.

Abushiri kabla ya kifo chake alifika Kalenga kwa Mtwa Mkwawa na kumsilimisha Mkwawa.

Mkwawa akachagua jina la Abdallah na akamfunza kusoma na kuandika.

Viongozi hawa wawili walikuwa maadui wakubwa wa Wajerumani.

Barua alizoandika Mtwa Mkwawa kwa herufi za Kiarabu zipo Mkwawa Museum, Kalenga.

Leo Manispaa ya Iringa ina misikiti 25 yote inasaliwa Ijumaa na Mkoa mzima una misikiti 80.

Zinawekwa picha ya Mtwa Mkwawa na kizazi chake katika utawala wa Wahehe hadi leo pamoja na picha za misikiti iliyoko Iringa.

Huu ndiyo urithi alioacha Mtwa Mkwawa aliyesilimishwa na Abushiri bin Salim.

Mwaka wa 1905 Vita Vya Maji Maji vikaanza dhidi ya Wajerumani hadi mwaka 1907.

Hapa kuna historia kubwa ya majemadari 67 wa vita hivi walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja la halaiki isipokuwa Nduna Abdulrauf Songea Mbano.

Inawekwa picha yake Nduna Abdulrauf Songea Mbano.

Historia yake inaelezwa kuwa huyu ndiye Songea Mbano ambae waandishi wa historia ya Tanganyika wanakwepa kuandika jina lake la Kiislam "Abdulrauf," kwa hofu ya kuidumisha historia ya Uislam Tanganyika.

Halikadhalika wanakwepa kuandika jina la mwanamke pekee aliyenyongwa na Wajerumani kwa kuwa mmoja kati ya majemadari wa vita ile Bi. Khadija bint Mkomanile.

Waandishi wa historia ya Tanganyika wanamtaja kwa jina moja tu "Mkomanile."

Wanataka kufifilisha historia ya vita hivi na Waislam.

Ikiwa tutakaa kimya bila kujibu clip kama hizi hakika dunia itaamini kuwa Tanzania ni nchi ya Kikristo.

Historia ya uhuru wa Tanganyika iligeuzwa ikawa historia ya Julius Kambarage Nyerere.

Historia ya TANU ikawa historia ya mtu mmoja.

Hili lilifanikiwa kwa kuwa tulikaa kimya lau kama walikuwapo wazalendo wenyewe walioupigania uhuru kwa hali na mali zao.

Sasa tueleze harakati za uhuru wapi zilianzia.
Tunaweka picha ya Dictionary of African Biography (DAB).

Kinawekwa kipande kifupi kinachomweleza Dr. Kwegyir Aggrey (1875 - 1927) kisha ndani ya Kamusi hilo hilo tunatoa na kumwekea mtazamaji wa clip yetu kipande kifupi cha Kleist Abdallah Sykes (1894 - 1949).

Wazalendo hawa waliotajwa ndani ya Kamusi hilo tunaeleza hawamo katika historia rasmi ya Tanganyika.

Mazungumzo kati ya Waafrika hawa wawili Dar-es-Salaam mwaka wa 1924 ndiyo yalisababisha Kleist kuunda African Association mwaka wa 1929 kisha kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.

Vyama vyote hivi viwili vilitawaliwa na Waislam.
Kwa nini ilikuwa hivi?

Swali hili atajibu mtazamaji.

Vyama hivi viwili ndivyo vilivyowasha moto wa utaifa kwa kuunda TANU mwaka wa 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika Waislam wakiwa mstari wa mbele.

Tunaweka picha ya wanawake Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tunaweka picha za masheikh walioongoza kupigania uhuru umoja Watanganyika.

Hawa wakaja na kauli mbiu: "Uhuru na Amani."
Kwa kuhitimisha tutauliza.

Huu wingi wa Wakristo Tanganyika umeanza lini?

Kwa nini madai haya hayakuwapo miaka yote na katika historia ya nchi hii wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika?

