Ijuwe tofauti ya kundi ukombozi vs kundi maslahi vs kundi chawa katika siasa za kidemokrasia Africa.

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kuna aina tatu za Viongozi wa kisiasa Barani Afrika, ikiwemo Tanzania.
1. #KUNDI_UKOMBOZI: Aina ya kwanza ni viongozi watetezi wa nchi, ambapo kwenye kundi hili ndipo utawakuta watetezi wa rasilimali za kiuchumi za nchi, utawakuta watetezi wa utawala wa demokrasia, utawakuta watetezi wa haki na usawa, utawakuta watetezi wa utawala wa sheria, utawakuta wanaharakati watetezi dhidi ya ukatili wa kijinsia, na utawakuta watetezi wa maendeleo wanaoguswa na shida, kero na matatizo ya wananchi.

Mara nyingi viongozi wenye kariba ya kundi hili, ni watu walionyooka, ni watu wasiokuwa na ndimi mbili kwa jambo moja, ni watu wasio kigeugeu. Kwao nyeusi ni nyeusi, na nyeupe ni nyeupe. Ni nadra kusikia kwamba, viongozi wa kundi hili wamehongwa, wamefika bei au kununulika na upande mwingine wa kisiasa. Ni aina ya viongozi ambao wako tayari kuyatoa maisha yao sadaka kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya nchi, pia kwa kile wanachokiamini.

Ni watu wanaochukia rushwa, ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya madaraka. Ni wafia Haki, Ukweli, na Uwazi. Ni viongozi ambao hutanguliza mbele maslahi ya taifa kuliko maslahi yao binafsi. Ni wapinga dhuluma, unyanyasaji, pamoja na ukandamizaji. Ni viongozi wanaopenda kuona matokeo chanya juu ya kile wanachokifanya, ikiwemo ustawi wa jamii wanayoiongoza. Kipaumbele cha viongozi wa kundi hili si cheo chao kwanza, wala maslahi yao kwanza, bali jamii kwanza, na nchi kwanza.

Kwenye kundi hili ndipo utawakuta watu kama hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, hayati Nelson Mandela, hayati Edward Moringe Sokoine, hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Tundu Antipas Mughwai Lissu, Luhaga Joelson Mpina, kwq kuwataja wachache...Unachopaswa kujua ni kwamba, aina hii ya viongozi wanaopatikana kwenye kundi hili si wengi kwa sababu Mungu huwaumba wachache, na hata hao wachache waliopo hupigwa vita kikweli kweli na makundi mengine wasipate nafasi za maamuzi kwenye Serikali.

2. #KUNDI_MASLAHI: Aina ya pili ya kundi la viongozi wa kisiasa, ni kundi maslahi kwanza, nchi na wananchi baadaye. Inaaminika kwamba, kundi hili ndilo kubwa kuliko makundi mengine yote. Ni kundi lenye nguvu kiuchumi kwa maana ya kumiliki ukwasi wa pesa. Ni kundi linaloamua kuhusu hatima ya nchi kwa kila kitu, kuanzia kiuchumi, kiutawala ikiwemo kupanga nafasi za uongozi, nani awe wapi na nani ashike wapi. Hili ndilo kundi linalomiliki rasilimali za kiuchumi za nchi kupitia mikataba ya kifisadi.

Ni kundi ambalo dhuluma, unyanyasaji na ukandamizaji ndiyo uti wa mgongo wa kundi hili. Kwenye kundi hili utawakuta aina ya viongozi wanaotetea dhuluma, wanaotetea ubadhirifu na wizi wa fedha za umma, wanaotetea rushwa na ufisadi. Aina hii ya viongozi wanaopatikana kwenye kundi hili utawakuta hata kwenye vyama pinzani, ambapo kipaumbele chao ni cheo kwanza ili wanufaike kwa pamoja na walioko kundi maslahi tawala, lakini wananchi baadaye.

Hili ni kundi ambalo katika mazingira fulani hutumia nguvu yake ya kiuchumi kuwanunua baadhi ya wanasiasa machachari walioko kundi ukombozi. Ukiona miongoni mwa viongozi wa kundi ukombozi wanazungumza kauli zinazofurahisha kundi madlahi, tambua tayari mvua imewanyeshea. Hali hiyo ilitumika kuisambaratisha NCCR Mageuzi, TLP, pamoja na CUF. Sasa ni zamu ya Chadema, ambapo, ninaamini, kundi ukombozi litavuka salama.

