Ikatokea ukapewa nafasi ya kukutana na rais Samia Suluhu Hassan

Ikatokea ukapewa nafasi ya kukutana na rais Samia Suluhu Hassan

Amepitisha nini? Umesikiliza lakini??
Mama D nisaheme bure kama nakukwaza ila hicho kwangu ndio kipimo pekee cha uzalendo wa Rais yeyote wa nchi hii. Vinginevyo naona "business as usual" tu. Hakuna jipya.
 
Hahahaaaaa akikujibu huoni Zahanati na Mabarabara kila kona?. Unataka mafanikio gani?
Zahanati na mabarabara si maendeleo ya watu.
Ni maendeleo ya vitu,huoni ukienda zahanati na kweny hayo mabarabara unatozwa pesa?

Hizo pesa watu watazitoa wapi kwaajili ya kulipia hizo zahanati na mabarabara?
 
Ningemuuliza baada ya kupata mkopo wa masharti nafuu wa corona ambao umeelekezwa kwenye kujenga madarasa mapya, zile fedha za tozo zilizokuwa hapo awali zinagawiwa kujengea madarasa haya zitaelekezwa wapi?

Amkumbushe Msigwa kwa kutumia kalamu kutuletea mtaalamu wa kero za muungano kama alivyo tuahidi ili atufafanulie na kuweka wazi kwa wananchi kero zilizo tatuliwa mpaka sasa na muafaka wake ulikuwa ni upi?

Akemee tabia hii ya kutaka kuonesha kuwa hatua zote zilizochukuliwa na mtangulizi wake hayati JPM kupambana na corona zilikuwa si sahihi. Afanye hivyo kuonesha kwamba yeye si sehemu ya wanaomzonga hayati kutaka kuonesha alikosea kwenye maamuzi yake yote juu ya kupambana na corona. Akikaa kimya na kuinyamazia tabia hii watu wengine wataona ya wezekana anawatuma hawa wanao endeleza huu upotoshaji.

Vitu vingine ni vikubwa na adhari zake zinakuwa kubwa vikinyamaziwa. Uko huu uvumi hapajF inawezekana na kwengineko, tetesi za kuanzishwa mchakato wa kisheria ili kubinafsishwa au kuuzwa shares baadhi za Tanesco. Si afya sana mambo kama haya kuyapotezea na kutosema lolote. Sio kila uvumi ni wa kupuuzia. Yako mengine lakini acha pengine wengine watayasemea.
 
Back
Top Bottom