Iweje wingi huu uzuke ghafla miaka hii tena bila kufanya sensa na kuweka kipengele cha dini?

Huu Ukristo unaopigiwa chapuo leo nini sababu yake?

Hakuna nchi duniani iliyokombolewa kwa amani au kwa kupigana vita ikawa wapigania uhuru wake ni kutoka jamii ndogo yenye watu wachache.

Halikadhalika hakuna nchi iliyoingia katika kudai uhuru wake ikawa waliokuwa mstari wa mbele kudai uhuru ni watu kutoka jamii iliyokuwa haina uongozi katika wingi wa wananchi ndani ya harakati hizo.

Tafuta dunia nzima hili hutolipata."
Nilipomaliza kujibu ukumbi mzima ulikuwa kimya kabisa.

Mkuu wa African History Northwestern University, Jonathon Glassman alinifata na kuniomba hapo hapo twende chuoni kwake tukafanye mjadala kama huu.

Nilikubali mwaliko na nikazungumza Northwestern University katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

1677731137760.jpeg

Northwestern University, Evanston Chicago​
 
Kuna Taasisi inaratibu hizo chuki .
Ndo maana unaona Dr Slaa sasa taratibu anatoka CCM kurudi Chadema kuongeza nguvu...
Dr Slaa alikuwa katibu zamani wa Taasisi husika...
Umenikumbusha 2005 wakati wa JK....
 
Kalamu,
Hakika dunia ya wazee wetu iliishia Kariakoo kwa Mtaa New Street na Kariakoo walipojenga Ofisi ya African Association kwa kujitolea kati ya 1929 hadi 1933 wakienda pale kujenga wanachama kila Jumapili.

Ilipoundwa TANU 1954 harakati zote zilikuwa Kariakoo kama mahali pa kuishi na Kariakoo Market hapo sokoni ambako Market Master alikuwa Abdul Sykes na akiuza kadi za TANU ofisini kwake.

Kwangu binafsi unaniletea kumbukumbu nyingi unapitaja Kariakoo hata kwa kejeli.

Muhudumu ya Ofisi ya Market Master alikuwa Mzee Abdallah niliyekuja kumfahamu ukubwani sote tukiwa waajiriwa na East African Cargo Handling Services.

Mzee Abdallah kanipa mengi aliyoshuhudia pale wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mwalimu Nyerere hapo Kariakoo ndiko alipofahamiana na watu mashuhuri wa mjini kama Mshume Kiyate na Shariff Abdallah Attas.

Mwalimu alipoacha kazi ya ualimu akenda kuishi Kariakoo nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Kariakoo kwetu ni mahali adhim sana kwani imebeba historia kubwa sana si ya uhuru wa Tanganyika peke yake bali hata historia binafsi ya Mwalimu Nyerere na Mama Maria.

Katika kupambana na maisha ni hapo Kariakoo Mtaa wa Mchikichi na Livingstone Mama Maria alifungua duka dogo la mafuta ya taa.

Kariakoo ni sehemu muhimu katika historia ya taifa letu.

View attachment 2534260
Shariff Abdallah Attas alikuwa na umri huu alipofahamiana na Julius Nyerere sokoni Kariakoo yeye alikuwa mkudanyaji ushuru wa nafaka

View attachment 2534261
Mshume Kiyate akimfariji Mwalimu Nyerere baada ya maasi ya tarehe 20 Januari 1964 yeye alikuwa dalali wa samaki Soko la Kariakoo

View attachment 2534265
Kariakoo Market 1950s
Hiyo hapo kulia nyumba ndogo ndiyo ilikuwa ofisi ya Market Master Mwingereza Brian Hodges na alipotoka Abdul Sykes akachukua nafasi yake​
Story za kwenye kahawa. Story za watu wavivu.
 
Story za kwenye kahawa. Story za watu wavivu.
Kitali,
Yawezekana ni hofu ya kuukubali ukweli au kibri cha mtu asiyetaka kukubali ukweli.
Nakuwekea historia nyingine.

Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Julius Nyerere akiwa Tabora mwaka wa 1955 katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Safari hii alikufatana na Bi. Titi Mohamed na walialikwa na wazalendo wa mjini Tabora mmojawapo akiwa Bilal Rehani Waikela.

Nyaraka za Waikela zilinisaidia kuandika paper, ''Islam and Politics in Tanzania” (1989) Al Haq International (Karachi).

Ikiwa wewe si mvivu unaweza kuisoma paper hiyo hapo chini ambayo inatengeneza ''Part Three": ''Conspiracy Against Islam'' katika kitabu: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, '' Minerva Press, London 1989.

1677730806405.jpeg
292488459_1212904036123639_4246115505430308971_n.jpg

Nyuma waliosimama wa pili ni Bilal Rehani Waikela na Julius Nyerere ni huyo hapo mbele​
 
Tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya teuzi nyingi tu na katika teuzi hizo wapo watu wamekaa standby kuangalia majina ya Kizungu (isomeke Kikristo) na Kiarabu (isomeke Kiislamu) ili waone kuwa watu wanaoendana nao kiimani "wameula" zaidi au la!

Nataka nieleze sababu za hivyo:

1. Mosi, kuna sense of entitlement.
Kwa miaka mingi sana nchini tangu Uhuru mpaka leo hii, nafasi za Utumishi wa Umma na Serikali zimekaliwa zaidi na Wakiristo kuliko Waislamu. Teuzi nyingi kuanzia Nyerere hadi leo hii Rais Samia, teuzi nyingi zinakwenda kwa Wakiristo.

Hali hii imelalamikiwa sana na Waislamu kwa miaka mingi, kuwa, hili jambo lina ukakasi. Iweje teuzi ziende kwa watu wa mrengo mmoja tu kila wakati wakati nchi hii ni yetu sote, na watu wenye vigezo wapo pande zote? Majibu ambayo watu hawa wamekuwa wakipata ni kejeli, kuwa nyie hamjasoma, kuwa nyie mnaendekeza elimu ahera, lakini hoja yao hiyo siku hizi imekuwa proven wrong.

Hata ikafikia hatua hadi Sheikh Khalifa kutoa orodha ya Waislamu wasomi mamia kwa mamia ili kufuta propaganda kuwa waislamu wenye vigezo vya kutosha kuhudumu katika teuzi mbalimbali hawapo, lakini licha ya hivyo hoja hiyo imekuwa ikifumbiwa macho. Sasa leo, Samia licha ya bado kuendelea kuteua Wakiristo wengi zaidi kuliko waislamu lakini angalau kidooogo waislamu nao wanaonekanaonekana kwa mbali.

Hili limeshtua wale waliozoea kuona teuzi za mrengo mmoja, wanahaha, wamepandwa na ghadhabu, wanataka waendelee kuteuliwa watu wa imani yao kwa wingi uleule (over representation) kama zamani.

2. Sababu ya pili ni kuwa, Siyo kweli kuwa baadhi ya hawa wanaolalamikia udini katika teuzi hawajui kuwa Samia bado anateua Wakiristo wengi zaidi kuliko Waislamu.

Bali wanataka kumblackmail ili asije akazoea kuteuateua Waislamu. Wanampa meseji kuwa, ukijaribu kubadili status quo katika nchi hii na kuwapa nafasi watu wa imani nyingine katika Utumishi wa Serikali kwa wingi kama sisi basi tutakusagia kunguni kwa watu wa imani yetu ili upate wakati mgumu kisiasa.

Kwa hiyo hizi kelele kimsingi ni fitina ya kumchonganisha Rais na Wakiristo ili Rais aogope kuwapa Waislamu nafasi na kwa hiyo Status quo ya Wakiristo kuendelea kudominate Utumishi wa Umma na Serikali, uendelee kama ilivyokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo.