Kwao, swala la kudai na kupigania haki na usawa kwenye mifumo kandamizi ya kisiasa na kidemokrasia, ikiwemo ya uchaguzi , si hoja ya msingi, bali cha msingi kwao ni maslahi yao binafsi kwanza. Rejea kundi la Chadema linalojiita G.55 ambalo linadai uchaguzi uendelee katika mazingira yaliyopo bila kujali wanatambua kwamba mazingira si wezeshi kupatikana kwa haki. Hawa ndiyo viongozi maslahi ambao Watanzania tunapaswa kuwatambua popote watapogombea au kutia nia, wapigwe chini. Ni viongozi wenye tamaa na uchu wa madaraka kuliko maslahi mapana ya nchi ya wananchi wake.

Ni kundi ambalo lina mtandao mpana, kuanzia kwenye Chama tawala, Serikali, pamoja na taasisi zake, na wakati mwingine kutokana na nguvu ya ushawishi wake, lina uwezo hata wa kusababisha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pinzani kuacha mwelekeo wa sera na dira ya vyama vyao na kuwa mateka wa kundi hili kisiasa, ambapo na wao huanza kucheza ngoma kulingana na mdundo wa kundi hili unavyolia.

Kundi hili maslahi lina silaha nyingi za kuhakikisha maslahi yake hayakorofishwi, na miongoni mwa silaha hizo ni pamoja na kufanya mambo yake kwa usiri mkubwa. Silaha nyingine ni kuteka nguvu ya vyombo vya habari ili kuhakikisha habari zake chafu zinachujwa zisiwafikie wananchi. Silaha nyingine ni kutumia vyombo vya habari kufanya propaganda kwa mambo mazuri pekee, na inapotokea ukosoaji wa kulivua nguo kundi hili, silaha ya mwisho ni nguvu ya vyombo vya dola kutumika. Ni kundi ambalo liko tayari kufanya chochote ilimradi maslahi yake yasitikiswe.

3. #KUNDI_CHAWA: Aina ya tatu ya viongozi wa kisiasa ni wale wanaojiita Chawa. Aina ya viongozi walioko kwenye kundi hili, ni wale wanaocheza ngoma kulingana na mdundo unavyolia kwa wakati huo, pamoja na upepo unavyovuma. Hawa, huwa hawana kanuni maalum wala si wa kudumu. Ni kundi ambalo humshabikia aliyepo madarakani kwa wakati huo ilimradi mkono wao uwende kinywani, na pindi upepo unapobadilika, na wao hubadili gia angani mara moja.

Hili ni kundi ambalo kiongozi aliyeko kwenye kundi hili, akipewa nafasi ya kuzungumza mahali popote, kabla hajasema chochote, huanza na sifa za yule anayemfanyia uchawa. Lengo la kufanya hivyo ni kupalilia kitumbua chake, au kufikiriwa kupewa nafasi iwapo bado hajaingia kwenye mfumo.

Kundi linalojiita G.55 la Chadema linalodai kufanyika kwa uchaguzi licha ya kasoro kubwa zilizopo, ni kundi linaloonyesha kwamba liko upinzani lakini viongozi wana mafungamano na kundi maslahi la Serikali.

Nataka kuwaambia Watanzania kwamba, kupitia kundi hili sasa ndo tuanze kuchuja kati ya mchele ni upi na chuya ni zipi. Kanuni ya ukombozi wa nchi huwa haianzi na watu wengi, bali huanza na watu wachache. Tulio nyuma ya kundi la ukombozi tuendelee kupaza sauti ya kutaka mabadiliko, na lile kundi linalojiita G.55 ambalo kimwili linaonekana kuwa Chadema, kumbe kiroho liko ni wafuasi wa kundi maslahi, waondoke waende kule wanakoshabihiana.

Credit: Mkweru Zakaria Maswale FB
1744075929434.jpg
1744075923272.jpg
 
At least tunaanza kuongea lugha moja sasa

History tends to repeat itself
Firsr Liberation ↔️ Second Liberation

Tusihofu Ukombozi wa Pili umeshaanza ni juu yetu sasa - we have the leader, now we the People need to rise to the occassion!
#ChangeTanzania
#NoReformsNoElection
#TutaelewanaTu
1744077877805.jpg
 
"Shida sio kwamba watu wetu wanaenda kuumizwa, shida ni kwamba twende ili tupate ruzuku, hiyo ruzuku inafika Masas? Na hayo maisha ya watu? Maisha ya watu kumbe ni ruzuku kwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi?

Nilidhani kwenye uchaguzi ni kwenda kutafuta viongozi! Kumbe kuna watu wanawaza pesa, hawajali watu kufa (kwenye uchaguzi), ndiyo hivyo? Hakuna mabadilko, hakuna uchaguzi" @TunduALissu

Masasi, Mtwara, leo, Aprili 07, 2025
#NoRefomsNoElection #NIMO
1744078880752.jpg
 
Kwenye kundi hili ndipo utawakuta watu kama hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, hayati Nelson Mandela, hayati Edward Moringe Sokoine, hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Tundu Antipas Mughwai Lissu, Luhaga Joelson Mpina, kwq kuwataja wachache
 
Mwaka 2015 ilifika hatua vijana walifosi wapate Vote I'd ili tu waipigie kura Chadema.

