Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

Uzwazwa huu kabisa. Hujielewi au unapotosha makusudi. Unaposema "Yesu alikufa Siku ya kwanza ya Juma" umetumia Biblia gani potoshi?

Yesu Kristo alikufa siku ya maandalio ya Sabato yaani Ijumaa jioni. Rejea Luka 23:53-54

"53 Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake.

54 Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia."

Siku ya kwanza ya juma ndiyo siku Bwana Yesu alipofufuka. Rejea Luka 24:1-3

"1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.

2 Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,

3 Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.

Acha kupotosha.
 
Ndugu Mitale, wakristo walio wengi wanaabudu Siku ya Kwanza a.k.a Jumapili kwa sababu hizi (baadhi).
  1. Yesu Kristo alifufuka Siku ya Kwanza ya Juma (Mt.28:1). Ufufuko wa Yesu ndio wokovu wenyewe; labda kama huamini katika wokovu.

M
Ubarikiwe kwa mchango mzuri.

Helen alikuwa anasali Jumapili (Mathodist) akaikumbuka sabato hakuwahi kuileta aliikuta.
Na Yeye ni MTU tu hawezi kutoa agizo kwenye agizo ambalo tayari Mungu ameshalitoa kama ambavyo tunaona kwa wenzetu.
Huu ni uhaini dhidi ya serikali ya Mungu wanayemuabudu.

Sababu zako nimezipitia hazijatoa ushahidi kuwa Kufufuka kwa Yesu ni mbadala wa SABATO.

Kwa kweli na Shahidi zifuatazo.

1: Sababu hii ni ya kimsisimko. Kufufuka kwa Yesu sio mbadala wa Kuikumbuka Sabato. Hizo ni hekima za wazee wa dini baada ya mitume. Usisahau wazee na hekima zao ndio waliwahi kushawishi waisraeli waabudu ndama na waseme ndiyr kawatoa misri. Kuwa makini na hrkima za wazee.
Sabato in a package zote za msalabani.

-Yesu aliyeumba mwanadamu nfiye kawaokoa msalabani.

- Tukio LA wokovu ni tukio LA kiuumbaji, na sabato ni sherehe ya uumbaji. Unasherekea kuwa licha ya dhambi Yesu amekuumba tena upya kwa damu yake.
Tazama MTU akiwa ndani ya Yesu amekuwa kuimbe kipya.

Hivyo huwezi kuitenganisha Sabato, Uumbaji, Wokovu msalabani.

2: Fungi LA kuchangishana michango Siku ya Jumapili halina uhusiano na ibada ya Sabato na agizo lake. Kukutana ili mchange sio mbadala wa sabato.

3: Kanisa halijaanzia Pentekoste. Huu ni mtazamo potofu. Kanisa kwa uelewa wa mcha Mungu lipo zote
Acts 7:38
[38]This is he, that was in the church in the wilderness with the angel which spake to him in the mount Sina, and with our fathers: who received the lively oracles to give unto us:
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.

Sababu ya pentekoste ni ya kihisia na msisimko zaidi sio mabadiliko. Kwanza Pentekoste walisali Siku kumi had I kufikia hapo. Hivyo Pentekoste haina uhusiano na Jumapili wala Jumamosi wala sabato.

*MSTARI UNAOONYESHA MITUME WALISALI VIPI BILA KONA, MSTARI ULIONYOOKA. TENA IBADA ILIHUSISHA WAMATAIFA KAMA WEWE NA WAFUASI WA YESU ILIFANYIKA SIKU YA SABATO.



ENDO YA MITUME 16 : 12 - 13.


12Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.

13Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali.*Tuliketi, tukaongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo.

*WAFUASI WA KRISTO KWENYE BIBLIA WALISALI SIKU YA SABATO


UBARIKIWE, UKIELEWA. UNATEKELEZA. DUNIA HAITAKI KUMWAMINI MUNGU UKIWA NA HOJA NYEPESI KAMA HIZO. SHETANI ATAKUNASA SIMPLE TU.
 
Nilikosea sikuhariri andiko language na sasa nimerekebisha.

Nashukuru kupitia makosa yaho umetoa kitu moyoni.

UBARIKIWE sana na Bwana wa Sabato.
 
Sasa mzee hapo si walikuwa hawajui km Yesu atafufuka!!!,Lkn baada ya kujua kuwa Yesu alifufuka siku ya Jumapili,Mitume walianza kukutanika kwaajili ya Ibada siku ya Jumapili km ilivyo Leo rejea 1Kor.16:1-2.
Mkuu kuweka AKIBA kwa ajili ya maskini waliokuwa YERUSALEMU ndilo kusanyiko la IBAADA?