3. Sababu ya tatu ni chuki tu, na ufia dini.

Islamophobia is real, kuna watu wanaamini kuwa, kwa kuwabagua watu wa dini nyingine na kuwapendelea watu wa dini yao ni kumfanyia Mungu Ibada!

Wapo watu makazini wakiona kuna wafanyakazi wanavaa hijabu, muda wa swala umefika wanaenda kuswali, au Salamu ya "Assalam Aleikum" imekuwa nyingi katika korido za ofisi wanaanza kuchukia, wanajenga hila mioyoni mwao na kibaya zaidi kuna baadhi wanakwenda mbali hadi ku collude na like minded people ili kuwaletea fitina wenzao n.k.

Enzi hizo wakati nasoma katika chuo kikuu kimoja hapa nchini, wanafunzi Waislamu waliomba chumba kimoja kilicho idle ili wafanye ibada wakazunguushwa mno, wengine wakawa wanapewa vitisho vya siri kuwa wawe makini na ajenda yao hiyo kwamba wachague chuo au dini (yaani ni kitisho cha kupigwa fitina hadi wafukuzwe chuo).

Lakini at the same time, kila siku jioni na siku za Jumamosi na Jumapili madarasa ya chuo hichohicho Wakiristo wameruhusiwa kuyatumia kusali na kuabudu. Umeona aina hii ya chuki, choyo na roho mbaya?

Ushauri wangu:
1. Watanzania tuachane na habari za kutaka upendeleo katika ajira na teuzi. Hii nchi ni yetu sote. Si vizuri kunung'unika watu wa imani nyingine pia wakipata fursa za kuhudumu katika nchi.

2. Lakini kama tunaona upendeleo wa dhahiri katika teuzi, hapo kweli tuseme na tupige kelele. Kuna wakati nchi hii Rais mmoja aliunda Baraza la Mawaziri la watu zaidi ya 20 akaweka Waislamu watatu. Sasa katika situation kama hiyo kweli hapo jamii nzima haipaswi kukaa kimya.

Hivyo hivyo leo hii Samia akiunda Baraza la Mawaziri akaweka Wakiristo watatu tu hata mimi sitokaa kimya. Tusiwe na double standard, kwamba teuzi zikifavour watu wetu tunanyuti, ila wengine wakianza kuchomoza basi tunakuja hapa JF kuanzisha nyuzi lukuki za udini. Hiyo siyo fair.

3. Tuzidi kuimarisha, Umoja, Amani na Mshikamano. Nchi hii Wakiristo are here to stay, Waislamu are here to stay. Yesu hakuoni mfuasi wake bora kwa kuwa mbaguzi na wala Mtume Muhammad hakuoni mfuasi wake bora kwa kuvunja amana za watu wote. Tupendeane mazuri.

Nawasilisha.
bonge la hoja kaka
 
Listen, hata hiki ulichoandika hapa kwangu ni muendelezo wa fikra duni, ujinga; sioni kama taifa tunaweza vipi kupiga hatua kimaendeleo ikiwa bado tutakuwa tunatazamana kwa jicho la dini, kabila, au rangi.

Wewe umekuja hapa kuwatetea wale wa dini yako, simply umekuja kuongeza tatizo, hukumbuki wapo wasio na dini, wakina Kiranga na wenzake wao wamenyamaza kimya, hawana msemaji wao, na wala hawana hivi viherehere mlivyonavyo wengine.

We need to stop this kind of ignorance, kwasababu kutaka watu wa dini yako wawepo kwenye mamlaka hakutakusaidia chochote kama hutakuwa na mahusiano nao ya moja kwa moja, zaidi, kinachowafanya wengi wazungumzie hii issue ni kama ulevi tu, tena usio na tija kwao, wala kwa taifa.