Na kweli walifanikiwa .
Kumbe nguvu zote zile kuna watu walikuwa wanatumika .

Japokuwa Mbowe Amefanya mambo makubwa Ila Taifa halitoweza kumkubuka Kama kiongozi wa Mfano.

Just imagine , watu wameuliwa , wamefungwa na wengine kupotezwa Ila bado kuna hao wanachadema wanadai mambo mawili tu ruzuku na chadema kuwa chama kikuu cha upinzani.

Mbowe katikati ya VITA Kali na shetani anashindwa kutia neno lolote hii Ina maanisha nini .

Tuupe muda nafasi .

Tumuombee Sana Lissu na zipo sababu kwanini hakufa maana angekufa tusingeyajua haya yote
 
Uhai wa lissu si bure, kuna sababu. kama sio kuchange siasa za nchi basi ni kuleta revolution mpya chadema na kukirudisha kutoka mavumbini
 
Kuna aina tatu za Viongozi wa kisiasa Barani Afrika, ikiwemo Tanzania.
1. #KUNDI_UKOMBOZI: Aina ya kwanza ni viongozi watetezi wa nchi, ambapo kwenye kundi hili ndipo utawakuta watetezi wa rasilimali za kiuchumi za nchi, utawakuta watetezi wa utawala wa demokrasia, utawakuta watetezi wa haki na usawa, utawakuta watetezi wa utawala wa sheria, utawakuta wanaharakati watetezi dhidi ya ukatili wa kijinsia, na utawakuta watetezi wa maendeleo wanaoguswa na shida, kero na matatizo ya wananchi.

Mara nyingi viongozi wenye kariba ya kundi hili, ni watu walionyooka, ni watu wasiokuwa na ndimi mbili kwa jambo moja, ni watu wasio kigeugeu. Kwao nyeusi ni nyeusi, na nyeupe ni nyeupe. Ni nadra kusikia kwamba, viongozi wa kundi hili wamehongwa, wamefika bei au kununulika na upande mwingine wa kisiasa. Ni aina ya viongozi ambao wako tayari kuyatoa maisha yao sadaka kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya nchi, pia kwa kile wanachokiamini.

Ni watu wanaochukia rushwa, ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya madaraka. Ni wafia Haki, Ukweli, na Uwazi. Ni viongozi ambao hutanguliza mbele maslahi ya taifa kuliko maslahi yao binafsi. Ni wapinga dhuluma, unyanyasaji, pamoja na ukandamizaji. Ni viongozi wanaopenda kuona matokeo chanya juu ya kile wanachokifanya, ikiwemo ustawi wa jamii wanayoiongoza. Kipaumbele cha viongozi wa kundi hili si cheo chao kwanza, wala maslahi yao kwanza, bali jamii kwanza, na nchi kwanza.

Kwenye kundi hili ndipo utawakuta watu kama hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, hayati Nelson Mandela, hayati Edward Moringe Sokoine, hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Tundu Antipas Mughwai Lissu, Luhaga Joelson Mpina, kwq kuwataja wachache...Unachopaswa kujua ni kwamba, aina hii ya viongozi wanaopatikana kwenye kundi hili si wengi kwa sababu Mungu huwaumba wachache, na hata hao wachache waliopo hupigwa vita kikweli kweli na makundi mengine wasipate nafasi za maamuzi kwenye Serikali.

2. #KUNDI_MASLAHI: Aina ya pili ya kundi la viongozi wa kisiasa, ni kundi maslahi kwanza, nchi na wananchi baadaye. Inaaminika kwamba, kundi hili ndilo kubwa kuliko makundi mengine yote. Ni kundi lenye nguvu kiuchumi kwa maana ya kumiliki ukwasi wa pesa. Ni kundi linaloamua kuhusu hatima ya nchi kwa kila kitu, kuanzia kiuchumi, kiutawala ikiwemo kupanga nafasi za uongozi, nani awe wapi na nani ashike wapi. Hili ndilo kundi linalomiliki rasilimali za kiuchumi za nchi kupitia mikataba ya kifisadi.

Ni kundi ambalo dhuluma, unyanyasaji na ukandamizaji ndiyo uti wa mgongo wa kundi hili. Kwenye kundi hili utawakuta aina ya viongozi wanaotetea dhuluma, wanaotetea ubadhirifu na wizi wa fedha za umma, wanaotetea rushwa na ufisadi. Aina hii ya viongozi wanaopatikana kwenye kundi hili utawakuta hata kwenye vyama pinzani, ambapo kipaumbele chao ni cheo kwanza ili wanufaike kwa pamoja na walioko kundi maslahi tawala, lakini wananchi baadaye.

