Mimi nimekupa facts za kiimani na sio hisia za kiimani. Ukombozi wa wakristo uko kwa kufa kwa Yesu kristo. Kwanini? Yesu hakustahili kufa, lakini kwa sababu ya dhambi zetu ilimpasa kufa yeye ili sisi tupone. Huo ndio ushindi wa imani ya kikristo. Hakukuwa na mtu mwingine ambaye angeweza kulipa hiyo gharama lakini Yesu akailipa kwa gharama ya kifo chake pale msalabani. Kwanini tusifurahi kwa hilo?
Kufufuka kwa Yesu ni chapter ingine kabisa katika imani ya Kikristo, kufufuka kwake ni udhihirisho wa kuwa kufa kwake kulifanikiwa kulipa deni letu la dhambi msalabani kikamilifu na akashuka kuzimu kumnyang'anya shetani mamlaka yote. Ufufuo wa Yesu haifuti dhambi zetu bali unatupa mamlaka ya kumshinda shetani kwenye nyanza zote.