Huu upuuzi una extend mpaka pale anapokuwepo kiongozi fulani, halafu wale wa dini yake wanakuwa hawaoni baya lolote toka kwake, huu nao ni ujinga mwingine mkubwa zaidi, kusifia/tetea kila linalofanywa na yule wa dini yako upuuzi.
ama hakika mpuuzi ni wewe ambaye uzi huu umeutazama kwa macho ya makengeza
 
Go back and revisit your home work. Go back to your drawing board. Wakristo kuwa wengi kwenye nafasi za uteuzi ndani ya Utumishi wa Umma kuliko Waislamu ni de facto inayoanzia kwenye utoafauti wa idadi hizo ndani ya Utumishi wa Umma wenyewe usiokuwa wa uteuzi. Huko huko kwenye MDAs and LGAs waislamu ni wachache(sababu zinaweza kuwa mada nyingine tofauti).

Kwa hiyo katika scaling up, huwezi kuwapata waislamu wengi kuliko wakristo kutokana na sababu hiyo kuu.

Pili, wapagani wengi Tanzania ni de facto wakristo. Yaani sehemu kubwa, kama wazazi ni wapagani hasa bara, mtoto akisoma kidogo, unamkuta ana jina la kikristo(Roman Empire Names).
de facto???au de jure unayoijengea de facto?
 
Tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya teuzi nyingi tu na katika teuzi hizo wapo watu wamekaa standby kuangalia majina ya Kizungu (isomeke Kikristo) na Kiarabu (isomeke Kiislamu) ili waone kuwa watu wanaoendana nao kiimani "wameula" zaidi au la!

Nataka nieleze sababu za hivyo:

1. Mosi, kuna sense of entitlement.
Kwa miaka mingi sana nchini tangu Uhuru mpaka leo hii, nafasi za Utumishi wa Umma na Serikali zimekaliwa zaidi na Wakiristo kuliko Waislamu. Teuzi nyingi kuanzia Nyerere hadi leo hii Rais Samia, teuzi nyingi zinakwenda kwa Wakiristo.

Hali hii imelalamikiwa sana na Waislamu kwa miaka mingi, kuwa, hili jambo lina ukakasi. Iweje teuzi ziende kwa watu wa mrengo mmoja tu kila wakati wakati nchi hii ni yetu sote, na watu wenye vigezo wapo pande zote? Majibu ambayo watu hawa wamekuwa wakipata ni kejeli, kuwa nyie hamjasoma, kuwa nyie mnaendekeza elimu ahera, lakini hoja yao hiyo siku hizi imekuwa proven wrong.

Hata ikafikia hatua hadi Sheikh Khalifa kutoa orodha ya Waislamu wasomi mamia kwa mamia ili kufuta propaganda kuwa waislamu wenye vigezo vya kutosha kuhudumu katika teuzi mbalimbali hawapo, lakini licha ya hivyo hoja hiyo imekuwa ikifumbiwa macho. Sasa leo, Samia licha ya bado kuendelea kuteua Wakiristo wengi zaidi kuliko waislamu lakini angalau kidooogo waislamu nao wanaonekanaonekana kwa mbali.

Hili limeshtua wale waliozoea kuona teuzi za mrengo mmoja, wanahaha, wamepandwa na ghadhabu, wanataka waendelee kuteuliwa watu wa imani yao kwa wingi uleule (over representation) kama zamani.

2. Sababu ya pili ni kuwa, Siyo kweli kuwa baadhi ya hawa wanaolalamikia udini katika teuzi hawajui kuwa Samia bado anateua Wakiristo wengi zaidi kuliko Waislamu.

Bali wanataka kumblackmail ili asije akazoea kuteuateua Waislamu. Wanampa meseji kuwa, ukijaribu kubadili status quo katika nchi hii na kuwapa nafasi watu wa imani nyingine katika Utumishi wa Serikali kwa wingi kama sisi basi tutakusagia kunguni kwa watu wa imani yetu ili upate wakati mgumu kisiasa.

Kwa hiyo hizi kelele kimsingi ni fitina ya kumchonganisha Rais na Wakiristo ili Rais aogope kuwapa Waislamu nafasi na kwa hiyo Status quo ya Wakiristo kuendelea kudominate Utumishi wa Umma na Serikali, uendelee kama ilivyokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo.