Hili ni kundi ambalo katika mazingira fulani hutumia nguvu yake ya kiuchumi kuwanunua baadhi ya wanasiasa machachari walioko kundi ukombozi. Ukiona miongoni mwa viongozi wa kundi ukombozi wanazungumza kauli zinazofurahisha kundi madlahi, tambua tayari mvua imewanyeshea. Hali hiyo ilitumika kuisambaratisha NCCR Mageuzi, TLP, pamoja na CUF. Sasa ni zamu ya Chadema, ambapo, ninaamini, kundi ukombozi litavuka salama.

Kwao, swala la kudai na kupigania haki na usawa kwenye mifumo kandamizi ya kisiasa na kidemokrasia, ikiwemo ya uchaguzi , si hoja ya msingi, bali cha msingi kwao ni maslahi yao binafsi kwanza. Rejea kundi la Chadema linalojiita G.55 ambalo linadai uchaguzi uendelee katika mazingira yaliyopo bila kujali wanatambua kwamba mazingira si wezeshi kupatikana kwa haki. Hawa ndiyo viongozi maslahi ambao Watanzania tunapaswa kuwatambua popote watapogombea au kutia nia, wapigwe chini. Ni viongozi wenye tamaa na uchu wa madaraka kuliko maslahi mapana ya nchi ya wananchi wake.

Ni kundi ambalo lina mtandao mpana, kuanzia kwenye Chama tawala, Serikali, pamoja na taasisi zake, na wakati mwingine kutokana na nguvu ya ushawishi wake, lina uwezo hata wa kusababisha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pinzani kuacha mwelekeo wa sera na dira ya vyama vyao na kuwa mateka wa kundi hili kisiasa, ambapo na wao huanza kucheza ngoma kulingana na mdundo wa kundi hili unavyolia.

Kundi hili maslahi lina silaha nyingi za kuhakikisha maslahi yake hayakorofishwi, na miongoni mwa silaha hizo ni pamoja na kufanya mambo yake kwa usiri mkubwa. Silaha nyingine ni kuteka nguvu ya vyombo vya habari ili kuhakikisha habari zake chafu zinachujwa zisiwafikie wananchi. Silaha nyingine ni kutumia vyombo vya habari kufanya propaganda kwa mambo mazuri pekee, na inapotokea ukosoaji wa kulivua nguo kundi hili, silaha ya mwisho ni nguvu ya vyombo vya dola kutumika. Ni kundi ambalo liko tayari kufanya chochote ilimradi maslahi yake yasitikiswe.

3. #KUNDI_CHAWA: Aina ya tatu ya viongozi wa kisiasa ni wale wanaojiita Chawa. Aina ya viongozi walioko kwenye kundi hili, ni wale wanaocheza ngoma kulingana na mdundo unavyolia kwa wakati huo, pamoja na upepo unavyovuma. Hawa, huwa hawana kanuni maalum wala si wa kudumu. Ni kundi ambalo humshabikia aliyepo madarakani kwa wakati huo ilimradi mkono wao uwende kinywani, na pindi upepo unapobadilika, na wao hubadili gia angani mara moja.

Hili ni kundi ambalo kiongozi aliyeko kwenye kundi hili, akipewa nafasi ya kuzungumza mahali popote, kabla hajasema chochote, huanza na sifa za yule anayemfanyia uchawa. Lengo la kufanya hivyo ni kupalilia kitumbua chake, au kufikiriwa kupewa nafasi iwapo bado hajaingia kwenye mfumo.

Kundi linalojiita G.55 la Chadema linalodai kufanyika kwa uchaguzi licha ya kasoro kubwa zilizopo, ni kundi linaloonyesha kwamba liko upinzani lakini viongozi wana mafungamano na kundi maslahi la Serikali.

Nataka kuwaambia Watanzania kwamba, kupitia kundi hili sasa ndo tuanze kuchuja kati ya mchele ni upi na chuya ni zipi. Kanuni ya ukombozi wa nchi huwa haianzi na watu wengi, bali huanza na watu wachache. Tulio nyuma ya kundi la ukombozi tuendelee kupaza sauti ya kutaka mabadiliko, na lile kundi linalojiita G.55 ambalo kimwili linaonekana kuwa Chadema, kumbe kiroho liko ni wafuasi wa kundi maslahi, waondoke waende kule wanakoshabihiana.

Credit: Mkweru Zakaria Maswale FBView attachment 3296523View attachment 3296524
Lema yupo kundi gani
 
Umepambanua makundi yote kwa ustadi mkubwa. Tunaombea kundi la kwanza liwe na wengi kuliko makundi mengine.
 
Back
Top Bottom