Wapi wamekusanyika nani kasema? Mungu ndiye anayena hapo au ni ushauri kutoka kwa PAULO MTUME?

Paulo ana mamlaka ya kutangua amri ya MUNGU?

IKIWA ALIKUWA ANAMAANISHA HIVYO, KWANINI YEYE HAFANYI IBAADA JUMAPILI, BADALA YAKE ALIKUWA ANASALI JUMAMOSI NA JUMAPILI ANAITUMIA KAMA SIKU YA KUSAFIRI?.

HEBU SOMA MAFUNGU HAYA KWA MAKINI.



MATENDO 13 :13,14,42, 44.

13Kutoka Pafo, Paulo na wenzake walipanda meli wakaenda hadi Perga katika Pamfulia; lakini Yohane aliwaacha, akarudi Yerusalemu.

14Lakini wao waliendelea na safari toka Perga hadi mjini Antiokia Pisidia. Siku ya Sabato waliingia ndani ya sunagogi, wakakaa.

42Paulo na Barnaba walipokuwa wanatoka katika lile sunagogi, wale watu waliwaalika waje tena siku ya Sabato iliyofuata, waongee zaidi juu ya mambo hayo

44Siku ya Sabato iliyofuata, karibu kila mtu katika ule mji alikuja kusikiliza neno la Bwana.


MATENDO 16 : 13

13Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali


MATENDO 17 : 2 ( Desturi ya Paulo)

2Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake, akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akitumia Maandiko Matakatifu.

MATENDO 18 :3, 4

Kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi
. 4Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.

PAULO ANATUMIA SIKU YA JUMAPILI KUSAFIRI.

MATENDO 20 :7

7Jumamosi jioni tulikutana ili kumega mkate. Kwa vile Paulo alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake

MIMI NIMETOA USHAHIDI KWA MAANDIKO ZAIDI YA SABA KWAMBA PAULO NA MITUME WALIKUWA WAKIFANYA IBAADA SIKU JUMAMOSI.

NAKUOMBA ANDIKO MOJA TU KWAMBA PAULO,AU MTUME YEYOTE,AU NABII YEYOTE AU YESU KUWA AMEWAHI KUSALI JUMAPILI.

WASALAAM.
 
Hatujakataa tunajua vizuri jumapili ni siku ya kwanza ya juma msifikiri hatujui.
Sabato vs Jpili/Ijumaa

Ni
Kauli/Agizo/Amrisho LA Mungu VS Mapokeo ya wazee wa kikristo baada ya mitume kufa.

Kila MTU anapoamua kuwa mfuasi wa Mungu ataacha mapokeo na kufuata kauli za Mungu.
 
Sabato sio dini. Sabato ni agizo LA mfalme Mungu wa milele.

Ukielewa ninachokufundisha nakusihi sana fuata.

Kitu ambacho shetani hatakudokeza ni kwamba Siku ya hukumu utasimama peke yako.

She he
Mchungaji
Padri
Papa
Kasisi
Mitume
Nabii
Shemasi
Mwinji

Watakukana.
Utabaki wewe na kauli za Mungu au Mapokeo.
 
Mimi nashauri tuombe vita ya kirafiki na hao watu
 
... kwa hiyo Mitume waliokusanyika siku ya kwanza; waliomega mkate siku ya kwanza; waliopumzika siku ya kwanza; Roho Mtakatifu aliyeshuka siku ya kwanza wote hao hawakujua kwamba Sabato ni siku ya saba na kwamba ndio siku sahihi ya kupumzika hadi alipokuja Bi Ellen "kutufumbua macho"?
 
Lkn Jumapili Alfajiri ndipo Yesu alifufuka ndio siku ya Ushindi, Hivyo lazima tumwabudu MUNGU siku hiyo Jumapili na sio jumamosi.
Naona kama mleta mada amechanganya mambo, suala la Sabato linahusiana na uumbaji hili la kuhusisha Pasaka na sabato sielewi vizuri
 
Mimi nashauri tuombe vita ya kirafiki na hao watu
Yesu ni mfalme wa amani.

Maombi ya vita na mauaji wanaomba wachawi, na WAFUASI wa adui.

Sisi tunaomba Giza LA ufahamu liwatoke watu waone uzuri wa Maagizo ya Mfalme wa amani.

WAFUASI wa Bwana wa Sabato sio watu wa vita ni watu wa amani.
 