3. Sababu ya tatu ni chuki tu, na ufia dini.

Islamophobia is real, kuna watu wanaamini kuwa, kwa kuwabagua watu wa dini nyingine na kuwapendelea watu wa dini yao ni kumfanyia Mungu Ibada!

Wapo watu makazini wakiona kuna wafanyakazi wanavaa hijabu, muda wa swala umefika wanaenda kuswali, au Salamu ya "Assalam Aleikum" imekuwa nyingi katika korido za ofisi wanaanza kuchukia, wanajenga hila mioyoni mwao na kibaya zaidi kuna baadhi wanakwenda mbali hadi ku collude na like minded people ili kuwaletea fitina wenzao n.k.

Enzi hizo wakati nasoma katika chuo kikuu kimoja hapa nchini, wanafunzi Waislamu waliomba chumba kimoja kilicho idle ili wafanye ibada wakazunguushwa mno, wengine wakawa wanapewa vitisho vya siri kuwa wawe makini na ajenda yao hiyo kwamba wachague chuo au dini (yaani ni kitisho cha kupigwa fitina hadi wafukuzwe chuo).

Lakini at the same time, kila siku jioni na siku za Jumamosi na Jumapili madarasa ya chuo hichohicho Wakiristo wameruhusiwa kuyatumia kusali na kuabudu. Umeona aina hii ya chuki, choyo na roho mbaya?

Ushauri wangu:
1. Watanzania tuachane na habari za kutaka upendeleo katika ajira na teuzi. Hii nchi ni yetu sote. Si vizuri kunung'unika watu wa imani nyingine pia wakipata fursa za kuhudumu katika nchi.

2. Lakini kama tunaona upendeleo wa dhahiri katika teuzi, hapo kweli tuseme na tupige kelele. Kuna wakati nchi hii Rais mmoja aliunda Baraza la Mawaziri la watu zaidi ya 20 akaweka Waislamu watatu. Sasa katika situation kama hiyo kweli hapo jamii nzima haipaswi kukaa kimya.

Hivyo hivyo leo hii Samia akiunda Baraza la Mawaziri akaweka Wakiristo watatu tu hata mimi sitokaa kimya. Tusiwe na double standard, kwamba teuzi zikifavour watu wetu tunanyuti, ila wengine wakianza kuchomoza basi tunakuja hapa JF kuanzisha nyuzi lukuki za udini. Hiyo siyo fair.

3. Tuzidi kuimarisha, Umoja, Amani na Mshikamano. Nchi hii Wakiristo are here to stay, Waislamu are here to stay. Yesu hakuoni mfuasi wake bora kwa kuwa mbaguzi na wala Mtume Muhammad hakuoni mfuasi wake bora kwa kuvunja amana za watu wote. Tupendeane mazuri.

Nawasilisha.

Yani mimi nikimuona mtu anazungumzia siasa na dini kwa wakati mmoja anakuwa ananivuruga sana
Nakuwa simuelewi kabisa
 
Dawa ni kukavunja haka ka muungano na kila mtu arudi kwao basi!

Wazanzibar mnakuja kuchuma huku mkituharibia Tanganyika yetu kwa kuinadi na kuiuza kwa warabu wenu.

Haya mengine waambie wapuuzi wenzenu!

Neno!
 
Mkuu, naona watu mnaingia kwenye mtego uleule ulionuiwa uwanase.
Inaonyesha dhahiri Samia na genge lake wanatafuta kuamsha hisia kama hizi zinazowaingia kichwani na kujisahau kabisa kwamba kuna ajenda inatekelezwa.

Kupambana na ajenda hiyo inalazimu utambue kwa nini inaletwa kwanza na utafute njia sahihi za kutoongeza petroli kwenye tatizo husika.

Hii ni Tanzania ya waTanzania, siyo ya kundi maalum. Tuaanzia hapo.
Upo sahihi mkuu, koo zilezile na dini ile ile
 
Back
Top Bottom