Asante sana. Mtume Mohammad SAW alikuwa muungwana sana kwenye hili.

Wafuasi tu ndio wanahitaji neema ya kuwa wepesi kuelewa Sabato ya Bwana Mungu wao.
Mtume Muhammad alikuwa muungwana mno,ndio maana nashawishika kuamini pia QURAN ni kitabu kilichobaki chenye original scriptures,maana IKIWA MANENO hayo yamebaki ndani yake kwa karne kadhaa bila kuondolewa,habari gani ingekuwa inatajwa kuwa MUHAMMAD ni mtume wa Mungu ndani ya BIBLIA,nakuhakikishia kwa akili hizi za WAKRISTO HAKIKA TUNGEFUTA.
 
Naona kama mleta mada amechanganya mambo, suala la Sabato linahusiana na uumbaji hili la kuhusisha Pasaka na sabato sielewi vizuri
Tazama MTU akiwa ndani ya Yesu amekuwa kiumbe kipya.

Sabato, Uumbaji na Ukombozi havitenganishiki.

Ndio Maana Alikufa ijumaa kuelekea sabato.

Alikomboa alichokiumba. Hakuna ukombozi kama hakuna kiumbe cha kukomboa.


Ni sayansi inayohitaji utulivu wa kiroho
 
Naafikiana nawe, maana kuna mvurugiko mwingi katikati hapa kutoka uyahudi kwenda ukristo na uislam, kutoka ukristo wa kikatoliki kwenda uprotestant, kutoka uprotestant kwenda usabato, kutoka usabato kugawika sabato 1 na 2 masalia
 
Kwa maagizo ya nani?au kwa maandishi gani ndani ya biblia yaliyoruhusu hilo.

Wakristo tumejitoa akili sana.

#MaendeleoHayanaChama
Inasitaajabisha mno,hadi baada ya miaka 300 baada ya UFUFUKO WA YESU hakuna MKRISTO yeyote aliyewahi kukanyaga KANISANI SIKU YA JUMAPILI.

IKIWA KWA KINYWA CHA YESU MWENYEWE ANAWAAMBIA

"WATU WANGU SABATO ILIFANYIKA KWA AJILI YA WANADAMU" - MARKO 2 : 21.

WAO WANASEMA HAPANA,SABATO NI KWA AJILI YA WAYAHUDI ILA JUMAPILI KWA AJILI YA WAKRISTO,UKIWAULIZA ANDIKO HAWANA HATA MOJA,WAULIZE HAYO MMEYATOA WAPI,HAWAJUI.
UKIIONA RAIA HUMU INAPINGA JUU SABATO

UKIONA DALILI HIZO TAMBUA TU HUONGEI NA BINADAMU UNAONGEA NA NYANI. (KWA MUJIBU WA QURAN).




QURAN AL A'RAAF 7 : 163 - 166.

163. Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja amri ya Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika (Sabato) hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.

164. Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu.

165. Basi walipo yasahau waliyo kumbushwa, tuliwaokoa walio kuwa wakikataza maovu, na tukawatesa walio dhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyo kuwa wakifanya upotovu.

166. Walipo jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni manyani wa kudharauliwa
 
Hakuna Original manuscript za Quran mkuu. Caliph Uthman alichoma vyote kwa Mujibu wa Sahih Bukhar.

Hivyo tubaki na chanzo cha biblia tu. Kama kuna kingine kinapatikana popote nje ya biblia tutachukua kinachoungana na biblia mengine tunawaachia.

Mfano Paulo akiwa Athene aliquote kauli za mwanaphilosofia na mtunga mashairi kusisitiza kilichomo kwenye Biblia sio kulinganisha na kuyapa hadhi sasa na maandiko matakatifu.
 
Kumbe mikuki inarushwa kuelekea siku ya sita na ya kwanza
 
Ili iweje?
Kila kitu alichofanya kilikuwa kimetabiriwa.
Yesu alikufa hii tunayoiita weekend Leo ili kutukumbusha kuwa Yesu Aliyekufa ndiye aliyeumba dunia Siku sita NA Ya sabato Jumamosi ya Sabato Akafufuka.

Sio MTU no Mungu muumbaji.
Hivyo aliongeza kina cha sabato kuwa Unapokumbuka Mauti ya ya Yesu ninili tuumbwe upya. Yesu jumapili hakwenda kwenye makanisa kukutana na wafuasi waliomuelewa. Aliwavizia njiani wakiwa wanaenda mashambani. Maana mambo ya ibada yaliisha Jumamosi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…